Pengo awalipua Maaskofu, asisitiza uamuzi wa aina ya kura ni wa mtu binafsi

Pengo ni mmoja wa watu wanafiki kuliko maelezo,hivi alikuwa na maana gani kuruhusu waraka usomwe makanisani halafu anaibuka na tamko lake!!! Ukiona maccm yanakufurahia jua wewe ni fisadi na mnafiki mwenzao
 
Serikali ina haki ya kuhamasisha kura ya NDIYO kama UKAWA walivyo na haki ya kuhamasisha kura ya hapana. Ila hawa viongozi wa dini wanapaswa kuwa kati. Waige mfano wa viongozi wa kiislam. Huwa hawatoi matamko yanayoligawa taifa

Ni kweli viongozi Wa kiislamu huwa hawatoi matamko hata kama yanatolewa ni nadra sana kusikia
Kwa mfano ijumaa ilopita nilipita eneo la Tandika wakati Wa swala ya ijumaa nikamsikia Imamu Wa msikiti akiongelea suala ya katiba Pendekezwa, alichokisema imamu huyo ni hiki " Ndugu watukufu waislamu suala lililopo mbele yetu juu ya mustakabari Wa nchi yetu ni hili la katiba pendekezwa, ndugu qaislamu Mimi kama imamu wenu nawashauri msiende kuipigia kura ya ndiyo au hapana na wala msiende kujiandikisha kwa kufanya hivyo mtawapa nafasi hawa mafisadi kuiba kura ili kupitisha katiba ambayo inatokana na ulevi na uhuni Wa viongozi tulionao"

Imamu Wa msikiti huo alienda mbali zaidi mpaka akamtaja mwalimu Nyerere akasema "ndugu watukufu waislamu nchi yetu ilipatwa kutawaliwa vizuri kwa miaka ya mwanzoni tu ya Uhuru wetu, hata kwa wakati Wa awamu ya pili mwalimu alikuwa akikemea uchafu ulokuwa ukitokea nchini, Leo oneni ni kiongozi gani mstaafu anaetoka mbele ya hadhara na kukemea uovu uliopo hakuna, hakuna kabisa"
 
Hakuna sehemu Pengo amekosea yeye katoa ushauri tu wala ushauri wake hauna nguvu ya kubatilisha kilichokubaliwa na TEC
Kuna watu pengine wanadhani Pengo ni ndo Kiongozi wa kanisa katoliki Tanzania kiasi kwamba anaweza kuliamulia Kanisa katoliki Tanzania ukweli ni kwamba mamlaka ya Pengo yanaishia jimbo la dar es salaam peke yake Cheo cha ukaeidinali ni kwa ajili ya kumshauri papa tu
 
Askofu Pengo ni makini sana! Abarikiwe na azidi kufuata nyayo za MTAKATIFU NYERERE!
UHURU NA AMANI YA TANZANIA HAVIKUSHUKA KAMA MVUA!
 
Serikali ina haki ya kuhamasisha kura ya NDIYO kama UKAWA walivyo na haki ya kuhamasisha kura ya hapana. Ila hawa viongozi wa dini wanapaswa kuwa kati. Waige mfano wa viongozi wa kiislam. Huwa hawatoi matamko yanayoligawa taifa

Shindwa pepo, kwa hiyo serekali ni chama cha siasa mpaka kishindane na vyama vya siasa!? Ama serekali imevaa koti la ccm hivyo wao wamaruhusiwa? Kwa akili yako fupi katiba ni suala la kisiasa ama mistakabali wa taifa ambapo kila mtu ni mdau sawa na mwingine, kwenye katiba hata JK ni sawa,na mkulima wa matikiti huki goba. Katiba ni sehemu ya kutunga kanuni za mchezo haiwezekani yoyote ajitungue kanuni bila ridhaa ya wote.
 
Askofu Pengo ni makini sana! Abarikiwe na azidi kufuata nyayo za MTAKATIFU NYERERE!
UHURU NA AMANI YA TANZANIA HAVIKUSHUKA KAMA MVUA!
 
Yaani maaskofu wote wa kikatoliki nzima wako chini yake?.Msaada kwa anayejua...
 
Pengo ni mnafiki na anatumika sana. Nadhani ni wakati muafaka sasa kwa baraza la maaskofu kula nae sahani moja.

Umesema murua kabisa,maana sasa hivi amekuwa upande wa Mafisadi hayupo tenda upande wa Wanyonge wa Tanzania. Na namshangaa anapata wapi mamlaka ya kumpinga ''Bosi'' wake Raisi wa TEC Mhashamu Askofu Mkuu Ngalelikumtwa.
 
Umesema murua kabisa,maana sasa hivi amekuwa upande wa Mafisadi hayupo tenda upande wa Wanyonge wa Tanzania. Na namshangaa anapata wapi mamlaka ya kumpinga ''Bosi'' wake Raisi wa TEC Mhashamu Askofu Mkuu Ngalelikumtwa.

Huyu mzee ana rangi mbili. Ni mtu wa maslahi, kama ni mkweli basi awapinge na viongozi wa serikali wanaposema wananchi waisome na kuipigia kura ya "NDIYO" katiba pendekezwa. Hivi ni kweli kwamba Pengo hajui kuwa katiba pendekezwa ilipitishwa kibabe tena bila maridhiano? Ni mnafiki sana huyu.
 
hapana, maaskofu wakuu ndo wapo chini ya cardinal, maaskofu wengine wapo chin ya maaskofu wakuu sawa na walimu kuwa chini ya mwalimu mkuu, afu mwl mkuu chini ya afisa elimu wa wilaya. ipo hivi papa......curia(cardinals)....archbishops (askofu mkuu).....bishops.....priests.....katekista.
 
Naomba nikusaidie katika hili mkuu. Kadinali pengo ni askofu mkuu wa Jimbo kuu katoliki la Dar es Salaam. Kwa utaratibu wa kanisa katoliki kila askofu ni kuu katika jimbo lake na anawajibika moja kwa moja kwa Baba mtakatifu-Vatikan. Cheo cha Ukadinali anaweza pewa hata padre wa kawaida asiye askofu (hapa najua hata wakatoliki wengi hawalifahamu hili) na ndiyo maana sio kila nchi ina Kadinali. Ukadinali hupewa baadhi ya viongozi wa kanisa kama washauri wa karibu wa papa na watu hawa pia hukabidhiwa parkia zao maalum Italy kama wakuu wa parokia hizo.

Nitajaribu kukutafutia link zaidi yenye maelezo hayo ili kuwaelewaesha wengi hasa wasio wakatoliki ambao hudhani Pengo ni mkuu wa kanisa katoliki tanzania. Kwa ufupi kanisa katoliki popote duniani halina kiongozi mkuu katika nchi husika. Japokuwa Maaskofu wamejiwekea utaratibu wao wa kuwa na raisi wa baraza ambaye ndiye huendesha vikao vya maaskofu nchini.
 
Yaani wewe umejiunga tu na jukwaa unaanza kukashifu viongozi wa dini?

Hao ni akina nani wasizungumzwe?

Ni binadam kama sisi na wanaongozwa na unazi kama alivyo Mapengo...

Nimekuja kugundua viongozi wa dini ni watu overrated kupita kiasi,sometimes ni watu wa hovyo sana

Kwa mtu yeyote rational,anachukulia binadam wote ni sawa,na anawatreat sawa

Viongozi wa dini 90% ni bunch of frauds,wakwende zao....
 
Uaskofu wa Pengo unaishia pale Bwawani.akiingia Morogoro anaomba kibali kwa askofu wa Morogoro..Rais wa TEC ndio kiongozi wa maaskofu wakatoliki Tanzania
 
Back
Top Bottom