MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 707
Ndugu Wananchi,
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 18-1, inatamka ifuatavyo:
Kwa mtazamo huu, tunavyoadhimisha Siku ya Uhuru wa Habari duniani, kwamba uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuta matangazo ya moja-kwa-moja ya vikao rasmi vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na, badala yake, kutayarisha kipindi ambacho kimehaririwa, ambacho kinahaririwa na kurushwa baadae kwenye kituo cha luninga cha TBC1, ni dhahiri kwamba Serikali IMEVUNJA KATIBA!
Kwa mujibu wa Katiba, Serikali inapata mamlaka ya kutawala nchi kama ifuatavyo:
8.- (1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo:
Bila KUMUNG’UNYA MANENO, ni dhahiri kwamba Serikali imekiuka Katiba kama ilivyoainishwa kwenye Ibara ya 9 na Ibara ya 18. SISI RAIA WA TANZANIA hatukuingia mkataba na Serikali ili ivunje haki zetu. Serikali inatudhulumu kwa kufanya maamuzi ambayo yake nje ya mamlaka yake; haina mamlaka ya kufanya uamuzi unaoingilia haki zetu za Kikatiba BILA KUTUSHIRIKISHA. Inaminya haki zetu, hususan haki ya “kupewa taarifa wakati wote kuhusumatukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii” kama ilivyoainishwa na Ibara ya 18.
Sasa umefika wakati – ambapo tumechelewa sana – wa sisi raia ambao ndio MSINGI WA MAMLAKA YOTE kuiwajibisha Serikali, kwa kuwa Serikali inawajibika kwetu sisi; SISI hatuwajibiki kwa Serikali.
Kwa kuwa Serikali – ambayo inawajibika kwetu – imeamua kukiuka mkataba uliopo kati yetu, ninapendekeza tufanye yafuatayo, baada ya muda wa saa 72 kukamilika, muda ambao ninapendekeza Serikali irudishe matangazo ya luninga ya moja-kwa-moja kupitia TBC 1, chombo cha habari kinachoendeshwa kwa kodi zetu. Mapendekezo yangu ni kama ifuatavyo:
Ndugu Wananchi, tambueni kwamba TUNAYO HAKI ya kufanya hivi bila kuvunja sheria, kwa kuwa SISI NDIO WAMILIKI WA SERIKALi! Serikali imeingia kwenye mkataba na raia wa Tanzania kupitia mkataba, na jambo hili limedhihirishwa kwenye Katiba kwamba “wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii” (Ibara ya 8-(1) (a). Kwa hiyo, ni dhahiri kwamba SISI WANANCHI ndio wamiliki wa MAMLAKA YOTE, na wanachofanya watendaji wa Serikali ni UASI; hawana mamlaka ya kufanya maamuzi makubwa yanayokiuka Katiba BILA KUTUSHIRIKISHA, kwa kuwa “Serikali itawajibika kwa wananchi.”
Tumekuwa wakimya KWA MUDA MREFU MNO! Sasa umefika wakati wa KUCHUKUA HATUA!
Tuna wajibu wa kudai haki zetu kwa kuwa, kama alivyosema William Hague, “Serikali zinazozuia azma za wananchi wake, zinazoiba na za kifisadi, zinazowanyanyasa na kuwatesa au kuwanyima uhuru wa mawazo na haki za kibinadamu, zinapaswa kuzingatia ukweli kwamba zitakuwa na wakati mgumu wa kukwepa hukumu itakayotolewa na wananchi enyewe, au, panapostahili, mikono ya sheria za kimataifa.”
#BungeLive
#UhuruWaHabari
#UhuruWaMawazo
Tushiriki zoezi hili la kudai haki zetu kwa kuweka sahihi zetu hapa
www.ipetitions.com/petition/bunge-live-now
================
TAMKO:
Sisi, raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunatumia haki yetu ya Kikatiba kutoa maoni yetu, kuhusu kitendo kiovu cha Serikali kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama ifuatavyo:
1.Kwa kuwa, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 18-2, inayosema "Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii",
2.Kwa kuwa, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 8(1)-a "wananchi ndio msingi wa MAMLAKA YOTE na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujubu wa Katiba hii",
3.Na kwa kuwa, kwa mujibu wa Katiba hii, "Ibara ya 8(1)-c, Serikali itawajibika kwa wananchi", na "(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii",
Tunatoa tamko lifuatalo:
1.Serikali imekiuka masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwanyima wananchi haki yao ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali mchini na duniani ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia, juu ya masuala muhimu kwa jamii, HUSUSAN matangazo ya moja kwa moja ya Vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2.Serikali imetoa kisingizio kwamba gharama za matangazo hayo ni Shilingi za Tanzania Bilioni 4 kwa mwaka, lakini imekataa kupokea michango ya gharama hizo kutoka kwa wananchi, bila kutoa sababu za kuridhisha, hata pale ambapo baadhi ya vyombo vya habari nchini vilipojitolea kubeba gharama hizo moja kwa moja na kutangaza matangazo hayo
Sisi Wananchi, raia wa Tanzania, tumeamua kufanya yafuatayo:
1.Tutaaacha kununua magazeti yanayochapishwa na vyombo vya habari vinavyosimamiwa na Serikali
2.Tutaacha kusikiliza vituo vya redio na luninga vinavyoendeshwa na Serikali
3.Tutafanya hivi kwa kipindi kisichopungua siku 30, baada ya muda usiopungua saa 72, ambazo tunaitaka Serikali iwe imerejesha mfumo wa matangazo ya moja kwa moja kupitia kituo cha luninga cha TBC1, ambacho kinaendeshwa kwa kodi za wananchi, yaani SISI, ambao kwa mujibu wa Katiba "ndio msingi wa MAMLAKA YOTE"!
Serikali yet IMEASI. Imetunyanyasa vya kutosha, imetupuuza vya kutosha, sasa tunasema, hatutanyanyaswa tena na hatutapuuzwa vya kutosha.
HITIMISHO:
Iwapo maendeleo ya kweli yanapaswa kufanyika, ni lazima wananchi wahusishwe! - Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Uhuru wa Mawazo
18.- (1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusumatukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.
(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusumatukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.
Kwa mtazamo huu, tunavyoadhimisha Siku ya Uhuru wa Habari duniani, kwamba uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuta matangazo ya moja-kwa-moja ya vikao rasmi vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na, badala yake, kutayarisha kipindi ambacho kimehaririwa, ambacho kinahaririwa na kurushwa baadae kwenye kituo cha luninga cha TBC1, ni dhahiri kwamba Serikali IMEVUNJA KATIBA!
Kwa mujibu wa Katiba, Serikali inapata mamlaka ya kutawala nchi kama ifuatavyo:
8.- (1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo:
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
Bila KUMUNG’UNYA MANENO, ni dhahiri kwamba Serikali imekiuka Katiba kama ilivyoainishwa kwenye Ibara ya 9 na Ibara ya 18. SISI RAIA WA TANZANIA hatukuingia mkataba na Serikali ili ivunje haki zetu. Serikali inatudhulumu kwa kufanya maamuzi ambayo yake nje ya mamlaka yake; haina mamlaka ya kufanya uamuzi unaoingilia haki zetu za Kikatiba BILA KUTUSHIRIKISHA. Inaminya haki zetu, hususan haki ya “kupewa taarifa wakati wote kuhusumatukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii” kama ilivyoainishwa na Ibara ya 18.
Sasa umefika wakati – ambapo tumechelewa sana – wa sisi raia ambao ndio MSINGI WA MAMLAKA YOTE kuiwajibisha Serikali, kwa kuwa Serikali inawajibika kwetu sisi; SISI hatuwajibiki kwa Serikali.
Kwa kuwa Serikali – ambayo inawajibika kwetu – imeamua kukiuka mkataba uliopo kati yetu, ninapendekeza tufanye yafuatayo, baada ya muda wa saa 72 kukamilika, muda ambao ninapendekeza Serikali irudishe matangazo ya luninga ya moja-kwa-moja kupitia TBC 1, chombo cha habari kinachoendeshwa kwa kodi zetu. Mapendekezo yangu ni kama ifuatavyo:
1. Kusitisha kununua magazeti yanayomilikiwa na Serikali, yaani “Habari Leo” na “Daily News”
2. Kusitisha kutazama na kusikiliza vituo vyote vya redio na luninga vya TBC 1, ambayo inasimamiwa KIMABAVU na Serikali; vituo hivyo ni TBC 1 na TBC 2; TBC Taifa, TBC FM na TBC International
3. Zoezi hili lifanyike kwa siku zisizopungua 30 (mwezi mmoja) hadi hapo Serikali itakaporejesha matangazo hayo ya Bunge ya moja-kwa-moja