Pemba walalamikia kupigwa mabomu ya machozi ktk vijiji ambavyo watu wasiofahamika waliharibu mazao

Pistol

Senior Member
Oct 13, 2015
194
86
Wakazi wa Pemba wamelalamikia Jeshi la Polisi kuvamia maeneo yao na kupiga mabomu ya machozi na kufanya doria usiku wa kuamikia juzi katika mitaa na vijiji mbalimbali kisiwani humo na kuzua hofu miongoni mwao.

Maeneo yaliyokabiliwa na hali hiyo ni pamoja na Mahuduthi, Kengeja, Mgagadu na Kiwani, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba ambako polisi wanadaiwa kupiga mabomu ya machozi zaidi ya 100 na kutumia risasi za mpira kuwatawanya watu.

“Ilikuwa saa 1.30 usiku (wa kuamkia Jumamosi), gari za polisi zilifika kiamboni (kijijini) kwetu zikipiga misere kwa kasi, sote tukawa na hofu, watu walikimbia na kwenda kujificha, wengine waliumia na baadaye wakapiga mabomu mfululizo, sijui waliondoka saa ngapi maana tulijifungia ndani,” alisimulia Zuberi Said (34), mkazi wa Kiwani.

Baadhi ya wakazi wa vijiji hivyo walidai huenda hatua hiyo ya polisi ilitokana na matukio ya kuhujumu mali za viongozi wa Shehia yanayoendelea.

Inadaiwa kuwa watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Ijumaa waliteketeza miti na mashamba yanayomilikiwa na Sabiha Mohamed Ali na Abdalla Makame Hamad, ambao ni mashekha wa Shehia za Kendwa na Kiwani wilayani humo.

Ilidaiwa watu hao pia waliteketeza migomba na mikarafuu mali ya viongozi hao na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.

Mkuu wa Wilaya ya Mkoani, Hemed Suleiman Abdallah aliyefika kujionea uharibifu huo alisema: “Sijui sababu ni nini, ila huenda ni kutokana na siasa chafu zinazoendelea hapa.”

Alilitaka Jeshi la Polisi na askari alioongozana nao katika ziara hiyo kufanya uchunguzi haraka ili kuwabaini na kuwakamata watu waliohusika na vitendo hivyo. “Wala msisubiri baada ya miezi 20 ndipo mkaanza kuchukua hatua,” alisema.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Mkoani Pemba, Mohamed Salim aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya Abdalla, alikiri kuwapo kwa hujuma na kuwatuma askari katika vijiji hivyo kufanya doria.

Chanzo: Mpekuzi
 
Kamanda Mohamed Salim amewatuma vijana wake kufanya doria au ku harrass wananchi?
 
Panapofuka Moshi.... Kalikawe nae aliimba... Ndio Maana huwa nasema Dini zimetungwa hakuna Mungu... Tizama Matendo yao haifanani na Walioitwa Mitume... Dhuruma mwanzo Mwisho...
 
Mimi ndugu Amoxlin ninakuunga mkono sana. Bora waachiwe wawe na nchi yao na serikali yao, na ikifanyika hivyo maendeleo na utulivu yatapatikana haraka. Hawa jamaa wameshachoka kunyanyaswa kwa muda wa zaidi ya miaka mia mbili, na hasa katika utawala wa miaka hii 52 ya watoto wa Nyerere. Idhlali imewasababisha kukuimbilia nchi mbali mbali za ulimwenguni, karibu kila mahala wapo wamegeuka wahindi. Zamani nchi yao ikiwavutia watu wengi kutoka mataifa mbali mbali duniani hasa India, Arabuni, Afrika, malesia, Indonesia, Iran nk. Hakuna mwananchi wa kule alietamani kwenda nchi nyengine kwani ilikuwa ni Pepo ya dunia, ndio maana kukawa na msemo ukisema Pemba peremba ukienda na joho utarudi na kilemba, watu walikuwa na imani ya juu kabisa na wala hakukuwa na shida yoyote kwa maana ya shida. Mali kubwa ilikuwa karafuu tu lakini zao la msimu mmoja pato lake likitumika kwa zaidi ya mwaka mmoja kumbuka karafuu kwa mwaka ina misimu miwili. NASEMA BILA KUMUMUNYA MANENO AFROSHIRAZI CHINI YA DIKTETA KARUME kwa makusudi ndio waloiuwa Pemba bila haya wala tahayuri. Hawa viongozi wa sasa wanaiga tu. Sisi kizazi cha sasa tutapambana na wao kwa siri, kisiasa na mapambano ya ana kwa ana tumechoka kuonewa, kudharauliwa na kudhululumiwa na vilaza. Liwalo na liwe potelea mbali
 
Migomba ya Sheha inasababisha wananchi kupigwa mabomu? hii ni aibu kwa serikali. Serikali inaendelea kuwachonganisha wananchi.
 
Back
Top Bottom