PCCB ushahidi wowote wanatakiwa kuupeleka mahakamani na si bungeni.Chochote wanachokusanya ni tuhuma tu zinazotakiwa kuthibitishwa na mahakama tu.Hata kama ilikusanya ushahidi wa nani kapewa au la wao hawana mandate ya kusema ni huyu na huyu ni mahakama pekee iwezayo tamka hivyo.
PCCB nadhani si chombo cha kisiasa na ijitahidi kubakia hivyo.
PCCB sio kikosi cha umbeya ambapo wakipata kitu wanaenda kubwabwaja mitaani au bungeni!!!!
mkuu mbona kama umechukizwa hivi na report ya pccb,hayo waliyofanya ni maelekezo ya bunge sasa hasira za nini.Ni mfumo wa nchi hii ndo mbovu ila wangeshawapeleka mahakamani saa nyingi