kali linux
JF-Expert Member
- May 21, 2017
- 2,299
- 6,102
Hello bosses and roses..
Kuna kitu nimekua nafikiria kwa muda mrefu, sina uhakika sana kuhusu uwepo wake kwa sasa au inawezekana kipo lakini kinafanyika kwa njia zisizo rasmi.
Hebu fikiria scenario hizi
1) Mtu au Biashara au Kampuni X imepata tenda ya kufanya project fln na mkataba ukasainiwa kati ya wahusika. Sasa X akaona labda mambo yamemuendea vigumu ili kukamilisha mradi huo, scenario hio huwa inaleta aidha migogoro au kufikia hatua ya kuvunja mkataba.
2)Mtu au Biashara au Kampuni X imepata mkataba wa kufanya projecf fulani lakini ikatokea inahitaji kiasi fulani cha pesa ambazo zinaweza kulipika endapo projecf hio ikikamilika lakini X hana assets au credit rating nzuri inayomuwezesha yeye kupata mkopo bank lakini mazingira ya huo mkataba yanaridhisha na mteja wake ana reputation na portfolio nzuri hivyo kuhakikisha ulipaji.
Sasa kwa hizo scenarios mbili nadhan utaona umuhimu wa kuwepo na soko huria la mikataba ambalo litakua regulated kuhakikisha validity ya parties zote mbili kwenye mkataba husika na kisha kuruhusu transactions na exchanges za mikataba kuendelea.
Hii itatua changamoto nyingi sana hasa kwa makampuni yetu ya ndani na biashara zinazochipukia. Lakini pia itaongeza ufanisi kwenye kukamilisha projects mbalimbali ambazo hukwama kwa sababu ya contractor kutokua na uwezo wa kifedha muda huo.
Je jambo kama hili tayari lipo? na kama lipo linafanyikaje hapa Tanzania?