Pembe ya faru John yapelekwa kwa Waziri mkuu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
IMG-20161209-WA0081.jpg

Dar es Salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea taarifa inayoelezea utaratibu uliotumika kumhamisha faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Sasakwa Black Rhino Sanctuary iliyoko kwenye Hifadhi ya Grumeti.

Akizungumza katika kikao kilichofanyika nyumbani kwake Oysterbay leo mchana na kuhudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na baadhi ya watendaji wa wizara yake, Waziri Mkuu amesema taarifa hiyo itafanyiwa kazi na wataalamu wa ofisi yake.

“Nilipokea taarifa yenu jana saa 7 usiku lakini nikaahidi kuwa leo tukimaliza sherehe za maadhimisho ya Uhuru tukutane na kujadiliana kuhusu taarifa yenu,” amesema.

Akisoma taarifa hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Profesa Maghembe amesema hadi kufikia Desemba 2015 wakati Faru John anahamishwa alikuwa na watoto 26 (sawa na asilimia 70.2) ya faru wote waliokuwepo ndani ya kreta.

“Uamuzi wa kumuondoa John ulikuwa ni muhimu ili kuwezesha kuongezeka kwa faru weusi na kupunguza tatizo la ‘inbreeding’ ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro,” alisema Waziri Maghembe.

Baada ya kuhamishiwa Sasakwa, Waziri Maghembe alisema Julai 10, 2016 afya ya faru John ilianza kudorora na alikufa tarehe 18 Agosti, mwaka huu. Taarifa hiyo iliandaliwa na Kamati ya Taifa ya kuwalinda tembo na faru. Kamati hiyo inaundwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tawiri, Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa, Mkurugenzi Mkuu wa NCAA na Mhifadhi Mkuu wa Ngorongoro.

Akikabidhi pembe za faru huyo mbele ya Waziri Mkuu, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa Wanyamapori, Robert Mande alimweleza kwamba pembe kubwa ya faru John ilikuwa na uzito wa kilo 3.6 na pembe ndogo ilikuwa na uzito wa kilo 2.3.

Watendaji wa wizara waliohudhuria kikao hicho ni Kaimu Katibu Mkuu, Iddi Mfunda; Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Freddy Manongi; Mkurugenzi Mkuu wa Tawiri, Simon Mduma; Kaimu Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori, Alexander Songorwa na Mkuu wa Pori la Akiba la Ikorongo/Grumeti, Nollasco Ngowe.

Desemba 6, mwaka huu, akiwa ziarani mkoani Arusha, Waziri Mkuu aliuagiza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), umletee nyaraka zote zilizotumika kumhamisha faru maarufu kwa jina la ‘John’ kutoka kwenye hifadhi hiyo ifikapo Alhamisi, Desemba 8.

Alitoa agizo hilo alipotembelea ofisi za makao makuu ya NCAA zilizoko wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha na kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafugaji ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo

Chanzo: Mwananchi
 
Kama huyo faru alikufa kifo cha kawaida kwanini walisubiri mpk kuwe na kutikisana ndio watoe hiyo ripoti........kwanini wasingemjibu tu Waziri Mkuu siku ile ile, na kama akitaka ripoti basi ndio wampatie........Watanzania tulivyo si ajabu hata kusikia hiyo ripoti imepikwa.......mawazo yangu.
 
Waipime kama ni kweli ni ya faru john wasije wakaua faru huko porini ili wapate pembe ya kutudanganyia.....
Watajuaje ni yeye kiongozi kwani wana wana visitors dna vyake hapo ofisini kwa pm ili wafanye comparisons wataomba hao ndiyo walete majibu tena hapo si ndiyo usanii utaendelea
 
Waziri Mkuu Anaishi Dar Siku Hizi ?
DNA Ihusike Kubaini Ikiwa Zinatoka Kwa John Hizo Pembe Ingawa Nchi Hii Ni Wapiga Deals Full Time
 
Waziri Mkuu alisema anajua wa kupelekewa. Hapo sijui ka si yule mfalme fulani mwarabu ili aweze kuwakoromea kisawia wakeze kwa nguvu ya John. Dah! wakware kazi mnayo
 
Kama huyo faru alikufa kifo cha kawaida kwanini walisubiri mpk kuwe na kutikisana ndio watoe hiyo ripoti........kwanini wasingemjibu tu Waziri Mkuu siku ile ile, na kama akitaka ripoti basi ndio wampatie........Watanzania tulivyo si ajabu hata kusikia hiyo ripoti imepikwa.......mawazo yangu.
yule bwana alitaka kujieleza akanyimwa fursa,hivyo hakuweza kueleza ukweli wa kile anachokijua.
 
Hapo inabidi wapime DNA za hizo pembe wakaoanishe na za Faru John,

Huenda za John zilishauzwa halafu mtu akaenda store kuchukua Pembe ya kumzuga Waziri mkuu kwamba ni za John kumbe za John zilishauzwa.
 
Inawezekana wametoa Hizo Pembe Store na kuzileta Kama za Hayati Faru John, Hawa Wanyama wangepewa uwezo wa kuzungumza nasi Wallah tungezimia kwa jinsi wangefunguka namna wanavyofanyiwa!

Inanikumbusha Swaga za aliekuwa Kamanda wa kanda Maalum wa Enzi za 'Nabii Nuhu' alivyokuwa akitoa Mzigo Kwny ghala la Silaha na kutangaza kazimata ili tu auze Nyago lake kwny TV kwny habari !
 
Inasikitisha Sana kuona huko Ngorongoro idadi ya Faru haifiki 40. Nikiwa kama mwanasayansi ninaelewa madhara ya inbreeding kijenetiki lakini ufike wakati sasa tutengeneze sera za kulinda haya mambo na sio wapiga dili wakiahidiwa milioni 200 wanahamisha Faru kwenda kwenye sehemu ambayo inavutia watalii matajiri kama Grumet
 
Back
Top Bottom