Kwanza nawasalim
pili naomba kuwashauri kwakuwa polisi wamezuia maandamano yetu ya kesho kwa visingizio mbalimbali ikiwemo ya mchina kuja tanzania na ccm kufanya maandamano kesho hiyohiyo naomba nishauri yafuatayo kesho tuwaachie ccm waandamane na mchina aje tanzania sisi tupange maandamano yetu siku nyingine na nashauri yawe baada ya pasaka na iwe siku ya j mosi ili kupata wafuasi wa kutosha maana siku za kazi wengine tunafanya kazi serikalini tukiacha kazi tukaenda kuandamana tunaweza kupoteza kibarua pili tukilazimisha kufanya kesho wakati wameshakataza mwitikio utakuwamdogo na wao wakapata ya kusema. Naomba tutumie busara nawasilisha.
wazo linazungumzika ila tujiulize yafuatayo؛
1. Cdm walipopanga tar.25 siku ya j3 kuna vigezo walizingatia
2.kati ya hizo sababu walizotoa polisi kuwa xi jinping na ccm kuandamana zina holdwater?
3.cdm wakibadili tarehe kwa kuzingatia ushauri wako kahali hii kandamizi watapewa kibali?
alipoulizwa itakuwaje maana kutakuwa na
ugeni wa rais wa china nchini, sababu
ambayo hata serikali imeitumia ili kuyazuia
maandamano hayo, mbowe alijibu:
"kilio chetu hakikuja na rais wa china, kama serikali ya ccm wanaona aibu
kumwajibisha waziri mmoja na naibu wake,
basi wasubiri aibu ya dunia kuona jinsi
tanzania inavyoendeshwa kibabe, ikiwa
haina elimu bora.
"tumetangaza maandamano wiki tatu
zilizopita, hatukuwa na taarifa na ujio wa
rais wa china, lakini jinsi mungu alivyo
upande wetu amemleta rais wa china,
kweli mungu ni mwema, hakuna tena nafasi
ya kusubiri kuficha ubovu katika sekta ya
elimu nchini, ndani ya siku ambayo
chadema waliandaa maandamano ili dunia nzima isikie kilio cha watanzania kuhusu elimu.
"sababu kuwa ccm nao wameandaa
maandamano kupinga maandamano ya
chadema hazina msingi ni kutowajibika
kwa jeshi la polisi. Hatukatazi maandamano, polisi wapange ratiba siku
tofauti, sisi tutaandamana kumpinga waziri
ili kama ccm wataandamana kumpongeza
waziri wao wapangiwe siku yao, ila sisi
tulitangaza mapema na barua tulipeleka
kwa mujibu wa sheria za nchi yetu."
mkuu, hope umeelewa. Kutoshiriki maandamano haya ni ubinafsi kwa wadogo zetu, ndugu zetu na elimu ya tanzania kwa ujumla
viva cdm,
tulianza na mungu, tutamaliza na mungu
hoja yako ni nzuri kaka. Ila lazima uelewe kuwa lengo la serikali kuzuia maandamano si kwa sababu ya ujio wa rais wa china bali ni hofu na mfululizo wa ubabe na kutofuata sheria tu.
Rejea matukio ya kupinga maandamano ya chadema kwa kisingizio cha sensa iringa, morogoro eti barabara ni ndogo, maandamano na mkutano wa jj mnyika eti kuna ukarabati wa barabara na kiwanja cha manzeshe ni parking ya magari. Arusha tunaambiwa eti ccm wamepanga maandamano siku hiyo. Rejea maandamano ya wanaharakati kupinga dowans eti kuna tishio la al-shaabab hivyo hairihusiwi mikusanyiko na wakati kipindi hicho kulikuwa na mechi kubwa uwanja wa taifa na mashabiki walihamasishwa kujitokeza kwa wingi.
Rejea maandamano ya madaktari ambapo jeshi la polisi lilidai kuwa hayana tija kwa kuwa serikali imeunda kamati, pia kutakuwa na maandamano ya wananchi kupinga mgomo huo ambao nao watatumia njia hizohizo. Na kama maandamano hayana tija kwa sababu ya xi, mbona wananchi wamehamashishwa na wameandaliwa, tena wamepatiwa na bendera kumpokea xi?.
Nb: Lengo la serikali ya tanzania ni kupinga maandamano ya upinzani kwa sababu zozote zile, na kama tutasubiri kupata kibali za kuandamana kamwe hakitatokea.
naona sasa zamu ya mbowe kunyea debe imewadia. Chezea na polisi wewe. Ngoja aandamane hapo kesho aone nguvu ya vyombo vya dola
naona sasa zamu ya mbowe kunyea debe imewadia. Chezea na polisi wewe. Ngoja aandamane hapo kesho aone nguvu ya vyombo vya dola