Pemba kila kitu kinyumenyume! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pemba kila kitu kinyumenyume!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngekewa, Sep 7, 2009.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  CCM yapoteza imani na polisi kisiwani Pemba[​IMG]
  Salma Said, Zanzibar

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa hakina imani na askari wa Jeshi la Polisi Kisiwani Pemba kikidai kuwa idadi kubwa ya watumishi hao wa chombo cha dola wamejiingiza katika siasa kwa kushabikia CUF, kitu ambacho kinawafanya washindwe kuwajibika kikamilifu kwa umma.

  Tuhuma hizi zimetolewa na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), Zainab Khamis Shomari alipokuwa akizungumza ofisini kwake Kisiwani hapa jana. Alisema polisi wengi wamejawa na itikadi za kisiasa ndani ya mioyo yao hivyo inakuwa vigumu sana kufaya kazi kwa haki.

  Mjumbe huyo wa Nec kutoka mkoa wa Kusini Pemba na ambaye pia ni katibu wa CCM wilayani Chake Chake alisema kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakifanya kazi kwa misingi ya itikadi za kisiasa.

  "Hakuna siri tena ni jambo ambalo kila aliye Pemba analijua; polisi wamekuwa mashabiki wakubwa wa CUF na ndio maana utendaji wa kazi zao unakuwa mgumu kwa kuwa wanaingiza ushabiki wa kisiasa katika kazi," alisema mjumbe huyo.

  Katibu huyo alisema kwamba ni jambo la kusononesha kuona watumishi wa polisi wametingwa na siasa huku wakitelekeza majukumu ambayo kimsingi hawapaswi kujiingiza katika masuala hayo na kumtaka Mkuu wa Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema kuichukulia hali hiyo kwa umakini wa hali ya juu.

  "Wananchi wa Pemba imani yao imebakia kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ)... sio tena kwa polisi. Huwezi kuwategemea askari ambao ni manazi wa siasa katika hali kama ya Pemba," alisema Zainab ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar katika kipindi cha mwaka 2000 hadi 2005.

  Mjumbe huyo wa Nec alishauri serikali kufanya kila iwezalo kutafutia ufumbuzi tatizo hilo ikiwa pamoja na kuwahamisha askari ambao wanajishughulisha na siasa kwenda mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara , ili kupunguza na kuondoa kabisa ubovu wa polisi wasiofuata maadili ya kazi zao.

  Shomari alitoa mfano wa wakati wa zoezi la uandikishaji wapigakura katika daftari la kudumu katika mkoa wa Kaskazini Pemba ambako polisi waliokuwa kazini walishindwa kuwaondoa wafuasi wa CUF, waliokuwa wakijikusanya katika baadhi ya vituo vya uandikishaji licha ya sheria kueleza kwamba, hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia au kukaa ndani ya mita 200 ikiwa hausiki na uandikishaji.

  "Sheria iko wazi... inasema kwamba hakuna mtu atakayeruhusiwa kukaa ndani ya mita 200 katika kituo cha uandikishaji, lakini tumeshuhudia watu wakiwa ndani ya mita tano hadi kumi lakini polisi wanawatazama na unapowaendea kuwaeleza wanasema wao hawana vya kuwafanya," alilalamika Zainab.

  Alisema kwamba katika tukio lililotokea hivi karibuni wafuasi wa CUF walijikusanya kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Chake Chake kwa nia ya kushinikiza kusajiliwa, kupatiwa vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi na ilibidi askari wa JWTZ kuwatawanya wafuasi hao. "Ni mara ngapi JWTZ itasaidia wakati ina majukumu mazito ya kulinda mipaka ya nchi na kazi nyinginezo. Jeshi la Polisi ndilo lenye majukumu hasa ya kulinda usalama wa raia na mali zao... nafikiri ipo haja kwa IGP (Said Mwema) kulipanga upya katika uwajibikaji hasa kisiwani Pemba," alisema kada huyo wa CCM.  Wacha huyu Bibi ashangae kwani amezoelea kuona kuwa Polisi kushabikia CCM tu. Hata hivyo namuomba Junius na Mwiba watupe ukweli wa hili, limewezekanaje?
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kama alivyoshauri, Bi Shomari ni kuwahamisha mara moja, na waletwe polisi waliohusu Musoma hapo PBA
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ukweli ni kuwa polisi wanapoamua kuachana na siasa basi hapo CCM wanajikuta wakiwekwa kwenye kona za ulingo wa siasa ,kama mtakumbuka huyu msemaje wa CCM amesahau wakati ule polisi walipokimbia na masanduku ya kura na kwenda nayo kusikojulikana wakaibuka na kusema kuwa CCM ni kidedea ?

  Ila kwa hilo alisemalo leo kuwa polisi ni washabiki wa CUF hilo halina mjadala hata wale wanamamluki wanaopelekwa Pemba na Unguja nao pia ni washabiki wa CUF ,hata ndani ya CCM pia kuna washabiki wa CUF ,yaani ndani ya uongozi mkuu wa serikali ya CCM kuna mashabiki damdam wa CUF ,hili jana jike halifahamu kuwa hata polisi na majeshi wengine wanafikwa na shida za kimaisha zinazosababishwa na serikali mbovu ya CCM ,sasa hapo unategemea waiunge mkono CCM mpaka kiama ?

  Nionavyo hao polisi na majeshi kama kuibeba CCM wameshaibeba sana na kwa sasa wanaonekana kuchoka ,vile vile litakapopasuka bomu la kushitakiwa UN basi wakuu wa vyombo hivyo nao hapo wanapaogopa kwa sasa ,kwani Raisi anaweza kuruka ,Katibu Mkuu wa CCM anaweza kuruka wakabakia wakuu wa vyombo hivyo ambao itabidi wakuu wa CCM wawagandamize kuwa walitumia nguvu kinyume na maelezo waliyopewa.

  Halafu kuzidiwa kubaya unaweza ukamlaumu refa kuwa anapendelea kumbe ukweli mmezidiwa na ndivyo hali inavyoelekea kuwa kila siku zinavyozidi kusogelea uchaguzi mkuu CCM wanajiona wanaelemewa kila kona ya Tanzania ,na hizo za kuwavamia mapolisi na majeshi ni dalili tosha kuwa sasa ngoma wanaachiwa waicheze kama inavyopigwa kila mtu anajiogopea kupandishwa UN.
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  wizi mtupu
   
Loading...