Utabakia kuwa Tomasso hivyo hivyo; kwani huna habari kuwa hizi noti contena zima ziliibiwa kabla ya kuanza kutumika kisheria!! Unafikiri wabongo walizifanyia nini, walizipikia ugali?
Mimi niseme sijui ni mshamba ama macho yangu yameona vibayaa.Jamani pesa mpya sijui wanajamii forum mnazionajee?pesa ni nyepesi sidhani kama zitamudu life la bongo,ndo maana nikasema mi sijui ni mshamba ama sijaona vizuri naomba maoni yenu
Hujamaliza sema zinachuja rangi. Huwezi weka kwenye mfuko wa shati has shati jeupe. Nadhani kunahitajika tume kuchunguza mchakato mzima wa utoaji zabuni na kama viwango vya ubora vilivyoainishwa kwenye mkataba vimezingatiwa. Zimesifiwa kwenye TV kumbe ni uchafu mtupu bora za zamani
Labda wazungu kwani wana historia ya uungwana. Lakini wanaotunyemelea ni wahindi, waarabu na wachina, nao si waungwana hata kidogo. Swala la kutawaliwa tena na wazungu waungwana haliko. Kilichoko ni kutawaliwa na matapeli, mijizi na miuza unga kutoka kote duniani wakishirikiana na hawa akina Mangungo wa ndani ya nchi, ili mradi wao wapate hapo tu vijisenti vya kufurahisha nafsi yao.