Pesa haitaki shida, inataka watu wenye suluhisho

Pesa haitaki shida, inataka watu wenye suluhisho

Mr George Francis

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
274
Reaction score
486
PESA HAITAKI WATU WENYE SHIDA, INATAKA WATU WENYE SULUHISHO.

Pesa ina njia zake. Ina tabia ya kupita mbali na mtu anayelalamika, anayetafuta msaada kila wakati, au anayeomba omba na kulialia shida kila mara.

Lakini ina tabia ya kumtembelea kwa ukaribu mtu anayetoa thamani, anayeleta suluhisho na kufanya maisha ya wengine kuwa rahisi au bora zaidi.

Pesa haina muda na shida zako: Eti kulialia kila siku “Nisaidie mwenzenu, nina shida mwenzenu, nina deni, nina njaa, mimi masikini, hapo pesa itasema... “Bye!”

Lakini kwa mtu mwenye suluhisho: Mfano “Nina hii bidhaa inasaidia moja mbili tatu." "Nina hii biashara inakupa faida one two three” Pesa nayo inasema “Njoo hapa baby, chukua hii zaidi!”

Ndio maana wafanyabiashara wakubwa, investors, na wenye pesa huwa wanatafuta problem solvers, si problem sharers.

Ukienda kuomba kazi waajiri wanataka mtu mwenye uwezo wa kuisaidia kampuni au taasisi kutatua changamoto katika uendeshaji wao na changamoto za jamii.

Kampuni haitaki mtu mwenye shida ya fedha anayetaka kufanya kazi ili apate pesa za kupeleka nyumbani kwao. Ukienda kupata kazi ili upate pesa maranyingi wanaogopa kukuajiri.

Unaweza kuwa na shida hata 100, lakini ukiwa na akili utaacha kuzisemasema kwa watu.
Badala yake ukatafuta suluhu kimya kimya, kisha uuze suluhisho iliyotokana na shida hiyo.

Mfano: Kuna mtu aliona kuna shida ya maji safi vyuoni, akapeleka mashine ya kisasa ya kuchuja maji na kutatibu yawe salama kisha kuuza kwa mtindo wa kisasa na kwa gharama nafuu.

Ni biashara inayomuingizia mamilioni kwsababu aliona tatizo na kuleta suluhisho.

Kwahiyo ili upate pesa usielezee watu matatizo yako bali angalia matatizo aidha unayopitia au yale wanayopitia wengine katika jamii kisha njoo na suluhisho, watu watakulipa watake wasitake.

Ni wakati wa kubadilisha mindset yako leo na kuwa mtu wa suluhisho.

Hata kutoa maarifa ya kile unachokijua vizuri ni njia moja wapo ya suluhu ambayo baadhi wa watu watakutafuta ili uwape ushauri wa ndani kuhusu changamoto zao na hapo watalipia huduma kisha wewe utakuwa umeingiza pesa.

Je, unatoa huduma gani ili watu waijue na waje wakuletee pesa ili kuipata?

Tuandikie kwenye comments.

#No_learnig_No_earning
So We Have To Learn.

Content By George Francis

#highlight #mrgeorgefrancis #motivation #viral
 
Back
Top Bottom