britanicca
JF-Expert Member
- May 20, 2015
- 16,288
- 33,948
Nimefuatilia kupitia YouTube yanayoendelea huko Tanzania, hasa kwenye ziara za mkuu wa nchi,
Napenda jinsi anavyoonekana kuguswa na matatizo ya watanzania hasa wanaomlilia,
Kuna kina mama wengi wameonewa, kuna watoto yatima na maskini wanaonewa na kudhulumiwa,
Nimeona video zao zinasikitisha
Mpaka machozi yanaweza kutoka,
Rais kusema kweli
Nimefurahishwa na kitendo chake kuwafariji wajane naa wazee wanaonyanyasika kwa kuwagawia Hela moja kwa moja,
Nina maswali machache
1. Hela hiyo inakuwa imeidhinishwa na nani mpaka kuigawa hivo? Au tutegemee mwaka mwingine C.A.G kutaja trillion nyingine ambayo haionekani imeenda wapi?
2. Au ni makato ya mshahara wake na aliowateua katika kutumia mishahara yao kutatua matatizo ya wanyonge? Maana kwa taarifa zisizo rasmi rais Ana posho ya 15,000,000 kila mwezi, hivo kama anatumia mshahara wake hakuna shida,
3. Je Rais hujui kwamba wajane na watu wenye matatizo kama ya hao unaowapa hela wapo chungu nzima Tanzania??
Na so wote watapata fursa ya kukutana na wewe kukueleza, wengine hautafika maeneo walipo,
4. Vipi usalama wa huyo unayemkabidhi Hela hadharani, si atavamiwa?
Pendekezo langu
A. Uwepo mfuko maalumu wa kuwasaidia watu hawa nchi nzima kama TASAFF walivokuwa wanasaidia wazee kuliko kugawa tu Hela mkononi, maana hata ambao hutawafikia watafikiwa kama sheria na utaratibu wa mfuko ulioanzishwa itafuatwa,
B. Viongozi wawajibike wasisubiri ziara ya rais ndo wanaanza kuhaha na kujifanya wanachapa kazi wakati kama wangekuwa wanachapa kazi matatizo kama hayo yangepungua kabisa,
C. Rais wangu angaza watu wanaokiuka na kuwanyanywasa wajane kiwepo kitengo maalumu kila.wilaya cha kusikiliza kero hizo, au ianze mahakama ya kutetea wanyonge kama ilivyo ya mafisadi,
Mwisho mi sijapendezwa na utaratibu wa kugawa hela mkononi, maana unapompa huyo mjane au kipofu unamuweka katika hatari zaid ya kuvamiwa usiku na majambazi kuzichukua Hela ulizompa, angalau ungekua unawapa kwa siri, japo najua kwa siri haitakupa sifa kama lengo lilivyo,
Britannica

Mkuu mleta mada, rais analo fungu la mengineyo, linafika milioni 100 kwa mwezi. Inategemea na aina ya maisha ya mtu mwenyewe.
Marais wengine hizi fedha walikuwa wananunulia masuti na kuhonga madada warembo wa mijini. Wengine ndio aina ya Ngosha, anashiriki moja kwa moja kwenye kuchangia mambo mbalimbali.
3. Je Rais hujui kwamba wajane na watu wenye matatizo kama ya hao unaowapa hela wapo chungu nzima Tanzania??
Na so wote watapata fursa ya kukutana na wewe kukueleza, wengine hautafika maeneo walipo,
4. Vipi usalama wa huyo unayemkabidhi Hela hadharani, si atavamiwa?
Pendekezo langu
A. Uwepo mfuko maalumu wa kuwasaidia watu hawa nchi nzima kama TASAFF walivokuwa wanasaidia wazee kuliko kugawa tu Hela mkononi, maana hata ambao hutawafikia watafikiwa kama sheria na utaratibu wa mfuko ulioanzishwa itafuatwa,
B. Viongozi wawajibike wasisubiri ziara ya rais ndo wanaanza kuhaha na kujifanya wanachapa kazi wakati kama wangekuwa wanachapa kazi matatizo kama hayo yangepungua kabisa,
C. Rais wangu angaza watu wanaokiuka na kuwanyanywasa wajane kiwepo kitengo maalumu kila.wilaya cha kusikiliza kero hizo, au ianze mahakama ya kutetea wanyonge kama ilivyo ya mafisadi,
Mwisho mi sijapendezwa na utaratibu wa kugawa hela mkononi, maana unapompa huyo mjane au kipofu unamuweka katika hatari zaid ya kuvamiwa usiku na majambazi kuzichukua Hela ulizompa, angalau ungekua unawapa kwa siri, japo najua kwa siri haitakupa sifa kama lengo lilivyo,
Britannica
Hapo jana iliripotiwa kwamba Rais Magufuli kamlipia faini Mchungaji Msigwa, ambaye mbunge wa CHADEMA kutoka huko Iringa.
Alimlipia shilingi milioni 38! Rais wetu huyu amekuwa na mazoea ya kuwapa watu hela akiwa kwenye ziara zake huko mikoani. Huwa anatoa kiasi tofauti tofauti. Huwa anatoa laki tano, milioni moja, mbili, n.k.
Jana ndio katoa hiyo milioni 38. Kwa wanaojua, huyu Rais wetu huwa anazitoa wapi hizo pesa?
Kwenye akaunti yake? Yeye ana pesa nyingi sana? Huwa anaenda hazina na kuchota pesa ambazo anakuja anawapa wanaomuomba?
Yawezekana labda kweli ana hela nyingi. Yaani pesa zake mwenyewe zilizopo kwenye akaunti yake/zake. Kama ni hivyo basi sawa. Binafsi siwezi kumpangia mtu matumizi ya pesa zake.
Miaka takriban 13 iliyopita niliwahi kuuliza kama kuna mtu anaujua mshahara wa Rais wa Tanzania. Nilianzisha uzi humu JF kuhusu mshahara wake.
Mpaka sasa sijawahi kuona mtu mwenye taarifa sahihi kuhusu jambo hilo kwani kiasi ambacho hutajwa si kimoja. Hiyo ni ishara kwamba hakuna ajuaye kwa uhakika.
Milioni 38 ni pesa nyingi sana kwa mtu kuzitoa tu kirahisi rahisi namna hiyo. Ndio hapa najiuliza, huwa anazitoa wapi hizo pesa?
Sent using Jamii Forums mobile app