PayPal Tanzania

PayPal Tanzania

The introvert

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2023
Posts
1,118
Reaction score
2,230
Wakuu habari za muda huu.

Ni mwaka 2025, dunia inakimbia kwa kasi kwenye suala la teknolojia, lakini sisi bado tumekwama kwenye jambo dogo la huduma ya kifedha ya mtandaoni kama PayPal.

Watanzania — hasa vijana wa kidigitali, wabunifu, wasanii, freelancers, na wafanyabiashara mtandaoni — wamefungiwa milango ya kupata kipato halali kutoka nje kwa sababu tu huduma hii muhimu kuwa haipatikani nchini.

Cha na kushangaza na kusikitisha zaidi, serikali ipo kimya, hakuna juhudi za wazi wala majadiliano yanayofanyika hata na Wizara husika ni kama imelifumbia macho hili jambo.

Na hata katika kipindi hiki cha sera na kampeni za uchaguzi mkuu, hakuna mgombea yeyote anayeonesha kuipa kipaumbele hoja hii muhimu ya uchumi wa kidigitali kwa ajili ya vijana wa Tanzania.

Ukweli ni kwamba, kutokuwepo kwa PayPal Tanzania kunaua fursa za vijana.

Wakati wenzetu wanauza sanaa, huduma, na ubunifu wao duniani kupitia mitandao, sisi tunabaki kuwa watazamaji.Mfano halisi nenda katizame Kenya 🇰🇪 tu hapo kwa jirani.

Ni wakati wa viongozi kuamka na kuangalia dunia inavyokwenda.

Wizara husika naomba mtupambanie vijana katika hili
 
Hivi walikua wanashindwana wapi? Serikali inataka nini na paypal wanataka nini?
Yani ni kwamba PayPal ni B2B hakuna udalali wa 10%, Sasa hichi kitu kinawakera sana viongozi wenu wa CCM, kwamba wanaruhusuje Biashara bila wao kupata chochote kitu.

Yan siku mkigundua viongozi wenu wa CCM ni watu wa aina Gani, mtalia sana
 
Hapo ndipo unabyopata picha ni jinsi gani Viongozi wetu hawapo tayari kutumikia wananchi wao wanawaza upigaji tu
 
Sisiemu haiwezi kuruhusu paypal kiongozi! Inajua kbs ndio kifo chake, umaskini ni kete kubwa kwao kuruhusu hao unaowaita freelancers wapate pesa bila masisiemu kujua details na chawa wake haipo tayari na money laundering pia ni biashara kubwa sana kwa makada, njia zote halali zinawaexpose pakubwa so sio leo wala kesho hii kitu itakuja
 
Duh
 
Back
Top Bottom