PENDEKEZO: Tuwe na VAR yetu ya kivyetu vyetu

Moja kitu nilichofahamu hivi karibuni, endapo kuna wazo au unahitaji implementation fulani basi liweke katika formal na lifikishe kwa wahusika.

Tunaweza andika barua kuzitaka timu zinazoshiriki Ligi Kuu kupitisha ombi Ligi Kuu, Bodi ya Ligi na TFF kuanza kutumia VAR.

Tunaweza kuziandikia Ligi Kuu, Bodi ya Ligi na TFF kuzitaka kuanza kutumia VAR, nadhani hii ndio njia rahisi ya kufikisha mawazo.
 
Mwenye kufahamu, Azam TV kupitia (Uhai Productions) wanafunga kamera ngapi katika mechi?
Sijui game kubwa, ila game ndogo hizi, huwa nahisi ni camera moja tu, mwanzo mwisho game unaiona kwa mtindo mmoja tu, zaidi wafanye kuvuta mpira ukiwa upande wa pilj basi.
 
Sidhani kama itafanikiwa maana naliona tatizo kwa azam tv pia. Azam tv hawana kamera nyingi zitakazo fanikisha kurudia tukio na kuonekana kwa usahihi zaidi. Mfano tukio la goli la yanga dhidi ya mbeya city mpaka leo hii hakuna mwenye uhakika kama ule mpira ulivuka mstari au la maana marudio ya azam tv hakuna sehemu walipo onyesha kama mpira ulivuka mstari au la.

Matukio ni mengi tu azam tv wakirudia hayaonekani vizuri.Kwa hiyo ili angalau twende sawa Azam tv waongeze kwanza kamera.
yote yanawezekana tu, zinawekwa kamera upande wa kibendera kila goli kamera moja moja, lakini pia inaweza kukubalika kwanza ni matukio gani yaweze kuangaliwa kwenye luninga mfano, yataanza kuangaliwa matukio ya offside na maamuzi kuhusu penati kwani hayo ndio matukio aghalabu hujitokeza katika ligi yetu..tutaanza taratibu kisha hayo mengine yatafuatia taratibu taratibu
 
Sijui game kubwa, ila game ndogo hizi, huwa nahisi ni camera moja tu, mwanzo mwisho game unaiona kwa mtindo mmoja tu, zaidi wafanye kuvuta mpira ukiwa upande wa pilj basi.
Whaat! Unamaanisha mechi inaonekana Vertical 15° to 27° tu hamna wakati hata mchezaji, referee au benchi wanaoneshwa?
 
yote yanawezekana tu, zinawekwa kamera upande wa kibendera kila goli kamera moja moja, lakini pia inaweza kukubalika kwanza ni matukio gani yaweze kuangaliwa kwenye luninga mfano, yataanza kuangaliwa matukio ya offside na maamuzi kuhusu penati kwani hayo ndio matukio aghalabu hujitokeza katika ligi yetu..tutaanza taratibu kisha hayo mengine yatafuatia taratibu taratibu
yaah inawezekana cha muhimu marudio ya tukio yawe clear.
 
VAR ya kivyetuvyetu itasaidi watu kutosusa na kujitoa kwenye ligi.
Itaondoa vitisho kwa marefarii kutishiwa kupigwa na wale jamaa.
Malalamiko kwa tff,Simba,Mo na Haji Manara pia yatapungua.
 
Tatizo azam huwa wanakuwa na camera 5 tu. Kuna tukio lilishawahi kuleta utata mwaka juzi na camera hazikuona
 
Tatizo azam huwa wanakuwa na camera 5 tu. Kuna tukio lilishawahi kuleta utata mwaka juzi na camera hazikuona
At least! Mchezo urushwe na kamera 10.

Kamera Kuu 'Coverage Cam'.
Sidelines Cams 2
Goal line's Cams 2
Positioning Cams 2
Behind Goals Cams 2
Other Sided Cam

Camera 3 katika hizi vyema zikiwa Gimbal's, hasa Positioning Cams na Sidelines Cams.
 
Hii kitu Utelembwe fc, a.k.a Paka Shume fc hawawezi kuikubali itumike, maana wao wamezoea vya kunyonga tuu.
 
Back
Top Bottom