Abu Ubaidah Commando
JF-Expert Member
- Sep 8, 2016
- 7,591
- 6,946
PELE aibuka tena na kumchana PAULO DYBALA.
June 10, 2017
Siku za karibuni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Juventus PAULO DYBALA amekuwa gumzo sana kutokana na uwezo wake, Dyabala kuna kipindi alionekana kama tegemezi kubwa la Waargentina wengi wakimuona dogo huyo kuchukua nafasi ya Mfalme LEONEL MESSI.
PAULO DYBALA amekuwa bora sana haswa na timu ya Juventus kiasi cha kuvivutia vilabu vikubwa duniani na wachambuzi wengi wa soka wamekuwa wakisema PAULO DYBALA anafanana kiuchezaji na gwiji wa zamani kuwahi kutokea na timu ya taifa ya Argentina DIEGO ARMANDO MARADONA.
Mwanasoka bora wa zamani ambaye alikuwa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil PELE ameibuka na kumkandia vikali PAULO DYABALA na kusisitiza kwamba DYABALA bado sana kufikia kiwango anachotajwa kuwa nacho.
PELE amesema DYABALA sio lolote “kwanza sio bora kama watu wanavyomzungumzia lakini pia nashangaa wanaomfananisha na DIEGO MARADONA wakati hawafanani hata kidogo na kitu pekee wanachofanana ni kutumia mguu wa kushoto kucheza mpira” alisema Pele.
Katika misimu miwili ya ligi kuu nchini Italia PAULO DYABALA mwenye umri wa miaka 23 ameifungia Juventus jumla ya mabao 30 na akiisaidia kubeba kombe la Serie A lakini alikuwepo uwanjani wakati wa fainali ya Champions League ambapo Juventus walikubali kipigo cha mabao 4 kwa 1 toka kwa Real Madrid.
Tukumbuke kuwa huyu huyu mzee alishawahi kumkandia hata MESSI. Kwahiyo ni jinsi gani anavyowachukia professional players wa Argentina na kuwasifia wabrazili wenzie. Anajiaibisha huyu kwa kweli.ni heri akae kimya