Pensheni kwa wastaafu toka hazina kulikoni?

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Mimi ni mmojawapo wa Wastaafu ninayepata Pensheni yangu kutoka HAZINA. Kila mwezi ninapata mafao yangu kuanzia tarehe 28 mpaka tarehe 1 mwezi unaofuata. Mpaka leo licha ya kwenda Benki kufuatilia hakuna kilichowekwa kwenye akaunti yangu. Ninauliza kulikoni?
 
Jaribu kuwauliza wenzio unopata nao pensheni yaweza kuwa kunatatizo kwako tu au kwa wote!!
 
Sisi wewe tu hata mzee wangu hajapata malipo take yakila mwezi yeye huwa anatumiwa message, usisumbuke kuwa unakwenda benk jisajili na huduma ya sim banking hutopata tabu tena mzee wetu.
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Sisi wewe tu hata mzee wangu hajapata malipo take yakila mwezi yeye huwa anatumiwa message, usisumbuke kuwa unakwenda benk jisajili na huduma ya sim banking hutopata tabu tena mzee wetu.
Naona mwezi huu hawakutuma ujumbe,jaribu kwenda kuangalia salio kwenye ATM,inawezekana ikawa imewekwa tayari.
 
Serikali ISIYOJALI Watumishi Wastaaf waliotumikia Nchi hii kwa JASHO KUBWA ni Serikali dhalimu na inapaswa kupingwa na kila mwenye akili TIMAMU
 
Mimi ni mmojawapo wa Wastaafu ninayepata Pensheni yangu kutoka HAZINA. Kila mwezi ninapata mafao yangu kuanzia tarehe 28 mpaka tarehe 1 mwezi unaofuata. Mpaka leo licha ya kwenda Benki kufuatilia hakuna kilichowekwa kwenye akaunti yangu. Ninauliza kulikoni?
Labda kwa sababu ya weekend mkuu,naamini watatoa,ila haijakaa vizuri.Hela yenyewe ni kidogo, halafu inacheleweshwa,ni shida kubwa sana kwa wastaafu,hasa ukizingatia kwamba wengi wa wastaafu wetu hawana njia nyingine ya kujipatia kipato,na hata kama wanayo mara nyingi haikidhi haja.Tunaomba hazina wajitahidi kuwalipa wazee wetu mapema,wanawapa adha kubwa.Wakumbuke kwamba na wao ni wazee watarajiwa.Wazee hawa
wamelitumikia taifa letu kwa juhudi na uadilifu mkubwa,tuwaheshimu.
 
Mimi ni mmojawapo wa Wastaafu ninayepata Pensheni yangu kutoka HAZINA. Kila mwezi ninapata mafao yangu kuanzia tarehe 28 mpaka tarehe 1 mwezi unaofuata. Mpaka leo licha ya kwenda Benki kufuatilia hakuna kilichowekwa kwenye akaunti yangu. Ninauliza kulikoni?
Wewe sio mstafu mzalendo
 
Daaa!funzo kubwa kwa watumishi.Angekuwa na miradi yake ya kumuingizia kipato ingepunguza machungu kipindi cha kucheleweshewa.Ila hawa wazee wetu sitaki kuwalaumu cze mfumo wa kipindi hicho uliwabana kufikiri nje ya box.
 
Zimbabwe hiyo!!!!!!!!!!! naiona.Waliimba mpaka nyimbo tukawadharau ila naiona.Mark my words.
 
Back
Top Bottom