Pete na heshima yake katika uhusiano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pete na heshima yake katika uhusiano

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mkwaruzo, Mar 1, 2011.

 1. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  "Leo ni siku ya pekee ambayo moyo wangu umeufanya uwe na furaha na amani ya ziada kutokana na matarajio mapya ya mapenzi yetu. Na hii ni kutokana na hatua yako ya kunivalisha pete ya utambulisho wa uchumba wetu. Nakuahidi utii wa uaminifu daima ndani ya penzi letu lote. Hivyo ni juu yetu kumuomba Mungu atufanyie wepesi katika kuifikia ndoa ambayo ndiyo lengo letu la kuanzishia maisha mapya yatakayotufanya kuwa familia mpya". Hayo yalikuwa ni
  maneno ya mrembo kwa mpendawa wake baada ya kuvalishwa pete ya uchumba.
  Ingawaje siyo utamaduni uliyorasmi katika jamii yetu kufuata mambo ya pete na maana zake ila kwa kiasi kikubwa tamaduni hiyo imekuwa ikitumika zaidi katika ndoa ambapo wenza wote wawili hushiriki katika kuvalishana pete hiyo (pete ya ndoa).
  Sasa kama mmejikubalisha kuufuata utamaduni huo (wa kuitumia pete kama inavyotakiwa kimaana) basi inakuaje mmoja kati yenu au nyote wawili mnakwenda kinyume na utaratibu huo tena kwa kujifichaficha ili kila mmoja asigundulike kwa mwenzie? Kitendo hicho kinatoa maana tofauti hasa ya kukosekana/kupungua uaminifu baina ya wanandoa au wachumba. Kwa mtazamo niliopata mimi kwa wanao fanya haya ni huu: 1)Ni kujiwekea urahisi katika mambo yao na kujiepushia masuali ambayo wanaweza kuyapata kuhusu pete hiyo ambayo kwayo yanaweza kuwa ni kikwazo katika kufikia lengo kwa yale wanayotaka kuyafanya.

  2) Ni kutaka kuwafurahisha wale wengine walionao kimapenzi pale wanapo onana na kuwaficha undani wao kuhusu uhusiano wao wa dhati waliyonao.

  Hili halipendezi kwasababu ni kitendo cha kumuondoshea
  heshima mwenzi wako. Hebu jiulize, heshima unapaswa
  kuiwekwa juu ya nani? Je ni juu
  ya pete unayoivua kabla ya kufanya uovu wako au ni kwa yule uliyeamua kuvalishana pete pamoja naye?

  Kama mnavyojua, kuvishwa pete si kuolewa, ndiyo vivyo hivyo basi hata kuivua pete si kuachana. Lakini hili la kuivua pete kwa kujifichaficha likitokea tena bila ya sababu za msingi, ni sawa na usaliti unaoupitisha ndani
  ya moyo wako kwa yule aliyekuvisha. Na kama kuna tatizo linalokufanya uivue/
  kushindwa kudumu nayo katika kuivaa, kwanini usimueleze mwenza wako?

  Binafsi, sitodiriki kwenda kinyume na maana halisi ya pete pale nitakapo jikubalisha kuivaa. Na yote hii ni kutokana na mapenzi ya dhati niliyonayo kwa yule ninayempenda. Wala sitoifanya migogoro itakayoweza kutokea kati yetu kuwa ndiyo sababu/ruhusa ya kuivua pete hiyo. Nitaithamini sawa na ninavyomthamini yule atakayenivalisha pete hiyo.
   
 2. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Aaaah unajua pete ina maana nyingi mie nilidhani ileeeeeee
   
 3. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hili halipendezi kwasababu ni kitendo cha kumuondoshea
  heshima mwenzi wako. Hebu jiulize, heshima unapaswa
  kuiwekwa juu ya nani? Je ni juu
  ya pete unayoivua kabla ya kufanya uovu wako au ni kwa yule uliyeamua kuvalishana pete pamoja naye?


  kwa hiyo wewe ukisalitiwa (cheated) na mpenzi wako huku amevaa pete yake mkononi kwako si issue kabisa coz to you heshima yako iko kwenye pete
   
 4. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35


  Heshima inatakiwa kuwepo ktk kila upande ndani ya mahusiano ikiwemo na ktk pete. Na usaliti ni ishu ila hapa sijaliongelea moja kwa moja hilo. Nilichoongelea hapa ni ile cheating inayoweza kufanywa juu ya pete ambayo kwa kiasi fulani inaweza kumtabulisha mtu yy ni nani kutokana na pete aliyonayo. Mfano, unahisi nini pale mke aliyekuwa anatumia pete, anaamua kuivua kila anapokuwa ktk mitoko yake? Si ni kujiekea mazingira ya uchochezi wa kutongozwa coz kati ya watongozaji, wapo wanaoona wake za watu ni kama sumu hivyo kutodili nao pale wanapojua kuwa anayetaka kumlia misere yupo ktk ndoa. Hivyo smtym huhoji juu ya uhalisia wa pete iliyovaliwa na mtu coz wapo wanaojikweza ktk uvaaji wa pete
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  yale yale ya sanamu!
   
 6. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkwaruzo bana tumekubalianaje kule jana???

  Hebu fata ushauri ule basi.
   
 7. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  dah, nimejitahidi lkn nitapunguza tena zaidi. Unajua hii scrin ya simu inanihadaa coz siwezi kuiona kazi yote hadi baada ya kuiposti. Lkn nitapunguza tena zaidi.
   
 8. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sawa bana nimekuona mahala fulani umenichokoza
   
 9. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  usijali utanizoeya
   
Loading...