Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 10,884
- 18,824
Pesa ina historia ndefu sana lakini leo napenda tujadili status iliyonayo pesa leo.
1. Pesa kama pesa haina thamani yeyote, ni makaratasi tu. Thamani ya pesa inatokana na wananchi kuamini kuwa ina thamani na serikali kutunga sheria kuwalazimisha watu kukubali kuwa pesa ina thamani. Ndiyo maana kwenye pesa kuna maandishi 'fedha halali kwa malipo ya Shilingi.....' Fikiria mfano huu, Tanzania kuna watu 60m na wanaiamini na kuithamini Tsh. Rwanda wana watu 11m nao wanaiamini na kuithamini pesa yao. Kuna nchi zina watu 2m na zingine laki kadhaa na nchi nyingine zina watu elfu kadhaa. Shuka hivyo hadi upate kuwa kila familia ya watu kadhaa ni nchi. Sasa kila familia(nchi) itengeneze pesa yake. Familia A hawezi kwenda kwa familia B kununua mbuzi au ng'ombe kwa kutumia pesa yake sababu familia B hawaiamini, nao wana pesa yao, familia C nao wanayo yao na D nao wanayo yao. Imani ndiyo inaipa pesa thamani.
Kwa hiyo ukienda kwenye kiini kabisa, pesa tunazotumia sasa ni makaratasi matupu na ndiyo maana watu wakipoteza imani nazo huwa zinashuka thamani kwa kasi
2. Serikali huwa zinatengeneza pesa hizo kutoka hewani tu.
Kuna kipindi Iddi Amin(RIP) aliambiwa kuwa nchi imepigika haina hela za kulipa mishahara yeye akawajibu "kachapisheni muwalipe" zamani nilimuona mjinga lakini kumbe ndivyo mambo yalivyo. Serikali huchapisha pesa zinavyojisikia bila kuulizwa na yeyote. Pengine ili kuepuka hili ndiyo maana wanasema benki kuu ya Marekani haimilikiwi na serikali. Serikali haiwezi kuwa kwenye shida halafu inauwezo wa kuchapisha pesa na isichapishe. Kuchapisha kupita kiasi kunaweza leta inflation lakini mara nyingi serikali za kidemokrasia hazijali hayo.
3. Serikali zinatengeneza pesa kutoka hewani kisha zinatukopesha kwa riba.
Baada ya serikali kutengeneza pesa kutoka kwa hewa wanazikopesha benki. Benki nazo wanakopesha watu. Kwa hiyo kama benki kuu/ serikali inachaji riba ya 10% benki iliyokopeshwa bilioni moja itatakiwa kurudisha bilioni moja na milioni 100. Kama benki nao wanaenda kukopesha wananchi kwa asilimia 20 maana yake wananchi watatakiwa kurudisha Tsh bilioni 1.2. sasa jiulize hii milioni 200 imetoka wapi? Yaani unaingiza noti za elfu kumikumi laki moja halafu unataka zirudi laki moja na ishirini, hizi noti elfu ishirini zinatoka wapi? Hapa ndiyo maana watu hufirisika na dhamana zao kuuzwa, ni kama upatu mmoja mkubwa.
Tujadili.