Pesa binafsi, usimamizi wa pesa, biashara na utajiri

wickerman

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
411
250
Nimesoma hii makala sehemu moja huko kwenye intaneti nikasema sio mbaya kama nikiitafsiri ili iweze kueleweka kwa wote, pia nimebadilisha baadhi ya mifano kuendana na mazingira yetu, maana imenigusa kwa namna fulani. Nimeambatanisha PDF ya nakala zote mbili ya kiingereza na kiswahili.

-------------------------------------------------------------------------------------------------​

Usifanye maamuzi yanayo pelekewa na hisia/mihemko kwenye maswala ya pesa. Siri ya kwanza ya watu wenye utajiri mkubwa ni huwa hawaruhusu sana hisia zao kufanyia maamuzi inapokuja kwenye kutoa au kutumia pesa. Haiwaathiri sana endapo rafiki zake wamenunua kitu kipya, wanabadilisha magari kila mwaka au wanakwenda kubaridhi nchi za nje kila mwezi. Watu wenye utajiri wanajua kwa hakika kuwa hisia/mhemko ni mshauri mbaya inapokuja kwenye pesa.

Tunanunua vitu tusivyo vihitaji, kwa pesa ambazo hatuna, kuwa onyesha watu tusiowapenda. Usipoteze pesa bure. Usitumie zaidi ya unacho tengeneza. Usiwe yule mtu anae nunua simu ya 600,000/= wakati kwa uhalisia anauwezo wa 150,000/=; Ishi maisha ya kawaida. Pata kifungua kinywa cha kawaida. Kula mlo wa mchana wa kawaida. Kula chakula cha usiku cha kawaida. Wakati bado ni kijana una nguvu na unaweza kujibadili kuendana na mazingira kwa urahisi; Mwili wako hautoteseka sana na mlo wa kawaida.

Jifunze kuishi ndani ya uwezo wako. Tunza pesa kwanza kabla ya kununua au kufanya kitu cha gharama. Hii ina kufundisha umuhimu wa uvumilivu na hautokuja jutia baadae. Usitumie pesa kupindukia kwenye nguo, viatu na mali ndogo ndogo. Jiulize kitu gani kweli unahitaji na kitu gani kweli haukihitaji kwa ulazima. Kweli unahitaji kuwa na TV ya inchi milioni?(😂); Uhuru wa kiuchumi unakuja kwa mtu ambae kweli anadhibiti maswala yake ya pesa. Hautofikia hapo kama hauto anza kubadilika.

Hatua ndogo ndogo, endelea kwenda mbele. Hatua moja kuelekea kwenye malengo yako kila siku. Hauhitaji kuwa na kila kitu au kufanya yote kwa mkupuo, moja baada ya moja inatosha. Chochote kilichotokea nyuma kipo nyuma. Usiruhusu yaliyopita yakakuathiri sana. Anza kuandika matumizi yako, hata kama ni kidogo. Na Kama utaweza, jikumbushe haya maneno kila siku asubuhi, “Sehemu ya pesa nitakayo ingiza leo nitajiwekea mwenyewe.” Usigawe pesa yako yote ulioingiza kwa mangi mwenye duka, kijana mwenye biashara ya chipsi au mmiliki wa baa.

Tunza asilimia kadhaa ya pesa uliyoingiza. Kila siku mti unakuwa kidogo kidogo, unaweza ona kama hakuna mabadiliko. Ukirudi kwenye huo mti baada ya miaka michache utaona mabadiliko makubwa. Mfano unataka kununua TV mpya kwa ajili ya nyumbani kwako, ipangie, itunzie pesa! Jifundishe nidhamu ya kifedha, jifunze kujizuia na matumizi ya pesa kwa hisia/mihemko. Usikopeshe pesa ambayo hauko tayari kiuchumi kuipoteza. Kopesha tu! pesa ambayo uko tayari kiuchumi kuipoteza.

