Pendekezo: Sam Mahela awe mfanyakazi bora 2012/2013

Pendekezo: Sam Mahela awe mfanyakazi bora 2012/2013

King Kong III

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Posts
60,374
Reaction score
88,609
Umofia kwenu wana bodi,

Poleni ambao hamna umeme ila kwetu wakukinga huku,Nimekuwa nikimfatilia huyu mtangazaji wa ITV Sam Mahela kiukweli jamaa anastahili tu(n)zo ya mfanyakazi bora wa mwaka 2012/2013 ndani ya Ipp Media, Nimeona hilo kutokana na kufanya mambo ambayo hata wengine hawawezi, moja ya matukio niliyoyaona ni lile la mama alivimba na mguu na jingine ni la leo ambalo mzee aliyetelekezwa na wanae miaka 8 na anajisahidia mumo ndani ya nyumba lakini jamaa aliingia na kushika mifuko iliyojaa nnya na kufungua maplastiki yaliyojaa mikojo(with bare hand)! Mengi tunakuomba umpe mfanyakazi bora wa mwaka 2012/2013.

Nawasilisha.
 
Ni kweli anastahili kwa namna alivyofanya bila kuona kinyaa. Big up Sam.
 
Anastahili kwa kweli binafsi wkt anashika mm nilikuwa najisikia kinyaa Mungu amsaidie cyo kila mtu anayeweza kufanya vile kwa mtu usiyemjua wengne hata ndugu hagusi
 
Binafsi namkubali yule wa kipindi cha dk 45
 
Anastahili kwa kweli,hasa kwa habari ya leo amenigusa sana!
 
Sam mahela hata mimi namkubali.
 
kwani kesi ya yule mama aliye zaa na mhindi then kumnyanganya mtoto iliishia wapi?
 
Akisha pata huo ufanya kzi bora yatamtokes kama ya herry muro,

Baada yakupata tunzo ya mwana habari bora akazushiwa mambo ya ajabu ajabu ilitu kumuua kihabari,

Kwa ma piiii piiii piiii yangu nikwamba bora abaki hivyo hivyo ilitufaidi habari zake,
 
Namkubali pia na mimi Mahela. Kazi zake zinagusa nyoyo sana. Ikiwezekana atengeneze vipindi maalum vyenye uelekeo huo.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Ni kweli anastahili pongezi kwa kuripoti matukio tata yaliyojificha lakini alichofanya leo sio sahihi.

Simpi credit kwa kushika mifuko ya vinyesi with bare hands. Ile si dalili ya upendo bali ni dalili ya kukosa umakini. Hakuwa na sababu yoyote ya kushika mfuko ule wala kuji-expose kwenye mazingira machafu ilhali hajui mgonjwa yule anasumbuliwa na maradhi gani.

Next time anapaswa kuwa makini. Huwezi kuonesha upendo kwa wife wako kwa kujipaka damu zake za hedhi usoni
 
Ni kweli anastahili pongezi kwa kuripoti matukio tata yaliyojificha lakini alichofanya leo sio sahihi.

Simpi credit kwa kushika mifuko ya vinyesi with bare hands. Ile si dalili ya upendo bali ni dalili ya kukosa umakini. Hakuwa na sababu yoyote ya kushika mfuko ule wala kuji-expose kwenye mazingira machafu ilhali hajui mgonjwa yule anasumbuliwa na maradhi gani.

Next time anapaswa kuwa makini. Huwezi kuonesha upendo kwa wife wako kwa kujipaka damu zake za hedhi usoni
Sure, awe makin sio sifa kushika vi2, Dunia inamaambukizo mengi, Taifa/familia inamuhitaji, awe makin
 
Umofia kwenu wana bodi,
Poleni ambao hamna umeme ila kwetu wakukinga huku,Nimekuwa nikimfatilia huyu mtangazaji wa ITV Sam mahela kiukweli jamaa anastahili tu(n)zo ya mfanyakazi bora wa mwaka 2012/2013 ndani ya Ipp Media,Nimeona hilo kutokana na kufanya mambo ambayo hata wengine hawawezi,moja ya matukio niliyoyaona ni lile la mama alivimba na mguu na jingine ni la leo ambalo mzee aliyetelekezwa na wanae miaka 8 na anajisahidia mumo ndani ya nyumba lkn jamaa aliingia na kushika mifuko iliyojaa nya na kufungua maparastiki yaliyojaa mikojo(with bare hand)! Mengi tunakuomba umpe mfanyakazi bora wa mwaka 2012/2013.

Nawasilisha.

King Kong Mi nakubaliana na wewe kabisa aise huyu jamaa anafanya kazi sana
 
uyu jamaa anastahili pongezi,waandishi wengi wa bongo wamekalia udaku fulan yuko na nani,amefumaniwa mara wamegandana,lakin uyu jamaaa anaangalia zaidi matatizo wanayopata wananchi,na anafatilia,ki ukweli jamaa na namkubali si mimi nimeona watu wengi wanamkubali,nitamtafuta nimpe ata ki prado
 
hata mi nimemuona. Yataka moyo aliyoyafanya
 
Amefanya yafuatayo yaliyogusa moyo wangu.
1. Dada aliyezaa na mhindiki kisha kunyang'anywa mtoto katika mazingira yenye utata. Baada ya kufuatilia na kufungua kesi hakimu akatoa hukumu kuwa yule mama alikuwa ni sahihi kunyanganywa mtoto kwasababu ya afya mama haikuwa nzuri. Ikumbukwe kuwa upande wa pili haukusililizwa na uthibitisho wa afya ya mzazi kutokuwa nzuri "kichaa" haukuwepo hali iliyoashiria mlungula kutembea toka kwa mhindi kwenda kwa hakimu. Msaada uliopatikana ni pamoja na kupata mwanasheria wa kumtetea yule dada ili aweze kupata mtoto wake hata kama wazazi wa upande wa pili walikuwa hawataki binti aolewe na kijana wao.

2. Yule dada wa Kibamba anayesumbuliwa na ugonjwa wa mguu kuvimba sana kiasi kwamba umeshakuwa na magamba. Anatakiwa kwenda India kwa ajili ya matibabu. Mara ya mwisho nadhani michango iliyotolewa na watu mbalimbali ilikuwa haijatimia kiasi kinachotakiwa. Pasipo Sam Mahela pengine hata hicho kilichopatikana kisingekuwa kimepatikana.

3. Kuna kijana alikuwa akimfungia mama yake ndani chumbani, hampi chakula, mama anajisaidia humo humo ndani na hiyo ilieleka majirani kutafuta jinsi ya kumsaidia huyo bibi. Nakumbuka aliongea naye Kiruga baada ya kugundua kuwa lugha ya huyo bibi naye anahifahamu na bibi ndo akafunguka vizuri kuwa kijana wake anamfungia humo ndani yeye anaenda kazini. mazingira ya chumba yalikuwa machafu, bibi kadhoofu kwa kukosa lishe bora.

4. Huyo mzee aliyetelekezwa na familia yake. Si jambo zuri katika jamii kufanya kitendo kama hicho na hasa mnapokuwa mnahishi na mtu kama huyo harafu hamumuudumii. Lakini hata wale wanataka kumsaidia mnawakasirikia. Hiyo inaonesha kuwa kuna kitu hakipo sawa ama wanataka kuchukua mali zake alizokusanya na kwahiyo wanataka apotee kwenye uso wa dunia mapema au kuna jambo lingine.

"UNDUGU SI KUFANANA BALI KUFAANA"
Hawa watu wawawezi kupinga kuwa Sam Mahela amekuwa ndugu yao maana amewafaa sana kwenye maswahibu waliokumbana nayo na amekuwa msaada mkubwa.
Sam ameonesha ni matatizo gani yanaikumba jamii, pengine kwa hayo jamii inajifunza kitu. Mimi ninajifunza.
 
Back
Top Bottom