Pesa hutoka wapi!?

Pesa hutoka wapi!?

Voxwiser

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2017
Posts
1,094
Reaction score
1,360
Habari ya jioni wakuu
Natumaini nyote niwazima

Mimi nlikua naswali kidogo naliwaza..... Wakati naendelea kutafuta majibu ndipo nlipokumbuka darasa langu pendwa la jamii forum

Swali langu je ni nani anaetengeneza pesa.... Na baada yakutengenezwa hupewa nani au huingizwa vipi kwenye mipangilio ya matumizi... Na hutengenezwa kwa utaratibu upi... Na nani anaetoa utaratibu wakuzitengeneza
Kwnini anaetengeneza asitengeneze nyingi azimwage tuu(najaribu kuwaza)
Je kunasheria yoyote ya pesa!?

Natanguliza shukrani kwa elimu mtakayo nipa
 
mimi sio mchumi wala sijasomea masuala ya fedha ila the way uchumi unavyo ongezeka yaan kuingiza fedha za kigeni basi tunapata nafasi ya kutengeza pesa mpya kulingana na pesa za kigeni tulizo pata lakini kumbuka tutatoa pesa tulizo agiza bidhaa nje ile faida inayobaki ndo tunapata nafasi ya kutengenezewa pesa mpya kwenye kampuni zinazohusika zenye uthibitisho kutoka (IMF), kuna kampuni maalumu zinazotambuliwa na mamlaka za fedha duniani, ikitumika ujanja wowote wa kuprint pesa pasipokupitia process ya kuipata katika service na goods basi uchumi wa nchi utaporomoka hatari, mfano zimbabwe kuna wakati pesa yao haikua na thamani kabisa mpaka imebidi watumie dollar.
 
Habari ya jioni wakuu
Natumaini nyote niwazima

Mimi nlikua naswali kidogo naliwaza..... Wakati naendelea kutafuta majibu ndipo nlipokumbuka darasa langu pendwa la jamii forum

Swali langu je ni nani anaetengeneza pesa.... Na baada yakutengenezwa hupewa nani au huingizwa vipi kwenye mipangilio ya matumizi... Na hutengenezwa kwa utaratibu upi... Na nani anaetoa utaratibu wakuzitengeneza
Kwnini anaetengeneza asitengeneze nyingi azimwage tuu(najaribu kuwaza)
Je kunasheria yoyote ya pesa!?

Natanguliza shukrani kwa elimu mtakayo nipa
Swali zuri.
Nitaeleza kwa ufupi.
Utengenezaji wa fedha ni jambo la kihistoria, na lina historia ndefu.
Kabla ilikuwa biashara ya kubadilshana, baaae ikaonekana kuna umuhimu wa kuhifadhi thamani ya huduma na vitu.
Katika hilo dhahabu ilitumika ilitumika zaidi wakati huo, ie ukitoa huduma au kuuza bidhaa unapewa dhahabu.
Baadae likaja suala au changamoto ya kuhifadhi hizo dhahabu, ndipo mabenki yalipoanza.
Unapopeleka dhahabu kuhifadhi kwa mhifadhi mwenye facility (benki) unapewa risiti sawa na kiasi cha dhahabu ulichohifadhi.
Hizi risiti watu walizitumia kununua vitu na kulipana kwa huduma mbalimbali.
Hizi risiti ndio fedha.
Kwa sasa Benki Kuu ndio inatengeneza fedha kwa kutumia wazabuni.
Inatengeneza kulingana na hitajio la mabenki inayohudumia ie uchumi.
Itaendelea...
 
Mi sielewi wanaposema pesa flan imeshuka thamani....au dola imepanda sijui....naomba nieleweshwe hapo tafadhali
 
najibu swali la pili @ kwanini wasichapishe manoti mengi watu tule bata?
kwanza benk kuu wao ndo wenye majukumu ya ku issue new currency, kwa hiyo wanaogopa kufanya hivyo kwa sababu hela itaongeza mtaani ( increasing of money suupply) na hela ikiongeza kila mtu anayo, itafanya money circulation iongeze ( mzunguko wa pesa utaongezeka) ikiwa hivyo vitu vitashuka bei ( fall in price au deflation ) hii itawaua nguvu producer..kwa hiyo tutakosa huduma sasa benk kuu wakiona hivyo itabidi watumie monetary tools ili kuitoa hela mtaani kwa kuuza hisa zake au security zozote ili hela itoke mtaani mambo yakae sawa. na hela ikiwa nyingi mtaani ndo inakuwa DEPRECIATION lakini hii sanasana ni baina ya nchi na nchi... haina thamani tena kila mtu anayo...refer zimbabwe walivyoamua kuchapisha hela zao wenyewe. kama nipo wrong mnirekebishe wachumi wezangu. ( jibu hili nimelijibu kitaalam)

ila swali la pili hela inatengenezwa wapi kwanini watengeneze NASKIA USWISS serikali inapeleka gold zinathaminishwa kwa value ya hela utakayopata then wanakuchapia mzigo unaotaka kama unataka kutoa mia tano za noti uwekewe za sarafu unawaambia hapohapo dizaini ya mkwanja wako kama unataka ikae sura yangu hapo hapo unawaambia ( HILI JIBU NI ELIMU KITAA TU SIO LA KITAALAM)
 
@travellwr asante naendeleA kujifunza
Hivyo ili utengenezeww hera lazima uwe na kitu chaku exchange nayo!?
 
Back
Top Bottom