kidi kudi
JF-Expert Member
- May 17, 2011
- 2,419
- 1,981
Kwa muda mrefu vilabu vyetu, wadau na mashabiki wamekuwa wakilia na kulalamikia sana maamuzi yanayoamuliwa na waamuzi wetu kwenye mchezo pendwa wa soka ama kandanda au kabumbu kama linavyofahamika na wengi.
Nimekuwa nikijiuliza hili suala la wenzetu hasa wale wa nchi za Ulaya walivyofanikiwa kuleta hii teknolojia ya matumizi ya VAR katika kusaidia waamuzi kufanya maamuzi hasa yale yanayoonekana yana utata, kwamba kwa huku kwetu kwenye ligi yetu ya VPL hatuwezi na sisi kuja na VAR yetu kivyetu vyetu tukipata msaada toka picha za video za AZAM TV hasa kwa zile channel zinazorusha mubashara hizi mechi zetu?
Napendekeza msimu ujao viongezeke vitu viwili kama ifuatavyo;
1. Awepo refa mwingine wa ziada ndani ya gari la kurushia matangazo za AZAM ambae kazi yake itakuwa ni kuangalia tena video mgando ya tukio lenye utata na kisha kutoa taarifa hiyo haraka kwa mwamuzi wa nje mezani (fourth official) ili nae awasiliane na mwamuzi wa kati, kisha
2. Pawepo na ka flat screen hata ka 32" ambako katakua hapo nje kwa huyo 'fourth official' ambako katakuwa kanaonyesha mchezo husika live toka kwenye gari la matangazo la AZAM maalum kwa mwamuzi wa kati kwenda kujiridhisha na maamuzi aliyo/atakayo yafanya (kama vile ambavyo wenzetu wafanyavyo hukooooo majuuu).
Hebu tujaribu kuanzia hapo naamini kwa kiasi fulani malalamiko yapungua kwa kiasi fulani.
NINAPENDEKEZA!