Pemba kunani?

Quinton Canosa

JF-Expert Member
Nov 2, 2012
1,211
1,185
Habari wakuu,

Ni muda sasa ninajiuliza kuhusu kisiwa cha Pemba, kwa muda nimekuwa nikifuatilia jitihada za serikali kuhusu kisiwa hiki, maana sijawahi kusikia hata jitihada zozote za serikali kuhusu kisiwa hiki. Hata sherehe nyingi za kiserikali sijawahi kuzisikia kwenye kisiwa hiki, ninaomba kujua nini kimefanya kisiwa hiki kijitenge sana wakati ni sehemu muhimu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

AU HUENDA KISIWA HIKI HAKINA SHUGHULI YOYOTE YA KIUCHUMI INAYOCHANGIA PATO LA TAIFA?

Wapemba wanasemaje kuhusu hili? Je,wana uhusiano mzuri na kisiwa cha Unguja? Je, kuwepo kwa nguvu ya chama cha CUF hapo Pemba kunakifanya kisiwa hiki kisiwe na maelewano mazuri na serikali kuu au nini kimekifanya kisiwa hiki kionekane kama kimejitenga?

NIELEWEKE MIMI SIO MWANACHAMA WA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA ILA NI MDAU WA MAENDELEO YA NCHI YANGU.

Nawasilisha
 
Quinton Canosa,

Shughuli zipi za kiserikali unazozitaka zifanyike?

Vipi miundo mbinu haijengwi huko?

Vipi hakuna vikao vya ndani vya kiserikali huko?

Vipi chaguzi hazifanyiki huko?

Unataka shughuli gani ?
 
shughuli zipi za kiserikali unazozitaka zifanyike?
Vipi miundo mbinu haijengwi huko?
Vipi hakuna vikao vya ndani vya kiserikali huko?
Vipi chaguzi hazifanyiki huko ?
Unataka shughuli gani ?
Nipe majibu ya haya maswali yako sasa ndio nayataka.
 
Kama watakuwa hawapelekewi maendeleo itakuwa ni uonevu na ubaguzi wa hali ya juu.
Wahusika wanatakiwa wapaze sauti,wasikike.
 
Huko CCM si ndiyo ipo madarakani kwa sasa baada ya CUF kukataa ile dhuruma waliyofanyiwa kipindi cha Uchaguzi Mkuu.
Sasa zile Ngonjera za CCM kupeleka maendeleo ziko wapi..?
 
Maendeleo yapo na vikao vipo.. .
Pemba ya zamani ni tofauti na sasa!
Tuwe wakweli ... na mjenga nchi ni mwananchi pia..

Wanaakili wachaga wao wapo dar ila kwao wanajenga... na mzunguko wa pesa upo!
Wapemba wengi wanaishi na kujenga nje ya pemba! na ndio vyema..maisha ni kutafuta..sio kelele na unafiki!
 
Pemba yote ni CUF, na pemba haijawahi kutoa rais tangu mapinduzi mpaka juzi ndio ametoka SHEIN huko, maana wote walikuwa waunguja, lakini wana bahati mbaya maana Shein ana chembe chembe za Mkapa, hajali kwao kabisa.
 
Back
Top Bottom