Pesa za maendeleo mashuleni sasa kupelekwa moja kwa moja kwenye mfuko wa shule.

mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,913
916
Wakuu amani kwenu,

kwangu mimi hii naiona imekaa vema,serikali imetangaza kwamba kuanzia sasa pesa za maendeleo katika shule hazitapitia tena kwenye acounti za halmashauri kama ilivyokuwa zamani badala yake serikali imeamua pesa hizo zitawekwa moja kwa moja kwenye acount za shule husika.

Hali hii itapunguza mzunguko wa kupata pesa hizo lakini pia itaziba mianya ya ulaji wa pesa hizo uliokuwa unafanywa na baadhi ya watendaji wa halmashauri wasiokuwa waaminifu.

chanzo; taarifa za habari saa mbili usiku ITV na TBC.
 
Sasa kitanzi kinaongezeka kwa wezi wa pesa za umma sijui wataiba vipi kila sehemu serikali inabana safi sana kawambwa na wenzako umethubutu mmeweza na sasa mnasonga mbele.
 
Uamuzi huu unechelewa mno, anyway niwaponveze angalau kwa hili.

Shule nyingi mf hapa Tdm zimejengwa na wananchi wenyewe, Madawati yamenunuliwa na wananchi wenyewe. Cha ajabu serikali ilitaka hata vitabu vinunuliwe na wanfunzi au wazazi wao wenyewe. Ukiuliza kunafedha za Maendeleo zinazofika shuleni walimu wanasema hamna. Michango ya sh mia mia au miambili kila siku ilikuwa haikomi, ingawaje sina hakika kama kweli serikali ilikuwa ikitenga kweli fedha husika lakini kwa mpango huu niwapongeze.

Ila ni lazima Tuangalie namna ya kubana mianya ya ulaji wa fedha husika. Isije kuwa tunahamisha ULAJI toka halmashauri mpaka kwa Wakuu wa Shule. Ni lazima serikali ijipange namna ya kufuatilia fedha hizo

BACK TANGANYIKA
 
Umetoa hoja ya msingi sana,ni juu ya wahusika kuja na huo mkakatwakuwabana wakuu wa shule,maana isije kua unahamisha huku kumbe na huku kuna walaji wengine,ingawa huku shuleni kuna kamati za shule ,labda wao wakiwa wajanja wanaweza kumbana mkuu wa shule na kumuuliza juu ya pesa hizo.

n
Uamuzi huu unechelewa mno, anyway niwaponveze angalau kwa hili.

Shule nyingi mf hapa Tdm zimejengwa na wananchi wenyewe, Madawati yamenunuliwa na wananchi wenyewe. Cha ajabu serikali ilitaka hata vitabu vinunuliwe na wanfunzi au wazazi wao wenyewe. Ukiuliza kunafedha za Maendeleo zinazofika shuleni walimu wanasema hamna. Michango ya sh mia mia au miambili kila siku ilikuwa haikomi, ingawaje sina hakika kama kweli serikali ilikuwa ikitenga kweli fedha husika lakini kwa mpango huu niwapongeze.

Ila ni lazima Tuangalie namna ya kubana mianya ya ulaji wa fedha husika. Isije kuwa tunahamisha ULAJI toka halmashauri mpaka kwa Wakuu wa Shule. Ni lazima serikali ijipange namna ya kufuatilia fedha hizo

BACK TANGANYIKA
 
Wakuu amani kwenu,

kwangu mimi hii naiona imekaa vema,serikali imetangaza kwamba kuanzia sasa pesa za maendeleo katika shule hazitapitia tena kwenye acounti za halmashauri kama ilivyokuwa zamani badala yake serikali imeamua pesa hizo zitawekwa moja kwa moja kwenye acount za shule husika.

Hali hii itapunguza mzunguko wa kupata pesa hizo lakini pia itaziba mianya ya ulaji wa pesa hizo uliokuwa unafanywa na baadhi ya watendaji wa halmashauri wasiokuwa waaminifu.

chanzo; taarifa za habari saa mbili usiku ITV na TBC.

hiyo ni kutekeleza uamuzi wa kusomesha bure mpaka f4 kuanzia mwakani, lakini umesikia upande wa vyuo vikuu? wanafunzi 20,000 watakosa mikopo ya elimu ya juu!
 
Back
Top Bottom