Peter: Sihusiki P-Square kuvunjika

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,161
2,000
Peter-Okoye-300x294.jpg

NYOTA wa muziki nchini Nigeria ambaye alikuwa anaunda kundi la P-Square, Peter Okoye, ameweka wazi kuwa yeye si chanzo cha kundi hilo kuvunjika.

Kundi hilo kwa sasa limevunjika kwa madai kwamba kila mmoja alikuwa anafanya mambo kinyume na utaratibu na kila mmoja sasa anafanya kazi peke yake.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, mapacha hao walikuwa wanasherehekea siku yao ya kuzaliwa, lakini kila mmoja alionesha kusherehekea kivyake japokuwa Paul aliposti picha yao ya utotoni.

Taarifa zilisambaa kwenye mitandao kwamba Peter ndio chanzo cha kuvunjika kwa kundi hilo, lakini ametumia ukurasa wake wa Instagram na kukanusha taarifa hiyo.

“Nashangaa kuonekana kuwa mimi ndio mwenye kosa, hakuna ukweli wowote nadhani kosa langu ni kuweka wazi tofauti zetu, ila mimi si chanzo kama watu wanavyosema kwenye mitandao ya kijamii, lakini nashukuru kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa,” aliandika Peter.

Mtanzania
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,131
2,000
Huwezi kushindana na nature....

Awali, originally, Peter and Paul walikuwa mbegu moja ya Mzee Okoye! Ilipofika makazi mapya, mbegu ikagawanyika pasu kwa pasu akatokea Peter na Paul

Peter na Paul nao wakaunganika kimuziki,

Na hivi sasa wamegawanyika tena kama ambavyo mbegu iliyowatoa wao ilivyokuwa imegawanyika hapo kabla.
 
Kanye2016

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
2,074
2,000
Yeye alitaka kuwa recognized kama anaweza kutunga nyimbo na kuimba pia, sasa pacha wake na kaka yao wakakataa kwa kuwa hawakumuamini, akaona enough is enough kama haaminiwi kwa nn asifanye kazi akaonesha kipaji chake, na ndo alichofanya mpaka sasa anangoma mbili na zote ni hit songs town hapa
 
ney kush

JF-Expert Member
Feb 16, 2012
1,311

umetumia kigezo kipi kwamba ni hit song?
 
zugazuga na mimi

JF-Expert Member
Sep 13, 2017
243
225
Huwezi kushindana na nature....

Awali, originally, Peter and Paul walikuwa mbegu moja ya Mzee Okoye! Ilipofika makazi mapya, mbegu ikagawanyika pasu kwa pasu akatokea Peter na Paul

Peter na Paul nao wakaunganika kimuziki,

Na hivi sasa wamegawanyika tena kama ambavyo mbegu iliyowatoa wao ilivyokuwa imegawanyika hapo kabla.
dah
 
kifimbocheza_

JF-Expert Member
Jul 14, 2017
1,116
2,000
Yeye alitaka kuwa recognized kama anaweza kutunga nyimbo na kuimba pia, sasa pacha wake na kaka yao wakakataa kwa kuwa hawakumuamini, akaona enough is enough kama haaminiwi kwa nn asifanye kazi akaonesha kipaji chake, na ndo alichofanya mpaka sasa anangoma mbili na zote ni hit songs town hapa
Hivi nn maana ya hit song?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom