Nichumu Nibebike
JF-Expert Member
- Aug 28, 2016
- 8,658
- 15,784
Katika kipindi hiki cha majonzi kwa wafiwa na wale wote walioguswa na ajali, niljaribu kutafakari wale ambao walibahatika kupona. Sio kupona kwa kuwa wamenusurika na ajali, bali kwa kuwa waliachwa nyuma kwa 'kukosa sifa za kuwa kwenye safari hiyo'...
Hiyo ilikuwa safari ya kwenda kufanya mtihani wa mashindano na tunajua kila shule huwa inapeleka the best team kwenye mashindano ya mtihani. Yani wale vichwa wanaoongoza darasani ndio huwa wanachaguliwa kuwakilisha shule.
Najaribu kupata picha katika safri hii baada ya wanafunzi cream kuchaguliwa, kuna wale waliosononeka kuwa, na mie ningekuwa na akili kama fulani, ningekwenda kuiwakilisha shule yangu na ningekuwa kwenye ile safari.
Hili nalifee personally maana kuna kipindi wakati niko form two shule yetu ilichagua watu cream kwenda kucheza mpira kutoka Mbeya mjini hadi Rungwe... Nilipowaona wenzangu wakipanda gari la shule wakituaga kwa mbwembwe na bashaha, nilitamani na mie ningekuwa na kipaji cha kucheza mpira, basi ningebahatika kwenda Rungwe kucheza mpria...
Basi sasa leo hii wale waliokuwa wanaomboleza wanatambua ni jinsi gani wamekuwa na bahati ya kupata nafasi ya kuendelea kuishi na jinsi wale waliokuwa wanaonekana na bahati wamepata tukio la kuhuzunishwa.
Hata huko porini kuna wanyama kama Swala walikuwa wakihuzunika kwa nini wao wamepewa pembe ndogo, na wanyama wengine kama punda milia wakisikitika kwa kukosa pembe kabisa, wote hawa wakiwatamani tembo na faru kwa kujaaliwa pembe kubwa.
Embu wafikirie tembo na faru walikatishwa uhai kwa ajili ya kile kitu wanyama wengine wanachokitamani!
Vivyo hivyo mpenzi msomaji, usisikitike kwa kutokuwa na kile amacho wenzako wanacho na unakitamani, labda ungekuwa mzuri sana wa sura usingeweza kumaliza shule maana waalimu wangekufelisha mitihani kwa kukataa kutoa penzi, labda ungekuwa tajiri leo hii ungeshauliwa na majambazi kwa kuwa tu wanataka pesa zako, labda leo hii ungekuwa na akili nyingi za darasani ungekuwa umeshakufa kwenye ajali ya ndege ukiwa masomoni kwenda ng'ambo...
Kwa hiyo huenda vile ulivyo na mapungufu yako ndio sababu ya wewe kuwepo hai mpaka leo. USISIKITIKE!