Pembe zilizoibwa Tanzania


kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
3,073
Likes
23
Points
135
Age
42
kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
3,073 23 135
OFISA wa Wanyamapori Ufilipino anatuhumiwa kuiba pembe za ndovu zinazosadikiwa kuwa sehemu ya nyara zilizoingizwa nchini humo kwa magendo kutoka Tanzania, ambazo zinaendelea kuhifadhiwa huku Serikali nchini ikiwa katika maandalizi ya huko kufanya uchunguzi.

Taarifa kuhusu wizi huo, zilitolewa jana katika baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa zikitaja kwamba jumla ya kilo 794 za pembe zenye thamani ya dola 80,000 za Marekani zimeibwa katika ghala zilikohifadhiwa.

Shirika la Habari la Ufaransa (AFP) lilimkariri Mkuu wa Idara ya Wanyamapori wa Ufilipino, Josie de Leon, akisema wafanyakazi wenzake na ofisa huyo anayetuhumiwa kuiba pembe za ndovu, walimhisi kutokana na matumizi yake kuwa makubwa.

Taarifa zilisema baada ya wafanyakazi wenzake kuchunguza pembe zilizohifadhiwa ndani ya ghala la serikali, waligundua kwamba kilo 794 zimepungua. Vyombo hivyo vya nje vilikwenda mbali kwa kusema ujumbe wa Tanzania uko mbioni kwenda Manila, wiki ijayo kukagua pembe hizo na kubaini kama ni za Tanzania kwa lengo la kuzirejesha nchini.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Wanyamapori, Tarimo Erasmus, alisema Tanzania ilianza kushughulikia taratibu za kwenda si tu Ufilipino, bali pia Vietnam tangu mwaka jana, kuchunguza pembe hizo.
 
M

Mchili

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2009
Messages
727
Likes
6
Points
35
M

Mchili

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2009
727 6 35
Bongo tutaibiwa sana. Wakati tunalia umaskini uchumi tumeukalia kwa nini wajanja asichulue. Safari za viongozi zinashughulikiwa kwa siku moja lakini kwa sababu hiyo ya kukagua nyara haina maslahi binafsi imekua akishughulikiwa toka mwaka jana!!! Upuuzi mtupu
 

Forum statistics

Threads 1,236,240
Members 475,029
Posts 29,251,215