Nipo chuo Nina mpango wa kufanya biashara lakini biashara hii nahitaji chumba, kwa wiki natumiwa tsh elfu 40, nipo mkoa mgumu katika kupata mahitaji nikimaanisha vitu bei ghali.
Sasa jamani kila Jumapili natumiwa Pesa tajwa hapo juu lakini kila ikija ijumaa au Jumamosi lazima nikope watu ela ya kula, ela huisha katikati haifiki Jumapili, kwa nilivyojifatilia nimeona Vocha inamaliza sana ela hasa kwa upande wa bando lakini sio bando tu kila ifikapo Jumapili nanunua kila kitu ambacho sina. Maradhi kwa ujumla lakini utakuta katika 40 always nabakiwa na 20 tu, 20 inakuwa imetumika kununua vitu ambavyo sina mf. Viatu, pafyumx, lotions, sabuni, kulipa madeni kwa wanaonidai etc.
Always inabaki humo kama sio 20 basi 18_16, sasa saizi Nina mpango wa kupunguza matumizi ili nilipie chumba cha biashara na niazishe biashara ndogo iweze kunipa faida niweze kuendesha maisha baada ya chuo na nipo semi ya mwisho. Sijui nitaweza!!!!!!!!!