GE2025 Pemba: Vijana wanunuliwa na CCM kwa boflo na maji ya kunywa! Ama kweli ujinga unatutesa sana!

GE2025 Pemba: Vijana wanunuliwa na CCM kwa boflo na maji ya kunywa! Ama kweli ujinga unatutesa sana!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Tanzania tuna safari ndefu ya kwenda mpaka kufikia ukombozi kamili. Sasa hivi nimeanza kuelewa kwanini Mwalimu Julius Nyerere alikuwa anapambana sana Watanzania tuondokane na ujinga.

Ona leo hii kinachoendelea, kijana wa Kitanzania mwenye akili timamu ananunuliwa kwa boflo tano na maji na kukiri kabisa kwa kupatiwa vitu hivyo basi kiongozi anastahili kuendelea kutawala tena!

Hii inanipa picha kwamba Watanzania asilimia kubwa bado tunateseka na ujinga, hatujui haki zetu, hatujui nguvu yetu kwa viongozi wetu kama Watanzania, na wala hatuna uelewa wowote kuhusu utawala.

Jaribu kufikiria kwa akili za vijana kama hawa, hivi kweli wataelewa ukiwaambia kuhusu, DP World? wataelewa ukiwaambia kuhusu utakatishaji wa mabilioni ya mapesa unaoendelea nchini?

Utakuja kujua kuwa kiwango cha kufikiria kipo chini sana.

Akipata maarifa, Mjinga si mjinga tena.

Kama kweli haya ni mapokezi halali ya Samia Simiyu CCM inaogopa nini kuicha Tume ya uchaguzi kuwa huru?

 
Hiyo ndiyo furaha ya watawala. Kuona wananchi wanabakia kuwa wajinga milele.
 
Tanzania tunasafari ndefu ya kwenda mpaka kufikia ukombozi kamili. Sasa hivi nimeanza kuelewa kwanini Mwalimu julius Nyerere alikuwa anapambana sana watanzania tuondokane na ujinga.

Ona leo hii kinachoendelea, kijana wa kitanzania mwenye akili timamu amekamilika ananunuliwa kwa boflo tano na maji na kukiri kabisa kwa kupatiwa vitu hivyo basi kiongozi anastahili kuendelea kutawala tena. Hii inanipa picha kwamba watanzania asilimia kubwa bado tunateseka na ujinga, hatujui haki zetu, hatujui nguvu yetu kwa viongozi wetu kama watanzania, na wala hatuna uelewa wowote kuhusu utawala.

Jaribu kufikiria kwa akili za vijana kama hawa, hivi kweli wataelewa ukiwaambia kuhusu, DP world? wataelewa ukiwaambia kuhusu utakatishaji wa mabilioni ya mapesa unaoendelea nchini?

Utakuja kujua kuwa kiwango cha kufikiria kipo chini sana.

Akipata maarifa, Mjinga si mjinga tena.

Kama kweli haya ni mapokezi halali ya Samia Simiyu CCM inaogopa nini kuicha Tume ya uchaguzi kuwa huru?

View attachment 3477718
Ukombozi wa kwanza Tanzania unatakiwa ukombozi wa fikra kwanza!!!
 
vijana wa hamasa hao,, hizi nguvu zingetumika kuboresha hiin nchi tungekua untouchable hapa africa
 
Tatizo mnategemea mimea ya kijani siku zote katika maisha yenu kujipatia chakula, ndio maana mnashindwa kuitoa ccm madarakani.
 
Kwahio na Mkate na maji asichukue ?; Au Maji na Mkate achukue na Bado akiona alternative aichukue ?

Ni kwamba bado mtanzania hajafika point of no return na bado ana hope ; na until that day watakapoona kabisa usiku na mchana baina ya Mwanasiasa A na B ndio pale watawabadilisha kwa hasira na nguvu zote (sababu at the moment ni ngumu kuwatofautisha i.e. makasongo ni wengi)

By the way unadhani ni marangapi The President that Never was "Maalim Seif" alishinda Zanzibar na CUF yake ?!!!!
 
Back
Top Bottom