Joseph Mshinga
JF-Expert Member
- Aug 27, 2014
- 232
- 143
Na:Joseph Mshinga.
Msisitizo wangu uko palepale kuwa Mshindi halali atangazwe na si vinginevyo. Hakuna cha kutangazwa hali ya hatari, sijui habari za katiba mpya mara serikali ya umoja wa kitaifa . Hakuna sababu kwa yote haya. Mshindi atangazwe.
Jecha ashitakiwe.
1.Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na ile ya Zanzibar ya mwaka 1984 inaitaka tume ya uchaguzi ya Zanzibar(ZEC) kushauriana mara kwa Mara katika kutekeleza majukumu yake na tume ya uchaguzi ya Taifa(NEC)
Kitendo cha Jecha kufanya maamuzi ya kufuta uchaguzi bila takwa la kikatiba la kushauriana na tume ya Taifa ni dhahiri kuwa amekiuka na kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar. Hivyo anapaswa kufunguliwa kesi ya kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar.
Ieleweke kuwa mashauriano yanayotakiwa kufanyika ni kati ya ZEC na NEC. isije kueleweka vibaya kuwa ni kati ya Jecha na NEC. hata kama Jecha alifanya mashauriano na NEC na mashauriano hayo hayajaripotiwa bado hayo si mashauriano ya ZEC na NEC bali ni mashauriano ya Jecha na NEC ambayo hayatambuliki kikatiba wala kisheria. Jecha ni mmoja ya wajumbe wa ZEC akiwa Mwenyekiti na ili ionekane kuwa ZEC imeshiriki basi uamuzi ule ulipaswa kuwa umejadiliwa kwanza ndani ya ZEC kitu ambacho hakikufanyika maana wajumbe walishakana tayari.
Hivyo Jecha kavunja katiba ya nchi na anapaswa kufunguliwa mshitaka.Hili ni kosa la kwanza.
Ieleweke pia kuwa Tume ya uchaguzi ya Zanzibar na NEC ya Taifa hazina kinga ya kutoshitakiwa. Vivyo hivyo hata Jecha hana kinga ya kutokushitakiwa juu ya uvunjaji wa katiba na sheria alioufanya. nasisitiza kuwa hana kinga ya kutoshitakiwa. Kisichoruhusiwa ni matokeo kuhojiwa mahakamani mara baada ya kutangazwa lakini si kushitakiwa kwa TUME yenyewe wala wajumbe na mwenyekiti wake.Hivyo sheria ichukue mkondo wake kwa Jecha.
2.Sheria ya uchaguzi ya Zanzibar namba 11 ya mwaka 1984 imeweka sharti kuwa uamuzi wowote wa tume ya Zanzibar ni sharti uwe umefanyika kwenye Kikao halali na tena kiwe na akidi inayotakiwa.
Kwa kuwa hakuna kikao cha Tume kilichofanyika kujadili na kuamua kufutwa kwa uchaguzi basi hili ni kosa la pili kufanywa na Jecha kwa kuvunja kifungu hiki cha sheria. Hivyo anapaswa kufunguliwa mashitaka kwa kuvunja kifungu hiki cha sheria ya uchaguzi.
3.Katika tamko lake la kufuta uchaguzi Jecha alikaririwa akisema kuwa kwa mamlaka aliyonayo basi anafuta uchaguzi wa Zanzibar.
Kwa kuwa Katiba ya Zanzibar na sheria ya uchaguzi Zanzibar hazimpi mamlaka mwenyekiti wa Tume kufuta uchaguzi basi atakuwa ametenda kosa kwa kukiuka sheria na kujipatia mamlaka ambayo hana.Anapaswa kufunguliwa mashitaka kwa kujipachika mamlaka ambayo hana kisheria wala kikatiba.
Mwisho naendelea kusistiza kuheshimiwa kwa maamuzi halali ya Wazanzibar.
Joseph Mshinga
12/11/2015.