Pesa zimepotea au zimepotezwa

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,335
2,000
Rais JPM mara nyingi husema watu wataishi kama mashetani na hivi karibuni amesema kuwa sadaka nazo zitapungua na wanaoumia ni watu wa madili.
Upo uwezekano kuwa Magufuli amedhibiti mianya ya ubadhirifu. Lakini je, hali hii ya uchumi nini kimetusababisha?
Kama kweli Magufuli amedhibiti matumizi mabaya ya fedha;
  • Miradi mingi ingeshika kasi
  • Ajira zingeshamiri serikalini
  • Biashara zingepamba moto.
  • Makusanyo ya kodi yangeongezeka
Lakini uhalisia maneno yake yanatofatiana na hali halisi. Ikumbukukwe serikali ilipitisha bajeti ya trillioni 29. Bajeti ilitegemea makusanyo ya kodi na vyanzo vingine vya serikali, misaada na mikopo ya masharti nafuu.
Kiuhalisia makusanyo yanasuasa kama ambavyo Waziri wa Fedha alikiri kupitia taarifa yake ya mwezi December na viashiria vya kwenye mabenki vipo dhahiri. Wastani wa misaada na mikopo, ni asilimia 20%.
Kwa ujumla tumekwama. Mkwamo huu JPM ni sababu kwa sera za kiuchumi na si sababu kwa kuwa ni mahiri wa kupambana na ufisadi. Hii ni kwa sababu, kama pesa zingekuwepo na zimetolewa kwa walafi, basi hawa wengine wangeona hayo matunda.
Lakini kiuhalisia biashara zinafungwa, mabenki yanatetereka na hata wale wapiga dili "kina mama ntilie, dereva wa bodaboda nk" nao wanataabika.
Tujitazame kabla hatujakwama zaidi.
Maneno ya masharti magumu yaliyotajwa na Mh Waziri wa fedha si mapya. Lakini ni mashartii gani hayo mpaka nchi iyumbe? Au tulipanga bajeti tusioiweza?
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
76,065
2,000
Usicheze na wazungu mkuu , wakiziba misaada haina tofauti na kuziba pumzi .

Halafu nchi hii sasa hivi imedharauliwa vibaya sana ! Usipime !
 

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,335
2,000
Usicheze na wazungu mkuu , wakiziba misaada haina tofauti na kuziba pumzi .

Halafu nchi hii sasa hivi imedharauliwa vibaya sana ! Usipime !
Mengi yanaongeleka na kubadilika. Kwenye diplomasia huwa hakuna ubabe. Tupange mipango kama nchi na tufahamu muelekeo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom