Siku za ajabu
JF-Expert Member
- Dec 23, 2012
- 1,369
- 987
Naona kama ile single ya 'Vifaranga na mama yao' imemgeuka!Zzk ni MM sasa connect dots hapo mipango ifanywe bila mkuu kujua itawezekana?Yuda kakamatwa pabaya..
Nilitegemea sana kuwa Zitto Kabwe angekuwa mtu wa kwanza kuwanyoshea kidole wale walioandaa waraka wa siri wa mabadiliko bila kumuhusisha nakumweka kwenye hali tata aliyonayo na chama cha CHADEMA. Nasema hivi kwa misingi ya kile kinachosemwa kuwa - imedaiwa hakuhusika na hakujua lolote kuhusu huo waraka. Kwa mantiki za kikawaida alitakiwa amutuhumu kwa nguvu zote Dr.Kitila na wenzake kwa hilo la uandaaji wa waraka unaomuhusu bila ridhaa yake. Kinachoonekana yeye Zitto anaungana na kundi la Kitila katika kuushutumu uongozi wa chama kwa hatua zilizochukuliwa. Iweje mtu makini ukubaliane kirahisirahisi vile na kundi la watu (hata kama ni rafiki zako) walioandaa waraka unaokutumbukiza kwenye matatizo bila kukupa taarifa kabla? Kuna siri gani hapo?!!!!!!
Na watimuliwe tu, yeye na wafuasi wake.. hiyo ndo ya habari vijijini.Kampeni kubwa sasa ng'oa na ondoa kbc zzk and ccm,, habari ya mjini
Naona kama ile single ya 'Vifaranga na mama yao' imemgeuka!
Mtazamo wako ni FINYU sana.Una ELIMU gani ndugu?Zito angekubali kuitwa john Paulo angekubalika chadema ila na uzuberi wake unatarajia nini? Chadema inamsafisasha aliyekubali kutenda makosa wazi ambaye ni dr. Kitila na kumshambulia anayetuhumiwa. Double standard inayosababisha na nguvu ya kiimani. Ni mtazamo yangu.
Nimewiwa kumtetea Zitto Kabwe na Freeman Mbowe na Dk. Wilbrod Slaa. Nina mashaka sana hakuna mwenye makosa, na kwamba tunachokiona kama machafuko katika CHADEMA katika hizi siku mbili tatu unaweza uwe ni mgongano tu wa taaluma mbili ndani ya Chama.
Kama Zitto Kabwe alipata Elimu ya Political Economy pale Chuo Kikuu Mlimani au kwingineko, yeye ni Mwanasiasa wa Kusomea. Sifa za Wanasiasa duniani zinajulikana. Ni watu wa kutafuta sifa, kujikweza na kutaka dunia nzima isikie na kujua kwa uhakika ni kipi hasa walichofanya.
Kwa hiyo Siwezi kushangaa kama nitasikia Zitto Kabwe akijisifia kupandisha bendera ya CHADEMA akiwa na umri wa miaka 16. Huyu ni mwanasiasa wa kusomea, na hapo atakuwa anafanya siasa kadri ya mafunzo yake.
Nasita kumzungumzia sana Dk. Kitila Mkumbo kwa kuwa hakuna ninachokijua zaidi ya kwamba ni Mwalimu wa Chuo Kikuu. Lakini wote tunajua huwezi kumtenga sana mwalimu na siasa kwa kuwa hii ni taaluma inayohusu kujieleza, na mwanasiasa sharti ajue kujieleza. Kwa hiyo naomba nimwite Dk, Kitila Mkumbo kuwa na yeye ni mwanasiasa wa kusomea.
Nitamjadili zaidi Zitto Kabwe hapa kwa sababu mzozo unaoonekana kuwapo katika CHADEMA leo unaonekana kuwahusu zaidi watu wawili hata kama wengine wameingizwa humo: huu mgogoro unamhusu Zitto Kabwe na Freeman Mbowe.
Freeman Mbowe ni Mfanyabiashara kama mimi, japokuwa tunapishana viwango kwa mbali kama ardhi na nyota. Lakini ndege ni ndege tuawe analala katika banda au kwenye mti; watakuwa na mambo yanafanana.
Sisi wafanyabiashara huwa tahupendi urasimu. We are doers. Kikao cha familia kikishakubaliana kuwa tunataka duka lijengwe hivi mahali, lipakwe rangi hii, tuweke nondo kwenye madirisha. Kitu cha muhimu ambacho huwa kinabakia hapo huwa ni results! Siyo Nani katoa hela, zilitoka saa ngapi, mkono gani ulizishika wakati zinatoka na upuuzi mwingine wa kuchelewesha results.
Nimeamka mapema sana leo kuandika mawazo haya kwa sababu sitaki kuona ugomvi katika CHAMA tegemeo la wananchi baada ya CHAMA kaka kuharibiwa. Pengine ni kweli Mbowe kafanya unilateral decisions katika mambo yanahusu fedha. Naamini hilo litakuwa lilifanywa kuharakisha results. Urasimu una desturi ya kuchelewesha sana results. Nionavyo mimi Chama kimefanya mambo mengi sana mazuri na kuna mafanikio makubwa yamefikiwa na yanaonekana hadi hapa tulipo chini ya uongozi wa Mbowe.
Tatizo ni kwamba mambo yanayofanywa na fedha za chama hayajapeleka sifa kwa kila mwanasiasa ambaye angependa fedha za CHAMA zitumike kumpa sifa na yeye pia. Hapa kuna tatizo la sifa!