Usinunue mali ambayo haujaielewa vizuri. Na Kama upo kwenye manunuzi, usidanganyike sana na bidhaa ambazo zinatangazwa kuuzwa kwa asilimia pungufu kama ofa kwako. Utaishia tu kutumia pesa nyingi zaidi kuliko budget yako uliopanga; hizi ni hila za kisaikolojia. Tenga dakika tano kila siku kuangalia miamala yako ya pesa. Usitumie pesa bila busara. Wekeza pesa. Na kuliko kuangalia namna za kutunza pesa nyingi zaidi, tafuta namna za kutengeneza pesa nyingi zaidi.

Tazama kwa umakini sehemu ambazo pesa inatumika na wapi watu wanauhitaji napo. Tafuta watu wenye njaa(uhitaji) na wasogezee chakula. Anzisha biashara yako ndogo na uweke matarajio yenye uhalisia. Pima maji na mguu mmoja kwanza kabla haujazamisha wa pili. Hata siku moja usijetumia hifadhi yako yote ya pesa kwenye wazo la biashara kabla hujalifanyia majaribio yanayoridhisha. (Kwa kusisitizia) Tenga dakika tano kila siku kuangalia miamala yako ya pesa.

Fanya uamuzi kuwa utakuwa muaminifu kwenye shughuli zako zote hata kama itakugharimu pesa. Sifa yako ndio kila kitu. Pesa siku zote itarudi haraka kwa yule anaeaminika. Ishi maisha ya kawaida na uwe na njia tofauti tofauti za kukuingizia kipato. Inabidi matumizi yako yawe chini ya unachoingiza. Kadiri ya jinsi vitakapopishana utajiri wako ndio utaongezeka.

Gusa uhitaji wa watu wengi kadiri ya uwezo wako kwa wingi wao au wachache kwa kiasi(faida ya juu) kupitia biashara unayoiongoza(miliki) na utakua tajiri. Jitengenezee tabia ya kutoa mchango kwenye taasisi za kijamii au kidini. (Bakuli lililojaa haliongezewi mchuzi).

MWISHO

Mjumbe hapigwi.
 
Attachments

 • File size
  62.8 KB
  Views
  23
 • File size
  493.3 KB
  Views
  21
Nov 4, 2019
10
45
Nimesoma hii makala sehemu moja huko kwenye intaneti nikasema sio mbaya kama nikiitafsiri ili iweze kueleweka kwa wote, pia nimebadilisha baadhi ya mifano kuendana na mazingira yetu, maana imenigusa kwa namna fulani. Nimeambatanisha PDF ya nakala zote mbili ya kiingereza na kiswahili.

-------------------------------------------------------------------------------------------------​

Usifanye maamuzi yanayo pelekewa na hisia/mihemko kwenye maswala ya pesa. Siri ya kwanza ya watu wenye utajiri mkubwa ni huwa hawaruhusu sana hisia zao kufanyia maamuzi inapokuja kwenye kutoa au kutumia pesa. Haiwaathiri sana endapo rafiki zake wamenunua kitu kipya, wanabadilisha magari kila mwaka au wanakwenda kubaridhi nchi za nje kila mwezi. Watu wenye utajiri wanajua kwa hakika kuwa hisia/mhemko ni mshauri mbaya inapokuja kwenye pesa.

Tunanunua vitu tusivyo vihitaji, kwa pesa ambazo hatuna, kuwa onyesha watu tusiowapenda. Usipoteze pesa bure. Usitumie zaidi ya unacho tengeneza. Usiwe yule mtu anae nunua simu ya 600,000/= wakati kwa uhalisia anauwezo wa 150,000/=; Ishi maisha ya kawaida. Pata kifungua kinywa cha kawaida. Kula mlo wa mchana wa kawaida. Kula chakula cha usiku cha kawaida. Wakati bado ni kijana una nguvu na unaweza kujibadili kuendana na mazingira kwa urahisi; Mwili wako hautoteseka sana na mlo wa kawaida.

