Pengo: Wananipakazia madawa ya kulevya!

Pengo: Wananipakazia madawa ya kulevya!

busar

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2011
Posts
1,071
Reaction score
1,069
Pengo anasema kaiona list ya wauza unga nae yumo, but anadai kabambikiwa ili kumtuliza. hebu mtujuze great thinkers

=======
UPDATE
=======

ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema yeye si mfanyabiashara wa dawa za kulevya ila anatajwa kwa nia ya kunyamazishwa asizungumze ukweli.

Kardinali Pengo akizungumza na vijana katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Kawe jana alisema hajapata kuona wala kujua dawa za kulevya, lakini anajua anatajwa hivyo na wanaotaka anyamaze.

"Mimi mwenyewe nimewekwa katika orodha ya dawa za kulevya, naona kwenye vyombo vya habari, dawa zenyewe wala zisijui, lakini naendelea kuzungumza kwa sababu najua yanafanywa na wanaotaka kuninyamazisha … sitanyamaza ng'o," alisema Pengo.

Alikuwa akiwaeleza vijana kuhusu utandawazi na kuwataka waache kuyumbishwa na kuamini kila wanachoona kimeandikwa kwenye mtandao.

Alisema mambo mengi ya ajabu yamekuwa yakiandikwa na kusemwa, lengo ikiwa ni kunyamazisha maaskofu na mapadri wasiendelee kufundisha ukweli, ili watu wachache wafaidike.

"Ni uzushi unaofanywa na watu kuharibu na kuchimbachimba Kanisa tusiseme ukweli, wachache waendelee kufaidika, naomba vijana msisombwe na hali hii, kwani watu hawa hawana woga ili mradi lengo lao la kuharibu Kanisa lifanikiwe … vijana mna uhai ndani yenu na mna uwezo kama maaskari wa kupambana na waovu wa Kanisa," alisema.

"Silaha ya vijana ni maisha yanayojua mnaamini kitu gani, msikubali kuyumbishwa na watu wanaotoa mambo vichwani mwao. Kama mnasikia natajwa, njooni mniulize, Baba mbona nimesikia habari fulani, badala ya kuyabeba na kushabikia…imani yenu si ya kutetereka, endeleeni kuwa imara watetereke wanaotaka tutetereke," alisema.

Alisema vijana pia wamekuwa wakitumika kama vyombo katika biashara ya kulevya huku watu wachache wakitajirika na kwamba baadhi yao wanaokemea au kuzungumzia, wanapuuzwa au kuambiwa ndio wafanyabiashara wa dawa hizo, jambo ambalo nyuma yake halina ukweli wowote.

Kardinali Pengo alisema lengo ni kutaka kuwanyamazisha watu wanaosema ukweli ili wachache waendelee kutajirika na biashara hiyo kwa kuwatia hasara vijana.

Naye Mhashamu Askofu Salutaris Libena, ambaye aliongoza Ibada Takatifu, alisema vijana wamekutana ili kumshukuru Mungu na kumwomba neema .

Libena ambaye pia ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, aliwataka vijana kuingia mwaka mpya kwa kumjua na kumtukuza Mungu.

Mbali na vijana kushiriki ibada hiyo lakini pia zilikuwapo burudani mbalimbali za kwaya na ngoma, sambamba na vijana kupima kwa hiari damu kwa ajili ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama.

Kila mwisho wa mwaka vijana kutoka makanisa mbalimbali ya Kanisa Katoliki hukutana kwa lengo la kumtukuza Mungu na kumshukuru kwa kumaliza mwaka.
 
Hii hbr imepangwa na kikundi kdg cha watu, na wamelitumia gazeti la Habari leo ambalo chuki yake dhidi ya kanisa katoliki ilidhihirika tangu sakata la Sumbawanga. CCM wameamua kufanya mchezo wa devide and rule, lakini kuna siku watajuta.
 
Inawezekana kweli anasingiziwa ili afunge domo asiwaseme mafisadi. lakini hao wanaomsingizia nia akina nani serikali au?
 
Utaratibu tuliojiwekea ni kwamba mtu ukitajwa tajwa basi unatakiwa kujivua gamba. Kwa hiyo Mhashamu Polycap Kardinali Pengo ametajwa tajwa kwenye madawa ya kulevya basi hana budi kujivua gamba asiendelee kulichafua kanisa la la mungu.
 
Hii hbr imepangwa na kikundi kdg cha watu, na wamelitumia gazeti la Habari leo ambalo chuki yake dhidi ya kanisa katoliki ilidhihirika tangu sakata la Sumbawanga. CCM wameamua kufanya mchezo wa d
evide and rule, lakini kuna siku watajuta.
kila kitu si siasa,hizi issue za kudhalilisha watoto zinzolikabili kanisa dunoa nzima sasa na wakatoliki wenyewe wanalalamika kwambapapa hachukui hatua anaficha madhambi,JE NI HABARI LEO,CCM AU SIRIKALI INAHUSIKA.yule pdre alomnajisi mtoto chuo kikuu kweye gari ni serekali imetunga au habari leo.anachotakiwa pengo kusema ni kuilazmisha serikali ithibitishe.HE WHO ALLEGE MUST PROVE
 
Utaratibu tuliojiwekea ni kwamba mtu ukitajwa tajwa basi unatakiwa kujivua gamba. Kwa hiyo Mhashamu Polycap Kardinali Pengo ametajwa tajwa kwenye madawa ya kulevya basi hana budi kujivua gamba asiendelee kulichafua kanisa la la mungu.

Vague!
 
Hayo majina yamekuwwpo muda mrefu ila Pengo hajawahi kusema kuwa anatajwa tajwa! Ukiona mtu anaanza kupiga makelele ujue kuna jambo linakuja na hivyo ana pre empty hali inayokuja. By the way, nani kamtaja taja?
 
busara za kadinali Pengo zinashangaza....sana....

kazi ya polisi ni kutodharau taarifa yeyote wanayopewa

sasa kama polisi wamepewa jina lake wafanyaje?
si lazima waliweke kwenye uchunguzi mpaka watakapothibitisha vinginevyo??

yeye ana wasiwasi gani ?

kwani wamemtaja hadharani au kwenda kum arrest?????
 
Najiuliza kwann hakuli address hili akiwaita waandishi wa habari? Ukweli utajulikana as time being
 
Kuna vita kubwa mbili kwa sasa.....mwenye akili wala hatakiwi kuambiwa ,moja kunyamazisha kanisa kwa ujumla wake na watu wake kwenye kukemea maovu na kushiriki kwenye siasa za majukwaani.....hasa kwenye kuonya na kukemea.....pili kujaribu kupambana na wanavyodai mfumo kristu....kujaribu kupunguza nguvu za hao wanaojidai wametawala kila sehemu...maana sasa ni zamu yetu!!!!!!
 
Kulelekea 2015 kuna mengi tutayaona kwani kiukweli tumepotea njia na hakuna anayeonyesha kwamba tumepotea njia, badala yake wote wanashindana kutuongoza kwenda mbele kwenye njia tuliyopotea tangu zamani. Pengo kuna wakati anasema UKWELI hata kama ukweli huo haupendwi na wengi.

Kwenye hili inaonyesha ameamua kuwawahi wapinzani wake kabla ya kuadhiriwa. Leo hii ikisemwa kwamba Pengo anajihusisha na madawa ya kulevya basi watu tutajua ama ni uzushi au ni muendelezo wa harakati za kuelekea 2015
 
busara za kadinali Pengo zinashangaza....sana....

kazi ya polisi ni kutodharau taarifa yeyote wanayopewa

sasa kama polisi wamepewa jina lake wafanyaje?
si lazima waliweke kwenye uchunguzi mpaka watakapothibitisha vinginevyo??

yeye ana wasiwasi gani ?

kwani wamemtaja hadharani au kwenda kum arrest?????

Wangekwenda kumuarrest ndio nigeona wanafanya jambo la maana. Kutaja majina magazetini ni sehemu ya uchunguzi wa polisi? Kwa vipi tuiunge mkono serikali ya vuvuzela isiyo na vitendo? Kwa hiyo tukae chini tutegemee kwamba kwa kuropoka magazetini ukweli utapatikana?

Huu ndio ujinga wetu watanzania. Na ndio maana kina Jairo wanaendelea kutesa mitaani hata baada ya kubainika wamefanya madudu. Ni ujinga huu huu ndio umefanya tupigie makofi hotuba ya rais alipoongea na wale wacheza bao wa mwembe yanga kuwa "kila mtu atapata nafasi ya kutoa maoni" bila kujali mustakabali wa maoni yako.

Na huyu Juha mwingine anayesema gari la kifahari la askofu ni dalili ya kuuza madawa ya kulevya, kuna uhusiano gani wa gari na madawa. Kanisa Katoliki sio institution maskini namna ya kushindwa kumnunulia Askofu gari au kumpangia nyumba mpaka apangiwe nyumba na serikali.

Kama yanayodhaniwa yapo, polisi wafanye kazi na akamatwe. Kupiga piga midomo majukwaani ni dalili ya akili za jikoni. Tusiwe wepesi kufanywa wajinga na CCM.

Juzi Lowassa kawauliza kama ana ishu chafu mbona hawamfungulii mashtaka?
Hakuna aliyelitafakari hili, ila kazi yetu ni kupiga mdomo kama wanawake wa baa wasiojua taarifa ya habari wala matukio ya wiki zaidi ya majarida ya udaku.
 
''jiwe likirushwa gizani atakayetoa sauti ujue limempata''

Haswaa,wala hujakosea! Wangapi wanamkumbuka Leonard Bhonke mhubiri wa kimataifa? Alikuwa anakusanya maelfu ya watu viwanja vya wazi,pia alihubiri live kwenye radio na tv akiwa uwanjani,lakini akanaswa na shehena ya madawa ya kulevya. Kikwete kwenda kuwaambia maaskofu kuwa viongozi wa dini waache kuuza madawa ya kulevya we unadhani alikurupuka? Na alipopewa masiku ili akanushe au adhibitishe na yeye kukaa kimya ulidhani yeye *****? Alijua akiwasema hadharani kuwa ni fulani na fulani hali ya nchi itakuwa hatarini kwani watu wa madawa hujipanga kwa njia zote. Mfano ikipangwa JK auwawe,na mpango ukafanikiwa basi ujue yale ya Rwanda yatakuja Tanzania lakini itakuwa baina ya Waislam na Wakristo.
 
Wangekwenda kumuarrest ndio nigeona wanafanya jambo la maana. Kutaja majina magazetini ni sehemu ya uchunguzi wa polisi? Kwa vipi tuiunge mkono serikali ya vuvuzela isiyo na vitendo? Kwa hiyo tukae chini tutegemee kwamba kwa kuropoka magazetini ukweli utapatikana?

Huu ndio ujinga wetu watanzania. Na ndio maana kina Jairo wanaendelea kutesa mitaani hata baada ya kubainika wamefanya madudu. Ni ujinga huu huu ndio umefanya tupigie makofi hotuba ya rais alipoongea na wale wacheza bao wa mwembe yanga kuwa "kila mtu atapata nafasi ya kutoa maoni" bila kujali mustakabali wa maoni yako.

Na huyu Juha mwingine anayesema gari la kifahari la askofu ni dalili ya kuuza madawa ya kulevya, kuna uhusiano gani wa gari na madawa. Kanisa Katoliki sio institution maskini namna ya kushindwa kumnunulia Askofu gari au kumpangia nyumba mpaka apangiwe nyumba na serikali.

Kama yanayodhaniwa yapo, polisi wafanye kazi na akamatwe. Kupiga piga midomo majukwaani ni dalili ya akili za jikoni. Tusiwe wepesi kufanywa wajinga na CCM.

Juzi Lowassa kawauliza kama ana ishu chafu mbona hawamfungulii mashtaka?
Hakuna aliyelitafakari hili, ila kazi yetu ni kupiga mdomo kama wanawake wa baa wasiojua taarifa ya habari wala matukio ya wiki zaidi ya majarida ya udaku.

aliekwenda magazetini ni Pengo sio polisi
 
Gari la kifahari?

Lile gari ni mali ya kanisa ndugu usipende kukurupuka ukadhani unaongea jambo la maana mbele za watu. Ni kama yale magari ya ikulu, ukiondoka unayaacha pale unless tuamue kukuzawadia. Hata chakula anachokula pale kinalipiwa na kanisa, njoo na lingine hilo la gari ni la jikoni.
 
Back
Top Bottom