Pengo amevuruga Wakatoliki na wakristo wote kiujumla! Hadi sasa bado wanajiuliza pindi ukifika muda wa kupigia kura katiba pendekezwa wapigie kura ya ndiyo au hapana?
Its obvious Pengo anatumiwa na watawala kuvuruga maoni ya wananchi. Yeye kama mjumbe wa jukwaa la wakatoliki na jukwaa la wakristu kwa ujumla lazima awajibike kwa tamko la jukwaa ambalo hata yeye binafsi ali sign (collective responsibility). kwa kweli mimi kama mkatoliki naona swala hili limeshusha sana hadhi ta cardinal Pengo mbele ya waumini wake na watanzania kwa ujumla.
Kama amesema wenzake ni UKAWA naona hapo ndo kapotoka.Alitakiwa kukana bila kuwajumuisha wenzake na Upande wa Ukawa.Sasa ninaanza kuwa na wasiwasi naye
Kwa ujumla Pengo yupo sahihi kwani hata kutoa maon wananch hawakushawishiwa na mtu kwa kulinda uhuru wao,sasa iwaje leo uwalazimishe kutoa uamuzi? Acheni ushabik rudini ktk hstoria ya mwanzo wa katba.
Yule Pengo asilia tunamfahamu mara zote alikuwa upande wa wananchi. Huyu Pengo feki wa sasa ninafikiri amejikuta njia panda. Mambo mengi ikiwa ni pamoja na tishio la serikali ya CCM kufungia Benki ya Mkombozi iwapo ataendeleza misimamo yake ya kuwa upande wa wananchi. Pia kuna suala la urais wa homeboy wake, Pinda. Pinda amemshawishi amuunge mkono na kuunga mkono Pinda maana yake lazima uende upande wa watawala vs wananchi. Ni kweli Kardinali yuko njia panda anapiga ramli achukue mwelekeo upi ambao utakuwa salama. Matokeo yake kauli tata na kinzani!