PETE (hadithi ya mapenzi)

PETE (hadithi ya mapenzi)

Ni Frank au Victor? Ametajwa Frank mwanzoni na victor baadae. Nadhani Victor itatoa ubishi!
Mwisho wa hii hadithi mmmmhh! Na tungoje
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Hata hivyo inategemea msomaji,
Kivyangu nikisoma mwanzoni nakuwa nimeshajua
mwisho itakuwaje, so wala situmii muda kuendelea kuperuzi.

Frank vs Victor...!!! Naomba uendelee kutumia Frank tafadhali...


In other news: Chaichungu i hate you kwa kuleta hii style ya kusimulia hadithi huku JF..hata mi ntaianza ingawa inakeraaaaaaaaa...na kwakuwa siez kereka mwenyewe ngoja niite wafuasi:
mwallu, KakaKiiza, Asprin, MziziMkavu, The Boss, Heaven on Earth, mwekundu, Mashaxizo, Mamndenyi, et al...
 
Last edited by a moderator:
Kutokana na PM nyingi Tunaendelea......samahani kwa kuchanganganya jina ninatumia la frank.
Baada ya frank kushika pete aliiangalia na kuiona nzuri ya duara na iliyopambwa kwa majina maua mazuri.akamsifia suzy na kumwambia pete nzuri na ya gharama na akamrudishia suzy.suzy akasema ndiyo ni ya gharama kama penzi lake kwangu.Franka kacheka.mda huo basi likawa linakimbia mida ya saa 1 walikuwa wanaingia shinyanga.taa za ndani ya basi zikawashwa na abiria wakawa wanashuka waliofika.kuiingia stendi ya shinyanga ya zamani kulikuwa na tuta basi likalusha watu.pete ambayo suzy alikuwa ameiweka mapajani kwa kuwa alikuwa anaogopa kuivaa wakati anataka atoke kwenye basi ili ashuke kujinyoosha kidogo wakati abiria wengine wakishuka.ikadondoka kutokana na tuta na kutereza hadi kwenye mfuko wa mzee mmja aliyekuwa ameuweka chini ili ashuke na ikakaa mdomoni mwa mfuko yule mzee akanyanyua mfuko na pete kuingia ndani ya mfuko.kuna bibi aliona yote akaanza kuongea kwa kisukuma kwa nguvu watu akiwa suzy na Frank wakageuka na kumwangalia.yule bibi akamfuata suzy na kuanza kumvuta.mkaka mmja anayejua kisukuma akamfuata suzy na kumtafsria.suzy akahamaki na kushuka amfuate yule mzee ambaye alikuwa ameshashuka.Frank nae akashuka kumsaidia suzy.konda akawaambia yule mzee ashachukua mizigo yake na kupanda landcruiser ya daladala.iliyoondoka.walipoulizia wakaambiwa inaelekea maswa.suzy akawa na hudhuni ajue afanye nini kwa maana hiyo ndo gari ya mwisho kwenda maswa.na ni mbali hadi bodaboda wakakataa kuifukuzia,akaamua ashushe mizigo yake yote na kuomba jina la yule mzee na namba yake waliyokuwa wameaandika kwenye tiketi ili kesho yake amfuatilie.alipojaribu kupiga simu ya yule mzee kwa namba alizopewa na konda ikawa haipatikani.Frank akamwangalia kwa huzuni na huruma na kumtakia mema kwa safari ya kumtafuta yule mzee kesho yake
Konda akamwambia frank basi linaondoka na Frank akapanda basi.suzy aliliangalia basi likitoka stendi huku ajui afanye nini au aanzie wapi kwa sababu ni mgeni hapa na safari yake ni kufika mwanzw kwa mpenzi wake.ghafla basi likasimama na akaona mtu ameshuka akiwa amebeba begi.kutokana na giza hakumuona vizuri ila yule mtu aliposogea akajua ni frank.akashangaa na kuuliza"nilizani unaenda mwanza?"ndiyo.ila kwakuwa naenda kupumzika nqzani hadi hapa shinyanga naweza nikiwa namsaidia mdada kuokoa penzi lake kwa pete."haha alicheka kidogo suzy.asante sana.na kusema kwa sauti ya chini.ok karibu akajibu frank..tutafute sehemu ya kulala hslafu kesho tumtafute huyo mzee au?akauliza frank.poa kwa maana hata apatikani kwenye simu yake itakuwa la muhimu.wakapanda tax na kutafuta gesti.bahati mbaya kila gesti waliyoenda ikawa imejaa wakabahatisha moja iliyokuwa ina chumba kimoja tu na kitanda kimoja yenye kila kitu ndani wakakubali kuchukua chumba hicho kwa maana walikuwa wamechoka.walipofika chumbani wakakubaliana kulala kitanda kimoja.tunaweka mto kati hamna mtu kuvuka sawa?sawa hata tukiweka mabegi mi poa tu.akajibu Frank.wote wakatabasamu
Kila mtu akajiandaa kulala kwa kuoga kwa zamu na mda walipomaliza wakajiweka kitandani na kuanza kuutafuta usingizi.usiku mwema"wakasema kwa pamoja na kucheka ha ya usiku mwema"wote wakasema huku wakigeuka upande wake na kumpa mwenzie mgongo huku kila mtu akiitafakari kesho
ITAENDELEA LEO USIKU
 
Back
Top Bottom