Makau Js
Member
- May 25, 2017
- 93
- 233
Josep "Pep" Guardiola Sala ametoka bila kikombe chochote katika msimu wake wa kwanza na timu yake ya Man City ,na siku zote mambo yake yanapokwenda kombo humtafuta rafiki yake anayejua kufikilia sana linapokuja suala la ushindani.
Guardiola hutafuta ushauri kwa bingwa wa mchezo wa Chess anayeitwa Garry Kasparov kumpa mbinu za kuwa juu siku zote za ushindani.leo Man City wamemsajili,Bernardo Silva kiungo fundi mwenye uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya kiungo na winger .
Bernardo Silva amecheza Monaco mechi 58 ,amefunga magoli 11 na kutengeneza nafasi 84 katika michuano yote aliyocheza As Monaco.Silva tayari ameishatua Man City kutoka club ya,AS Monaco FC ya Ufaransa kwa ada ya£43million.
Msimu ujao Mwenyezi -Mungu akitupa pumzi na afya tutaiona Man city yenye Gabriel Jesus miaka 20,Raheem Shaquille Sterling miaka 22,Leroy Sané miaka 21.[HASHTAG]#SoccerMtambuka[/HASHTAG].