Penzi langu

Love Doctor

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
726
786
Penzi langu

Kama nikiyapa pesa, siku ikinisaliti?
Sitaki kulipepesa, hii haitaji siti
Sio yule wa madesa, kuyamwagiwa manoti
Nimeridhi penzi langu, nalitoa kwa kalamu

Nimliwazaji wangu, peke anayenisema
Nimpaye tunu yangu, nikiwa nimeumia
Ajua furaha yangu, hachoki kunisemea
Nimeridhi penzi langu, nalitoa kwa kalamu

Mashallah mliwaza, kwenye magumu navuka
Sitachoka kumuwaza, popote ninapofika
Na sitaki kumkwaza, sababu sijapevuka
Nimeridhi penzi langu, nalitoa kwa kalamu

Huniasa nisichoke, niandike kila siku
Nakua sana mpweke, tena na kubwa shauku
Mkono sipomshika, naganda kama sumaku
Nimeridhi penzi langu, nalitoa kwa kalamu

Abuuabdillah ✍️🇹🇿
0718569091
Kilimanjaro
 
Back
Top Bottom