Jifunze kuishi ndani ya uwezo wako. Tunza pesa kwanza kabla ya kununua au kufanya kitu cha gharama. Hii ina kufundisha umuhimu wa uvumilivu na hautokuja jutia baadae. Usitumie pesa kupindukia kwenye nguo, viatu na mali ndogo ndogo. Jiulize kitu gani kweli unahitaji na kitu gani kweli haukihitaji kwa ulazima. Kweli unahitaji kuwa na TV ya inchi milioni?(); Uhuru wa kiuchumi unakuja kwa mtu ambae kweli anadhibiti maswala yake ya pesa. Hautofikia hapo kama hauto anza kubadilika.

Hatua ndogo ndogo, endelea kwenda mbele. Hatua moja kuelekea kwenye malengo yako kila siku. Hauhitaji kuwa na kila kitu au kufanya yote kwa mkupuo, moja baada ya moja inatosha. Chochote kilichotokea nyuma kipo nyuma. Usiruhusu yaliyopita yakakuathiri sana. Anza kuandika matumizi yako, hata kama ni kidogo. Na Kama utaweza, jikumbushe haya maneno kila siku asubuhi, “Sehemu ya pesa nitakayo ingiza leo nitajiwekea mwenyewe.” Usigawe pesa yako yote ulioingiza kwa mangi mwenye duka, kijana mwenye biashara ya chipsi au mmiliki wa baa.

Tunza asilimia kadhaa ya pesa uliyoingiza. Kila siku mti unakuwa kidogo kidogo, unaweza ona kama hakuna mabadiliko. Ukirudi kwenye huo mti baada ya miaka michache utaona mabadiliko makubwa. Mfano unataka kununua TV mpya kwa ajili ya nyumbani kwako, ipangie, itunzie pesa! Jifundishe nidhamu ya kifedha, jifunze kujizuia na matumizi ya pesa kwa hisia/mihemko. Usikopeshe pesa ambayo hauko tayari kiuchumi kuipoteza. Kopesha tu! pesa ambayo uko tayari kiuchumi kuipoteza.

Usinunue mali ambayo haujaielewa vizuri. Na Kama upo kwenye manunuzi, usidanganyike sana na bidhaa ambazo zinatangazwa kuuzwa kwa asilimia pungufu kama ofa kwako. Utaishia tu kutumia pesa nyingi zaidi kuliko budget yako uliopanga; hizi ni hila za kisaikolojia. Tenga dakika tano kila siku kuangalia miamala yako ya pesa. Usitumie pesa bila busara. Wekeza pesa. Na kuliko kuangalia namna za kutunza pesa nyingi zaidi, tafuta namna za kutengeneza pesa nyingi zaidi.

Tazama kwa umakini sehemu ambazo pesa inatumika na wapi watu wanauhitaji napo. Tafuta watu wenye njaa(uhitaji) na wasogezee chakula. Anzisha biashara yako ndogo na uweke matarajio yenye uhalisia. Pima maji na mguu mmoja kwanza kabla haujazamisha wa pili. Hata siku moja usijetumia hifadhi yako yote ya pesa kwenye wazo la biashara kabla hujalifanyia majaribio yanayoridhisha. (Kwa kusisitizia) Tenga dakika tano kila siku kuangalia miamala yako ya pesa.

Fanya uamuzi kuwa utakuwa muaminifu kwenye shughuli zako zote hata kama itakugharimu pesa. Sifa yako ndio kila kitu. Pesa siku zote itarudi haraka kwa yule anaeaminika. Ishi maisha ya kawaida na uwe na njia tofauti tofauti za kukuingizia kipato. Inabidi matumizi yako yawe chini ya unachoingiza. Kadiri ya jinsi vitakapopishana utajiri wako ndio utaongezeka.

Gusa uhitaji wa watu wengi kadiri ya uwezo wako kwa wingi wao au wachache kwa kiasi(faida ya juu) kupitia biashara unayoiongoza(miliki) na utakua tajiri. Jitengenezee tabia ya kutoa mchango kwenye taasisi za kijamii au kidini. (Bakuli lililojaa haliongezewi mchuzi).

MWISHO

Mjumbe hapigwi.
Ahsante!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom