Pengo: Wakataeni wanaosaka urais kwa mabilioni

Pengo: Wakataeni wanaosaka urais kwa mabilioni

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,805
Reaction score
165,557
Katika gazeti la Nipashe la leo tarehe 29/12/2014,linaongozwa na kichwa cha habari kinachosomeka,"Pengo:Wakataeni wanaosaka uraisi kwa mabilioni".

Huu ni unafiki mkubwa kwani viongozi wa dini ndio vinara wa kupokea misaada ya fedha kutoka kwa mafisadi.
========================

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, ameitaka jamii kuungana kuhakikisha anapatikana rais aliye bora na kutodanganyika kuchagua mabilionea wanaotumia fedha nyingi kuelekea uchaguzi mkuu kutafuta uongozi wa nchi mwakani.

Kardinali Pengo amesema kiongozi wa aina hiyo akishaingia madarakani hatawatumikia wananchi maskini.

Kauli hiyo ilitolewa na Kardiali Pengo wakati kukiwa na baadhi ya viongozi wa chama tawala cha CCM walioonyesha nia za kutaka kuwania nafasi ya rais katika uchaguzi mkuu ujao mwakani.

Alitoa kauli hiyo juzi wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari, baada ya ibada maalumu ya kutimiza miaka 70 ya kuzaliwa kwake, iliyoandaliwa na mapadri wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam na kufanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph.

Alisema ili kuondoa wimbi la viongozi hao, jamii inapaswa kuungana na kuwaondoa madarakani kupitia nguvu ya umma.

"Viongozi wenye uwezo mkubwa kifedha kamwe huambatana na wenzao wenye tabia kama hiyo, hivyo ni mara chache sana viongozi kama hao kushirikiana na watu maskini, ambo ni wengi," alisema Kardinali Pengo.

Alisema viongozi wa aina hiyo ndiyo chanzo cha matatizo katika jamii, ikiwamo kuleta tofauti ya kipato baina yao kwa kuvunja maadili ya uongozi.

"Hali ya uchumi imekuwa ni mbaya, hasa kwa watu wenye kipato cha chini kutokana na kuongezeka kwa tofauti ya aliyenacho na asiyenacho. Hali hii siyo nzuri kwa amani, utulivu na ustawi wa nchi," alisema Kardinali Pengo.

Aliongeza: "Tunahitaji kuwa na viongozi wenye nia halisi, ambao wanaweza kuweka umakini kwa changamoto hizi ili kuwainua watu wa kawaida."

Aliionya jamii kuacha kufikiri kwamba viongozi walio na fedha nyingi ndiyo wanaoweza kuchangia ustawi wa watu maskini ambao ni wengi.

Alisema historia katika nchi tofauti duniani, zinaonyesha kuwapo kwa mabadiliko ya maendeleo katika nchi hizo baada ya kutumika nguvu ya umma kwa kuwaondoa viongozi wasio wawajibikaji.

Kwa mujibu wa Kardinali Pengo, kwa sasa nchi inakabiliwa na changamoto kubwa ya tofauti ya kipato na kuporomoka kwa maadili ya watumishi umma na kusababisha rushwa.

Kuhusu matarajio yake, alisema iwapo Mwenyezi Mungu atamjalia uhai, kabla ya kustaafu angependa kuona idadi ya parokia za jimbo kuu zimefikia 100, ambazo kwa sasa zipo 85.

Kwa upande wake, Askofu Msaidizi wa Jimbo hilo, Titus Mdoe, alisema jamii na viongozi wana wajibu wa kujifunza kutokana na utumishi uliotukuka ulioonyeshwa kupitia utumishi wa Kardinali Pengo.

Alisema utumishi wa Kardinali Pengo, unaweza kuelezewa kwa namna tofauti, ikiwamo uanzishwaji wa Parokia mbalimbali, ujenzi wa vituo vya afya, shule na vyuo vya ufundi.

Naye Mwenyekiti wa Mapadri Wazalendo wa Jimbo hilo, Novatus Mbaula, alisema awali maadhimisho hayo yalitakiwa kufanyika Agosti 5, mwaka huu, lakini ikashindikana kutokana na Kardinali Pengo kuhudhuria matibabu ya afya nje ya nchi.

"Kutokana na hali yake kiafya kuimarika, tumeamua kufanya ibada hii kipindi hiki," alisema Padri Mbaula.

Ibada hiyo ilihudhuriwa na maaskofu wasaidizi; Askofu Eusebius Nzigilwa na Askofu Mdoe pamoja na mapadri, watawa wanaofanya kazi katika jimbo hilo na waumini.

Kwa mujibui wa sheria za Kanisa hilo, askofu maaskofu na makardinali hustaafu rasmi katika utumishi wa kanisa wanapofikisha umri wa miaka 75.

Chanzo: Nipesha
 
Naona Lowassa kila mti kwake unateleza kadri uchaguzi unavyokaribia. Pengo ni taasisi tunaweza kumbeza yeye kama binadamu lakini ukweli unabaki kwamba taasisi yake inanguvu kubwa.
 
Mimi ni Mkristo lakini hao viongozi wa dini ndio wanaotuchanganya wananchi na nawaona niwanafiki wakubwa,ebu tujiulize alikuwa wapi tangu sakata la escrow lianze?.Jana nimesikia kiongozi wa Waislamu naye anasema wanajiandaa kutoa tamko kumpongeza Jk kwa hotuba na hatua nzuri dhidi ya Escrow. Mbona hawakujitokeza hadharani kukemea au kutoa ufafanuzi?.Nitaenda kanisani kusali lakini sintowasikiliza nakuwaamini kwahayo!
 
Mimi ni Mkristo lakini hao viongozi wa dini ndio wanaotuchanganya wananchi na nawaona niwanafiki wakubwa,ebu tujiulize alikuwa wapi tangu sakata la escrow lianze?.Jana nimesikia kiongozi wa Waislamu naye anasema wanajiandaa kutoa tamko kumpongeza Jk kwa hotuba na hatua nzuri dhidi ya Escrow. Mbona hawakujitokeza hadharani akawakemea?.Nitaenda kanisani kusali lakini sintowasikiliza nakuwaamini kwahayo!

Ukienda kanisani kutoa sadaka na michango mingine ya kusaidia kanisa wanafurahi sana ila kikinuka wanakukataa through matamko ya kinafiki hivi, ukirudi kanisani tena wanakupokea na sadaka yako.
Unafikism
 
Nakubaliana na ushauri wa Kardnali Pengo. Ila ingependeza zaidi kama viongozi wa dini wangewakataa na kuacha kuwaalika mafisadi wanaotafuta uhalali makanisani kwa kutoa mamilioni ya pesa zao chafu kama michango na sadaka.
 
Lowasa ni janga, WAOGOPENI KAMA UKOMA WANAOKIMBILIA IKULU KWA NJIA ZA RUSHWA,Mwl J K Nyerere
 
Katika gazeti la Nipashe la leo tarehe 29/12/2014,linaongozwa na kichwa cha habari kinachosomeka,"Pengo:Wakataeni wanaosaka uraisi kwa mabilioni".

CHANZO:Nipashe(kupitia Channel 10).

Huu ni unafiki mkubwa kwani viongozi wa dini ndio vinara wa kupokea misaada ya fedha kutoka kwa mafisadi.

Askofu mnafiki mkubwa huyu atuambie amechukua hatua gani kwa bank take ya kanisa kufisadi pesa za nchi na maaskofu wake kulipwa mamilioni.hakuna cha Askofu wala mama take na askofu msaka tongue huyu
 
Katika gazeti la Nipashe la leo tarehe 29/12/2014,linaongozwa na kichwa cha habari kinachosomeka,"Pengo:Wakataeni wanaosaka uraisi kwa mabilioni".

CHANZO:Nipashe(kupitia Channel 10).

Huu ni unafiki mkubwa kwani viongozi wa dini ndio vinara wa kupokea misaada ya fedha kutoka kwa mafisadi.
Unaposema viongozi wa dini unakosea kwani wate wanahongwa hizo pesa acha mambo yako bana.
 
Askofu mnafiki mkubwa huyu atuambie amechukua hatua gani kwa bank take ya kanisa kufisadi pesa za nchi na maaskofu wake kulipwa mamilioni.hakuna cha Askofu wala mama take na askofu msaka tongue huyu
Kwani ile banki anaimiliki pengo hujui hata sheria za kuanzishwa kwa bengi unakurupuka tu.
 
Yeye amewakamata wasaidizi wake walioibia watanzania kupitia Escrow? Kweli nyani haoni kundule
 
unatakiwa kushika mafundisho ya mtumishi wa mungu siyo matendo yake
 
Pengo safi sana endelea kutoa dozi. Vibaraka wa fisadi Lowasa inawauma. Potelea mbali hatufai kuwa rais wetu hata kidogo.
 
Pengo ni mpiga dili kama wapiga dili wengine tu mtaani.
 
Back
Top Bottom