Pensheni ya Marehemu sasa kusomesha watoto

Pensheni ya Marehemu sasa kusomesha watoto

Tukiwaambia hawa viongozi hawafai na hawana uchungu na nyinyi wala hawanampango wakuwaletea maisha bora baadhi yenu mnakuwa hamuelewi somo.Poleni watumishi na wastaafu.
 
SHERIA mpya ya Hifadhi ya Jamii imefuta Fao la Elimu lililokuwa linatolewa na mifuko ya hifadhi ya jamii, badala yake fedha za mwanachama aliyefariki ndizo zitatumika kuwasomesha watoto wake...

Chanzo:NIPASHE, Novemba 22, 2018
kama watoto wote wameshamaliza elimu yao na wanajitegemea??.........
 
Mbona haya majitu yanawazia vifo tu kwa wanachama? Yaani kila sehemu utaona mwanachama akifa.....
Haya majitu yatangulie kwanza yajue uzuri wa hiyo sera
Hapo ndipo serikali hupata faida licha ya hivyo siku hizo kila kukicha ni uhakiki wa wanachama na NSSF yenyewe iko hoi kifedha malipo mpaka ihemee toka kwa walio kazini ndiyo iwalipe wastaafu.
 
Huku kuna mtu anasisitiza zaeni kwa fujo, upande wa pili lijitu linakuja hakikisheni hawazaani kwa kufa mapema kwa msongo.

Ni bora hilo fao la kusomesha kabla mtu hajafa, kwanza linampa mtu faraja na uhakika kwa watoto wake. Mzazi yeyote anakuwa furaha kama akiona future ya mtoto wake ni ya uhakika hasa elimu.

Kwa umri wa miaka 60 nani anakuwa bado anazaa na kusomesha??? Unless kama wanamaanisha watalipia masomo ya phd ya watoto!

Hawa watu ni kundi jingine la wanyang'anyi hakuna wanachowaza zaidi ya kuwaibia wastaafu kwa mwamvuli wa sheria na sera walizozitunga.

Wenyewe kwa sasa utakuta wanajilipa vizuri, safari za nyingi zisizo na tija ndani na nje ya nchi. Kujilipa allawance hata kwa vikao vya ndani ("hili ni tatizo kubwa kwa taasisi za umma") mtu analipwa posho ya kuuzulia kikao cha ndani cha kujandili utendaji wa taasisi yake. Sijui alitegemea nani aje amfanyie hicho kikao? Kutumiza wajibu wako unataka kulipwa!! Wewe CEO, Director, Manager au Chief au whatever kuwasilisha report au kusimamia kikao ni sehemu ya wajibu wako. Ikitokea kuna vikao zaidi vyote mtu analipwa lakini bado utendaji mbovuuuu.

In short naweza hitimisha kwa sasa hii mifuko agenda ya kubwa ni kuhakikisha inampeleka mstaafu kaburini mapema kadli iwezekananyo na unaweza kuta hii ni KPI ya mtu mwaka huu umepunguza wastaafu wangapi? kisha watu wanagonga mvinyo kujipongeza
 
Back
Top Bottom