Paul Makonda: The untouchable one, the chosen one

Paul Makonda: The untouchable one, the chosen one

Kitendo cha makonda cha kuwachafua vijana wenzake kitakuja kumtokea puani, ni suala la muda tu, sasa hivi anaishi kwa hofu kama digidigi
Mwacheni kipenzi cha Baba ukitaka mambo yako yanyooke kuwa karibu naye, ukimgusa utaondoka wewe. anachokitaka kokote anapewa hata akitaka wake za watu atapewa ukogoma utakiona cha stemakuni utakuwa tu unahusika na dawa za kulevya!!!!!
 
Wakati tunamchaguwa Rais tulitegemea aongoze kwa usawa. tulimuchaguwa Rais atuongoze lakini pia atusikilize kwa kuwa Tanzania ni yetu wote. Hatukumuuzia nchi, nchi ni yetu wote, ni ya Watanzania wote, asituondolea haki zetu kwaajili ya kumpendelea mtu mmoja. Sheria ya vyeti basi iwe kwa wote, wanafunzi wamefukuzwa mashuleni, kwa vyeti feki, wafanyakazi wamefukuzwa kazi kwaajili ya vyeti, Watanzania tulisifu na kuona sawa kabisa, lakini alipoanza kuchaguwa na kumkingia kifua Mkuu wa mkowa, mwenye kuaminika ametumia vyeti feki, mwenye kuvunja sheria kuwa harass Watanzania wenzake kwa kutumia cheo chake, na mabunduki ya umma. Mkuu mwenye mali ambazo hawezi kuelezea kazipataje, na bado Rais kumtetea na kumfukuza kazi Waziri anayepigania haki, hii imewaumiza wengi sana.

Nikiwa mmojawapo aliyekuwa na matumaini makubwa na serikali ya Rais Magufuli si mimi tu ni wengi, Sasa tuna mashaka makubwa na serikali, masikitika haitaleta mabadiliko yoyote. Watanzania Tabu zetu zinaendelea vile vile kama zamani. Nampongeza WazirinNape kwa kutetea haki, cheo ni dhamana, waliokuwa madarakani Leo kesho watanyatuka, na historia yao itawajaji. Unyonge wa Watanzania wa kuongozwa kama ng'ombe na ukimya tulionao hautusaidii. Ndiyo maana according to UN Watanzania ni watu wenye majonzi makubwa duniani ingawaje nchi yetu ina utulivu, lakini utulivu na ukimya huu unatuuwa pole pole kama cancer kwa ajili ya utawala mbovu.
point
 
Taratibu na sheria zipi?

Tanzania tumekuwa wanafiki sana kwa kujifanya tunajua sana "taratibu na sheria" wakati nchi inazidi kudidimia wakati hizo sheria zipo.

Sasa ni bora zaidi Magufuli aiendeshe nchi kwa utashi wake kuliko hizo sheria za kipuuzi mnazosema.

Tulitamani sana tupate Rais mwenye msimamo mkali kama huyu na tumempata. Wenye akili zetu, tunafurahia sababu dua yetu imesikiwa.

Chapa kazi Rais Magufuli, chapa kazi Rc Makonda. Watanzania tupo pamoja na nyie.
sema ww upo pamoja nao..usitusemee
 
Wenye matatizo ya akili ni wale wanaompinga Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya kwa taifa hili.

Wenye matatizo ya akili ni wale wanaompinga Paul Makonda kwa kazi nzuri anayoifanya ya kupambana na wauza madawa ya kulevya.

Inawezekana na wewe ni mmoja wao.
wewe nawe ulizungusha bla shaka. makonda anapambana na wauza unga??!!!! my foot....alienda clouds kufanaje?
 
Acha mawazo mgando na akili tegemezi wewe!

Kama Watanzania wana mawazo kama yako, basi mbona kazi bado ipo!


Unataka Rais Magufuli akuletee chakula nyumbani kwako?