Naamini Mbowe hajaiba fedha CHADEMA kama kambi ya Zitto inavyotuhumu. Naamini kinachoelezwa kuwa udikteta wa Freeman Mbowe katika CHADEMA ni mgongano wa mitizamo ya utendaji unaojitokeza kutokana na taaluma mbili kugongana. Zitto Kabwe angependa kila kinachotendeka kilete sifa kwake pia. KInachotendeka pale katika chama kinaleta sifa kwa mtu mmoja tu anayeamua kipi kifanyike.
Inawezekana kabisa ni kweli Mbowe anafanya maamuzi ya kiimla. Wafanyabiashara wengi wapo hivyo mara nyingi kwa sababu ya kuwahi kukamilisha lengo. Tupo Goal Oriented. Na ni rahisi sana kuwakwaza watu katika mazingira hayo kutokana na sifa za manunuzi say ya pikipiki zinunuliwe wapi kutokumpatia sifa na Zitto Kabwe. Maswali ambayo napenda kusikia wanaCHADEMA wakiuliza ni haya: Mbowe kaiba Sh. Ngapi? La pili likiwa hili: kwamba ni kitu gani katika manunuzi ya CHAMA kilipangwa kufanywa ili kufaidisha chama hakijafanywa na kufaidisha chama?
Hoja ya Umamluki wa Zitto nayo inaweza kupata maelezo: kwamba taaluma ya upelelezi tangu mwanzo wa historia ya binadamu imehusu neno moja tu katika lugha ya Kiingereza--neo EMBED.
Ku-embed ni kupandikiza mtu miongoni mwa jamii inayopelelezwa kwa namna ya kumwezesha kuonekana ni mmoja wao. Mpelelezi anayefaulu katika kazi yake ni yule anayemudu ku-embed mwenyewe, au kwa kuwezeshwa. Kwa maana hiyo, mpelelezi mzuri atazungumza lugha ya wenyeji, atavaa mavazi ya wenyeji, atakula chakula cha wenyeji, atafanya biashara kama wenyeji, hata atazaa na wenyeji, atakuwa mmoja wao, ataishi kama wao. Kumtambua mpelelezi aliye-embed vizuri ni ngumu sana. Unaweza usijue milele yote. Kwa wale waliosoma Biblia mifano ni mingi mule, mzuri kuliko yote ukiwa mfano wa Mpelelezi Delila, ambaye alitumia mbinu inayoitwa honey trap kumpeleleza Samsoni kwa niaba ya Wafilisti.
Waliobobea katika taalum ya upelelezi watasema njia pekee ya kumtambua mpelelezi miongoni mwenu ni kusoma associations zake nje yenu. Associations za nje ni mahusiano yake na watu waliopo nje ya kundi lenu. Kwa hiyo mtatizama mahusiano yake na watu kitaaluma, kidini, kimapenzi, kibiashara, kimichezo kwa namna iwayo yote itayoweza kutoa picha ya associations za suspect.
Mkipata undani wa hizo associations zake sasa mtasikiliza huwa anasema nini anapokutana na hao watu katika associations zake kwa siri. Mtamsikiliza kwa kutumia njia halali au njia haramu; au vyote kwa pamoja ikibidi. Kujua sana ilani za chama, na katiba zake, na sera zake, na historia yake, SI sababu tosha kumtoa mtu kwenye list ya mapandikizi. Pandikizi anatakiwa kuvijua vyote katika chama anachokipeleleza, sawasawa kabisa na shetani anavyojua vifungu katika Biblia.
Ili kujua kama Zitto ni Jasusi wa CCM, labda sasa CHADEMA watuambie waliupata wapi huu waraka unaoitwa mpango wa hujuma. Je waliupata kwenye Kambi ya CCM? Je waliupata kwenye associations zake nje ya chama?
Mwisho napenda kuwasihi WANACHADEMA kukubali kwamba pengine Zitto hana makosa. Na kama huu ndo ukweli, basi naomba Mbowe na Dk. Slaa watoe majibu ya haraka kuhusu kila alicholalamikia Zitto.
Achana na upuuzi wako.
Chadema sio Mbowe wala Slaa au Zitto. Vikao vya chama vikifanya maamuzi yawe ya makosa au sio makosa inabidi yaheshimiwe. Kamati kuu sio Mbowe na Slaa , kuna watu wengi wenye akili timamu.
Sisi tusiokuwa mashabiki wa watu tunaona hizi hatua zilizochukuliwa zitatia watu adabu wanajiona wako juu ya chama.
Msifanye tafukuri za kijinga hapa. Chadema sio kilabu ya pombe ya kila mnywwaji anabwatuka kivyake.
Chama makini usimamia maamuzi yake hata kama yana kosa
Zito anaonekana kuchanganyikiwa ndio maana nafanya very silly decisions kama ya kuwa-flanked by defiant group of masalia type. Mentors wake wamshauri to remain dumb until his defense is delivered. When the decision is made he will have comfortable space to hit what he purports to be an unguided missile. (sic) Otherwise he is strategically committing political suicide.Bwana Highlander,pamoja na mawazo yako mazuri ya kuelimisha,naomba nikuulize swali moja:
Wakati Zitto anaenda kujibu tuhuma pale Serena hotel;ukumbi ule ambao angeutumia Zitto kujibu mapigo,uliandaliwa na kupambwa na Stellah Mwampamba na baadhi ya vijana wa ccm;---- uhusiano gani hapo?
You are quite right brother Kapongoliso.Let him learn from your point.Zito anaonekana kuchanganyikiwa ndio maana nafanya very silly decisions kama ya kuwa-flanked by defiant group of masalia type. Mentors wake wamshauri to remain dumb until his defense is delivered. When the decision is made he will have comfortable space to hit what he purports to be an unguided missile. (sic) Otherwise he is strategically committing political suicide.