Peter Madeleka: Rais aliongea kwa uchungu sana watu kubambikiwa kesi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Peter Madeleka, amekosoa utendaji wa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na jeshi la polisi, akidai kuwa mchakato wa utoaji haki nchini umejaa migongano ya kisheria na matukio yanayovunja utu wa binadamu.

Soma: PostGE2025 - Rais Samia: Huko Mahabusu kuna watu hawana hatia, wanafungwa kwa kesi ya kubambikiwa tu


Akizungumza na Jambo TV leo, Januari 14, 2026, Madeleka amerejea kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa jana Jijini Dodoma kuhusu kukerwa na kesi za kubambikiwa. Madeleka amesema kama kauli hiyo ingechukuliwa kwa uzito wa kiutendaji, watu wote wenye kesi za uongo wangepaswa kuwa wameachiwa huru kufikia leo asubuhi.

Wakili huyo ametoa mifano ya kustaajabisha ya ukiukwaji wa taratibu, akitaja tukio la polisi kumpima mkojo mtuhumiwa wa kosa la "uchochezi," jambo ambalo amesema halina uhusiano wowote wa kisheria wala wa kitaalamu.

Your browser is not able to display this video.
 
Kauli hazitoshi, unakuja na solution
{Mimi nikiwa rais} nitakuja na solution maana problem inajulikana, what is missing is SOLUTION.
 
Kauli hazitoshi, unakuja na solution
{Mimi nikiwa rais} nitakuja na solution maana problem inajulikana, what is missing is SOLUTION.
Vinginevyo aulizwe anayeshikiliwa jela,atoa ushauri na suluhisho la tatizo la taifa hili!
 

Sasa basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…