stigajemwa
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 449
- 430
Mpaka tutakapounda mfumo imara ndipo tutakapopiga hatua za maendeleo.Tunapozungumzia mfumo tuna maana kuundwa kwa taasisi imara zenye sera na mfumo unaojitoshereza kimaamuzi.Mfano 1 1.Kuunda katiba mpya inayoweka mipaka mamlaka ya raisi
2.Kuandaa mtaala wa elimu ulio katika maandishi unaotoa sera,muelekeo,malengo na falsafa ya elimu yetu kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu na masomo yote .Hii itasaidia kila waziri kutekeleza mtaala huo na si kuanzisha mitazamo yake
3.Kuunda mihimili au taasisi imara za kimaamuzi kama vile bunge,mahakama na dola.Hii itasaidia kuisimamia serikali vizuri nakumzuia raisi kufanya anayojisikia yeye
Hivyo kama tutafanikiwa kuunda mifumo hiyo niliyoitaja lazima tuendelee kwa kuwa kila uongozi unapoingia unakuwa na mahali rasmi pa kuanzia.Pia itasaidia kuondoa mkanganyiko wa kila uongozi kuanzisha mambo yake na kuvuruga yale yaliyokwisha fanywa na watangulizi wake.Pia hii itatuondolea hofu ya kuchagua serikali ya upinzani kwakuwa yeyote atakaeingia hawezi kuharibu nchi kwakuwa mifumo tayari ipo kinachotakiwa ni kuiendeleza na si kkuivuruga.Kwa mfano mifumo imara ndio inaoiokoa Marekani kwa sasa dhidi ya Trump alieonekana kutaka kuvuruga nchi .
Tatizo la mfumo ndilo linalomkabili Magufuli.ushahidi ni pale bandarini ambapo amebadilisha watu( uongozi) kila kukicha lakini bado matunda ya bandari hayaonekani huku akiendelea kukamata ufisadi kila akienda huko.Pia kule TRA amefanya mabadiliko mara kadhaa bila mafanikio.Kule nishati na madini nako ni yaleyale.Tatizo siyo watu bali ni mfumo kwani ukimweka mtu safi kwenye mfumo mbovu bado hutapata matokeo bora