Performance Review ya Dr. Hoseah (PCCB) na IGP Mwema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Performance Review ya Dr. Hoseah (PCCB) na IGP Mwema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kagalala, Jun 30, 2012.

 1. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,360
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Kama kuna watu ambao mimi binafsi sijuhi utendaji wao wa kazi katika nchi yetu ni Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Rushwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi. Tangu watu hawa washike nyazifa zao, sioni ambalo wamechangia katika hali yetu Tanzania. Hivi Dr Hoseah na IGP Mwema wakistahafu leo tutawakumbuka kwa lipi jema?

  Kwa upande wa Dr. Hoseah' rushwa imeongezeka nchini ofisi yake imekuwa chombo cha kupambana na dagaa wakati papa wanakula nchi.

  Kwa IGP Mwema, Mambo ya hajabu yanaendelea nchini kama vile ujambazi, vifo vya kutatanisha, mateso kwa watu bila majibu na mauhaji ya raia kutoka kwa Polisi lakini hakuna anayemuuliza IGP Mwema anafanya nini na jeshi lake.

  Kwa nchi ya wenzetu kila mwaka huwa kuna Performance Review ya kila mfanyakaziv ambapo wanaangalia ni nini amefanya kwa mwaka mzima. Na hili linasaidia kujua kama anafaa kuendelea na kazi yake au hapana.

  Katika viwango vya 1 - 4 naomba tuwapime hawa watu, na hili labda litamsaidia Rais kujua sisi wananchi tunawaonaje hawa watu

  1 - Hafai kabisa na aondolewe katika cheo hiki
  2 - Anajitahidi lakini bado yuko nyuma
  3 - Kazi yake inalidhisha
  4 - Kazi yake nzuri sana na endelee kuwepo madarakani
   
 2. paty

  paty JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,219
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  HOSEA = Hafai kabisa na aondolewe katika cheo hiki _________S.MWEMA = Hafai kabisa na aondolewe katika cheo hiki. Sababu za kuwapa ushazitoa mwenyewe hapo juu , kama unataka sababu zaidi ntaweka
   
Loading...