Pembe za ndovu?

Pembe za ndovu?

Luali

Senior Member
Joined
Jan 1, 2013
Posts
101
Reaction score
11
Mimi najiuliza tu ; hivi hizi pembe za ndovu zinapokamatwa zinapelekwa wapi? Na kama huwa zinauzwa mbona mapato yake hayako wazi kwa wananchi? Na naona kama wakikamata hata tani 1 ndio wanazitumia kulemaza umma kujua serikali inawajibika saaaana kumbe tani kibao hazikamatwi. Wewe una maoni gani?
 
Maoni yangu ni kuwa KUPUNGUA kwa NGUVU za Kiume kunaendana na Ujangili zaidi wa Tembo, Faru na Papa baharini... Muda si mrefu pweza nao wataanza kuadimika! Nawashauri Wanaume wenzangu tuache kula Junk Food na Pombe kupita kiasi...Tufanye mazoezi tupunguze Stress kwa faida ya Tembo, Faru na Viumbe vingine vya baharini...
 
Baada ya kukamatwa,tunatangaziwa,kisha aliyekamatwa anaulizwa "mzigo wa nani?",anamtaja.Kisha anaitwa mwenye mzigo,heee!kumbe bosi kubwa rafiki wa mkuu wa kaya,wanachekacheka pale,anawapoza kidogo,kisha anakabidhiwa mzigo wake,maisha yanaendelea.
 
Subiri wachina wakujibu

Kama wanaongea Kiswahili wanakaribishwa, si unajua nchi yetu haina ubaguzi wa rangi na ni somo halijawaingia watanzania kiasi cha kuwa wabaguzi wa rangi.
 
Baada ya kukamatwa,tunatangaziwa,kisha aliyekamatwa anaulizwa "mzigo wa nani?",anamtaja.Kisha anaitwa mwenye mzigo,heee!kumbe bosi kubwa rafiki wa mkuu wa kaya,wanachekacheka pale,anawapoza kidogo,kisha anakabidhiwa mzigo wake,maisha yanaendelea.

Inawezekana uko right kabisa, ila angalia kucha hizo!
 
Biashara za wakubwa.kesi ya nyani anapelekewa ngedele, unadhani ni ni kitatokea
 
Biashara za wakubwa.kesi ya nyani anapelekewa ngedele, unadhani ni ni kitatokea

Kabisa bro, ila baada ya comment yako usitembee usiku tafadhali, tusije tukakukosa!
 
Back
Top Bottom