Pebble: Saa Ya Kimtindo Kwa Wanateknolojia

ManiTek TV

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
410
159
19/03/2013


Teknolojia inaelekea kwenye gajeti za kuvaa, miongoni mwa gajeti hizo Saa ya Pebble ni saa ya kimtindo. Ni saa inalenga wana-teknolojia kama watumiaji wake. Saa hii sio tu itawafurahisha watumiaji hao bali inatabiriwa kubadili namna saa zilivyo ulimwenguni na kuongeza matumizi mengi kwenye saa. Wakati wengi wameacha kuvaa saa kwa sababu ya gajeti kama simu, Pebble itawafanya wengi wavae saa kwa sababu ya simu.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba Pebble haikamiliki bila ya kuwa na simu ya Android au iPhone. Pebble ni saa yenye skrini aina ya e-paper, skrini sawa na zile zinzotumika kwenye gajeti za kusomea vitabu (E Book Readers), Saa hii ni saa inayotarajiwa kuwa na matumizi mengi kuliko saa yoyote Duniani kwa sasa. Hii ni kwa sababu Pebble itatumia Apps za kushirikiana na simu.

Saa ya Pebble inawasiliana na simu ya mtumiaji kwa teknolojia ya bluetooth, humuwezesha mtumiaji kutambua anapopigiwa simu hata kama simu imezimwa sauti, kwa vile Pebble ina vibrate na kuonyesha namba ya mpigaji, hivyo kama simu iko mfukoni au mbali kidogo na mtumiaji, mtumiaji ataweza kumtambua mpigaji kabla ya kuifikia simu yenyewe.

Kwa mtindo huu huu, Pebble itamuwezesha mtumiaji kupata aina nyingi za ujumbe zinazoingia kwenye simu moja kwa moja kwenye saa hiyo, ujumbe kama vile wa SMS, iMessage, Twitter, ukumbusho wa kalenda (calendar alert), hali ya hewa, na hata ujumbe wa facebook.
Kivutio kikubwa zaidi cha saa hii ni kwamba watengenezaji wa Pebble wameshatoa SDK itakayowawezesha maprograma kutengeneza apps zaidi za saa hizi, tayari kuna apps nyingi ambazo unaweza ku-install kutoka kwenye simu yako ya Android au iPhone. Pia saa hii inaweza kutumiaka kama pedomita kwa ajili ya mazoezi katika michezo mbali mbali inayokuwezesha kushiriki ukiwa na simu yako mfukoni.

Saa hii ilikuwepo kwenye maonyesho ya CES mwaka huu mwezi uliopita, watengenezaji waliomba wawekezaji wachangie saa hiyo ili kuweza kuileta madukani, watengenezaji wa Pebble walitangaza kwamba wanahitaji dola laki moja kuanza uzalishaji, mafanikio makubwa yamepatikana kwani kwa mujibu wa mtandao wa Pebble wawekezaji wamewekaza jumla ya dola za Kimareani milioni Kumi. Hii inadhihirisha kiasi gani saa hii ni kivutio kikubwa kwa sasa.

Vile vile watumiaji wataweza kubadili muonekano wa skrini ya saa hiyo kwa ku-install aina mbali mbali za muonekano wa saa kutoka kwenye simu. Kwa mujibu wa mtandao rasmi wa Pebble tayari unaweza kutoa oda ya Saa ya Pebble na wateja watarajiwa wategemee kuzipata saa zao kuanzia mwezi nne na wa tano. Mtandao wa Pebble unaonyesha tayari kuna oda 85,000.

Chanzo: http://www.gajetek.com/2013/03/pebble-saa-ya-kimtindo-kwa.html
 
Kwa mujibu wa taarifa zilizoko kwenye iOS App "Is Pebble Shipping" Saa hizi zimeshaanza kuuzwa"
photo.JPG
 
Back
Top Bottom