Pepsi, Coca zaua Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pepsi, Coca zaua Mbeya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Apr 16, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,426
  Likes Received: 22,341
  Trophy Points: 280
  NI vita ya ushindani wa kibiashara ilikuwa imehamia barabarani baada ya malori mawili ya kampuni zinazopambana vikali katika biashara ya vinywaji laini, Pepsi na Coca-Cola kugongana na kusababisha vifo vya watu watano.

  Magari hayo, Mitsubishi Fuso linalomilikiwa na kampuni ya SBC
  inayotengeneza soda za jamii ya Pepsi, na Mercedes Benz linalomilikiwa na Coca-Cola yaligongana eneo la Mlima Senjere kwenye barabara ya Mbeya/Tunduma wakati gari moja likitaka kulipita lori lililokuwa limebeba bia.

  Chriss Kashiririka, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, alisema dereva wa Fuso, Benedict Sanga, 50, alikuwa akijaribu kulipita gari la Coca-Cola lililokuwa likiendeshwa na Henry Mbalah, 38, lakini ghafla akaliona lori lililobeba bia likipandisha mlima na hivyo kuamua kurudi kwenye njia yake na kujikuta akiligonga kwa nyuma Benz hilo.

  Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Advocate Nyombi Waliokufa katika ajali hiyo ni pamoja na dereva wa gari ya Pepsi (SBC) Sanga ambaye ni mkazi wa Sae, afisa mauzo wa Pepsi, Martha Mushigati, 32, mkazi wa Forest, Enos Elia, 32, mkazi wa Iyunga na Samuel Thomas, 25 mkazi wa Nzovwe ambao walikuwa vibarua kwenye gari hilo la Pepsi.

  Mwingine ni dereva wa kampuni ya SBC aliyekuwa ameacha gari yake katika mji mdogo wa Vwawa wilayani Mbozi na kupanda gari hilo laPepsi, Albert Mbanga, 38, ambaye ni mkazi wa kitongoji cha Uyole jijini Mbeya.
  Kamanda Nyombi amesema ajali hiyo ilitokea majira ya saa 2:00 usiku na kwamba miili ya waliofariki imehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
  Alisema ajali hiyo ilisababishwa na mwendo wa kasi wa gari hilo la SBC wakati akishuka kwenye mteremko huo na kushindwa kudhibiti breki zake.
  Kamanda Nyombi alisema katika ajali ya pili iliyotokea jana saa 02:45 usiku eneo la Nzovwe jijini Mbeya, mpandabaiskeli aliyefahamika kwa jina moja la Nick alikufa papohapo baada ya kugongwa na gari aina ya Toyota Hiace iliyokuwa ikiendeshwa na Nicholous Masebo mkazi wa Nzovwe ambaye anashikiliwa na jeshi hilo.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Nilipata habari hizi mara baada ya ajali kutokea, huyo dereva aliyeacha gari yake Tunduma akapewa lifti kwenye gari ya PEPSI (Albert Mbanga) ni jamaangu wa karibu, tunatoka kijiji kimoja ..
  Too bad!
  Mazishi yake kesho!
   
 3. elimumali

  elimumali Senior Member

  #3
  Apr 16, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mungu awalaze pema peponi marehemu wote. Pole PJ.
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Mungu awalaze pepa peponi Amen
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,426
  Likes Received: 22,341
  Trophy Points: 280
  Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
  Pia pole sana kaka kwa kuondokewa na rafiki yako.
  MUNGU NI MKUU SANA, TUNAMUOMBA AKUFARIJI NA KUKULINDA, UPATE AMANI.
   
 6. E

  Erica Furaha Member

  #6
  Apr 16, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mwenyenzi mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi amen
   
 7. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Poleni sana wafiwa...
   
 8. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Rip
   
 9. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Advocate Nyombi Waliokufa katika ajali hiyo ni pamoja na dereva wa gari ya Pepsi (SBC) Sanga ambaye ni mkazi
  Mungu awalaze pema peponi marehemu wote. Amina.
  Nilihudhuria mazishi ya huyo jirani yangu kwenye bold. baadhi ya wafanyakazi wa Pepsi wanaolifahamu gari hilo lililopata ajali wanasema lilikuwa bovu na mara kwa mara hukutwa limeharibika njiani. Na baadhi ya wengine wanaolifahamu wamekuwa wakilikwepa kwenda nalo kwenye mauzo. Siwezi kujua kama ubovu wa gari hilo umechangia katika ajali hiyo mbaya.
   
Loading...