Peformance appraisal, Rais Samia amepata 100

Peformance appraisal, Rais Samia amepata 100

AUGUSTINO CHIWINGA

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2017
Posts
220
Reaction score
689
Kipimo cha uwezo wa sehemu ya kazi hupimwa kwa kitu kinachoitwa Perfomance appraisal. Tangu ashike madaraka Rais wa Tanzania wa awamu ya sita ni wazi amescore credit zote 100.

Mosi kuweza kumaintain uendelezwaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kama vile SGR na Bwawa la Nyerere huku makusanyo ya kodi yakipaa mpaka kufikia Trilioni 5 ni uwezo mkubwa sana alionao.Trilioni Tanio hizo ndizo zinaletwa huku vijijijni na mitaani kuja kutatua changamoto mbalimbali za wananchi.

Uwezo mwingine mkubwa alionesha ni ule wa kumwaga ajira kwenye sekta mbalimbali za umma kama vile polisi, ,magereza na zimamoto. Sasa kile kilio cha ukosefu wa ajira Rais Samiah amekipatia mwarobaini wake. Jambo hili linaenda sambamba na uimarishaji wa sekta binafsi ambapo ndani ya miezi mitano tu jumla ya biashara zenye thamani ya Bilion 3 zimeweza kusajili jambo ambalo limeongeza ajira kwa vijana wengi.

Achilia mbali miradi mingi midogomidogo na ya kati inayoendelea kote nchini kama vile barabara za majimbo ambazo kupitia TARURA zimeingizwa shillingi milioni 500 mpaka Bilioni moja kote nchini.Nchi inanawiri na kustawi maendeleo yanazidi kupatikana tena kwa kasi kubwa bila ya kusahau bei nzuri za mazao yao waliyoyapata wakulima mwaka huu.

Rais wetu ni mchapakazi hodari makini mwenye huruma mpole lakini mkali kwenye mambo ya hovyo . Watanzania wana imani nae, mama atatuvusha.
 
Mwambie wasiojulikana wamenza kuteka tena watu.

Pia mwanamke kuwa dikteta haipendezi.
 
Kipimo cha uwezo wa sehemu ya kazi hupimwa kwa kitu kinachoitwa Perfomance appraisal. Tangu ashike madaraka Rais wa Tanzania wa awamu ya sita ni wazi amescore credit zote 100.

146E0E38-DB6A-4508-93CA-D50AAF3A3AA4.jpeg


C02E4B83-C62A-45E7-B2E2-0A287083EA58.jpeg


DED178E4-AE95-4A9F-BD03-B74D319F38B3.jpeg


974B8485-F29C-4B0F-B04C-5E8DD1460F01.jpeg
 
Performance appraisal haihubiliwi kwa nguvu namna hii kama wokovu.

If its there; people will just know it.
 
Kipimo cha uwezo wa sehemu ya kazi hupimwa kwa kitu kinachoitwa Perfomance appraisal. Tangu ashike madaraka Rais wa Tanzania wa awamu ya sita ni wazi amescore credit zote 100...
Sijui umetumia kigezo gani kupima iyo OPRAS ya Hangaya??
 
Tunakwenda na Hangaya hata mlete upotoshaji wa ajabu tumeishaona mwanga sasa.
 
Mama anaendelea kuupiga mwingi sana

Hongera Mama yetu kipenzi Mh.SSH...

Hizi ndo critical issues zikuinue..utendaji unaonekana...
Issue za gender achana nazo..
 
Back
Top Bottom