Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,198
- 25,517
Hapo mwaka 2015 tutakapochagua viongozi wetu kwa kipindi kitakachowekwa na Katiba,napendekeza kuwe na kura ya wazi. Wapigakura wafike vituoni na kutamka kupigia chama fulani au mgombea fulani. Kwanza,itarahisisha kuhesabu kura.Pili, mshindi atajulikana mapema.Tatu, kura kuibiwa itakuwa ngumu sana.
Ni vyema vyama vinavyotaka kura ya wazi kwenye kupitisha Katiba vikajenga hoja hii. Kwamba,hapo mwaka 2015 katika Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani,kura iwe ya wazi. Upigaji huu wa kura hautamlazimisha mpigakura kuondoka nyumbani baada ya kupiga kura yake.Atakuwa na haki ya kubaki na kusikiliza wenzake wanasemaje na wamemchagua nani. Kwakuwa kampeni zitakuwa zimeshafanyika,itakuwa ni kutaja tu mchaguliwa.
Hii hoja vipi wanasiasa wa Tanzania?