Pesa ya elimu ya Bure zaweza kuwa kiama huko zinakopelekwa

NJALI

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
1,534
1,090
ELIMU ni moja ya sekta zinazotoa huduma hapa nchini Tanzania, ELIMU haizalishi kupata FAIDA kana TPDC, EURA, NHC n.k. Hivi karibuni serikali yetu sikivu ilitangazia umma wa watanzania kuwa kuanzia January ELIMU ya Msingi na sekondari ya kawaida itakuwa bure KWA SHULE zote za umma.

Hapo nikiwa mwalimu naipongeza serikali KWA kuwapunguzia watanzania wenzangu mzigo WA ada na msululu wa michango shuleni.

TATIZO
Ni kwa jinsi gani sirikali imejipanga kuhakikisha kuwa PESA hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ?
Kama mnakumbuka Prof Kikwete akiwa bado Rais aliwahi kuzilalamikia Halmashauri kuwa ni mchwa unaokula PESA za walipakodi zinazotumwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Mbaya zaidi kipindi hayo yanatokea waziri mkuu wa sasa alikuwa Naibu waziri WA TAMISEMI ambao ndio wasimamizi wakuu WA miradi hiyo.

Je serikali imeshaandaa dawa ya kuua mchwa huyo ? Au inangoja mchwa ule PESA ndio iuangamize ? Je mchwa utakao bainika umekula PESA unachukuliwa hatua zipi ?
 
Yaani we bado tu unalinganisha awamu hii na ya mkwere

Au hukumsikia Magufuli alichosema nini, au unadhani naye ni wa kucheka cheka kama mkwere, We subiri uone atakayethubutu kuila hiyo hela ndo atamjua vizuri Magufuli
 
Rais esema pesa inapelekwa kwenye bank account ya shule moja kwa moja na siyo halmashauri. Ili mkuu wa shule aweze kusimamiwa kila pesa ikipelekwa shuleni mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya na mkuregenzi wa wilaya wanapata nakala ya nini kimeenda kila shule. Kwahiyo hapo kuna mtu mmoja tu atakayekuwa responsible...mkuu wa shule. Ninavyojua hizo shule zina bodi na lazima katika manunuzi mkuu wa shule atahusisha board.
 
Hizi bodi si ndo zikikaa zina jilipa mamilioni na hizi hiz ndio wanakuwa na tenda humo humo shuleni kama ya stationary na madawati
 
Hizi bodi si ndo zikikaa zina jilipa mamilioni na hizi hiz ndio wanakuwa na tenda humo humo shuleni kama ya stationary na madawati

Ndo maana wamewekewa watchdog...mkurugenzi, DC na RC kwa kuwapa nakala. Hawatafanya bila kufuatiliwa. Kwa vyovyote vile lazima kazi zifanyike maana utasema halmashauri nao ni mchwa. Ni afadhali kuwaondoa halmashauri katika kishika pesa ili wasimamie shule vizuri.
 
Sawa nimependa michango yenu let us Waite and see, time will tell.
 
Fedha ikipita kwenye mikono mingi ni shida na wakuu wa hizo shule wasiposimamiwa vizuri ni shida!
 
Hizi bodi si ndo zikikaa zina jilipa mamilioni na hizi hiz ndio wanakuwa na tenda humo humo shuleni kama ya stationary na madawati

Mpaka wanafunzi wanapata huduma, itakuwa July 2016, na Desemba 2016 kesi za wasiofuata taratibu za manunuzi. Januari 2017 walimu wengi watakuwa watoro wanakimbia mkono wa sheria. Take my word.
 
Hizi bodi si ndo zikikaa zina jilipa mamilioni na hizi hiz ndio wanakuwa na tenda humo humo shuleni kama ya stationary na madawati

Shule haina board, ina kamati ya kuratibu shughuli zote. Watakaobainika kuibia serikali watafungwa na wengine watajifunza. Halmashauri zinanuka rushwa fedha haziendi kwa wakati na bank transaction charges toka hazina kwenda tamisemi then halmashauri then kwenye account za shule zinacost pia.
 
Wewe nawe wa wapi?

Kamati ziko shule za msingi tu, lakini sekondari huko kuna bodi ya shule!!
 
Mimi nashauri,signatory mmoja awe ofisa wa takukuru,dso,au mkurugenz,wanapoandka muhtasar wakmalza,hao maafsa wasain

Watakosa meno ya kuwang'ata, wewe inaonesha ni mgeni kwenye adminstration and procurement.
Takukuru na dso wawajibike fedha zikiliwa bila wao kuzuia. Lengo ni kuthibiti siyo kufunga walimu pingu.
 
Back
Top Bottom