Pentagon chief threatens Iran with ‘pre-emptive action’ if embassy attacks continue

Iran hawezi jidanganya kurusha chochote ndani ya Israel maana hadi Marekani kumuua mtu mkubwa kivile maana yake keshapima maji kajua uwezo wa kuyavuka

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sawa mkuu, lakini mahesabu huwa yanakosewa hasa kwenye vita. Magaidi wa Bosnia walivyomuua Archduke Ferdinand walidhani ugomvi wao ungeishia tu Austria-Hungary bahati mbaya ufalme wa Ujerumani na Ufalme wa Urusi wakajikuta wamevutwa na mara vita ya dunia hii hapa.

Upande mwingine wa shilingi ni kwamba karne yetu ina uzuri wake : Miaka yetu kuna taasisi za kimataifa zenye nguvu kama Umoja wa Mataifa, pia nchi nyingi zimejifunza kutokana na makosa ya kihistoria yaliyotokea mwaka 1914 na 1939 ndiyo maana mpaka sasa unaona kila upande umejizuia kwa kiwango kikubwa kuchukua maamuzi ya haraka wakiogopa kukosea mahesabu.

Sasa kwenye mazingira kama haya usitegemee kuona vita kubwa kwa ghafla (Conventional Warfare) bali vita ya ndogo ndogo (Asymmetric Warfare with plausible deniability) ambazo zitasababisha maumivu na madhara makubwa kwa pande zote mbili kama hivi unavyoona. Japo pia Asymmetric Warfare can lead to a major military confrontation.

Hivyo tusijihakikishie kwamba hakitatokea chochote, kwasababu tumewaangalia Marekani na Iran pekee tukisahau kwamba ule ukanda una mataifa kama Saudi Arabia, Lebanon, Iraq, Syria na Israel ambayo kwa namna moja au nyingine hiki kifo kitaathiri mwenendo wa sera zao za ulinzi na diplomasia.
 
Back
Top Bottom