Rais Magufuli amefanya mambo mengi sana ambayo watangulizi wake hata robo tu hawakufikia.

Maisha utayaona magumu sana kipindi hichi sababu kama ulitegemea kupata kipato kwa kupiga dili basi andika maumivu. Sasa hivi "dili" hakuna tena. Tafuta kazi ya kufanya ya kukuingizia kipato halali na usitegemee Rais atakuletea "mchicha na unga wa mahindi" nyumbani kwako.
yataje?
 
Hahaha hahaha sijawahi kutishwa sitishikagi..tena usinipangie...hyo ndio hali halisi badala mumsaidie apone mnanitisha...mpeni huduma upesi...wewe si unatuma ujumbe kwa wahusika...kabla ujumbe haujashughulikikwa mie ntakuwa nshakushughurikia...
wewe unazan watu wanaish manzese kama wewe?.
 
Taratibu na sheria zipi?

Tanzania tumekuwa wanafiki sana kwa kujifanya tunajua sana "taratibu na sheria" wakati nchi inazidi kudidimia wakati hizo sheria zipo.

Sasa ni bora zaidi Magufuli aiendeshe nchi kwa utashi wake kuliko hizo sheria za kipuuzi mnazosema.

Tulitamani sana tupate Rais mwenye msimamo mkali kama huyu na tumempata. Wenye akili zetu, tunafurahia sababu dua yetu imesikiwa.

Chapa kazi Rais Magufuli, chapa kazi Rc Makonda. Watanzania tupo pamoja na nyie.
Wenye laana mpo wengi mkuu
 
achane mambo yaende kila siku yatupasa kuangalia faida na hasara kuna faida nyingi sana makonda kuendelea na kazia yake ova kuliko hasara nadhani hata wewe bila chuki unalikubali hili .
 
Ungesema wasiwe wasaliti pia kwa maslahi yao binafsi

Clouds watajipanga upya, yataisha.

Magufuli oyeeeee

Makonda oyeeee
siku akitoa roho za watu na hasa ndugu yako uje useme hivyo hivyo oyee, manake ndio tunakoelekea, wamefanya hivyo wameona hamna reaction sasa watamresitisha mtu in peace, na msisifie kuwa marehemu alikuwa hodari na mtiifu, noo, imbeni wimbo wenu wa oyeee
 
siku akitoa roho za watu na hasa ndugu yako uje useme hivyo hivyo oyee, manake ndio tunakoelekea, wamefanya hivyo wameona hamna reaction sasa watamresitisha mtu in peace, na msisifie kuwa marehemu alikuwa hodari na mtiifu, noo, imbeni wimbo wenu wa oyeee
acha uoga wewe lazima nidhanu iwepo nchini
 
siku akitoa roho za watu na hasa ndugu yako uje useme hivyo hivyo oyee, manake ndio tunakoelekea, wamefanya hivyo wameona hamna reaction sasa watamresitisha mtu in peace, na msisifie kuwa marehemu alikuwa hodari na mtiifu, noo, imbeni wimbo wenu wa oyeee

Acha kukuza mambo na kuandika upupwu, eti kututoa roho kwani wanakuwekea chakula mezani au inabidi wewe ujiwekee ule!?

Clouds watazidi kupaa na yao sababu wako vizuri tangu.

Hapa kazi tu

Makonda oyeeeee
 
Acha kukuza mambo na kuandika upupwu, eti kututoa roho kwani wanakuwekea chakula mezani au inabidi wewe ujiwekee ule!?

Clouds watazidi kupaa na yao sababu wako vizuri tangu.

Hapa kazi tu

Makonda oyeeeee

Hayo ndiyo mawazo ya mtu ambaye hana akili, unachofikilia wewe ni chakula tu, elimu yetu imetufanya tumekuwa wajinga sana, tunakubali kuona mtu kuonewa as long sio sisi tunaonewa. Sio wewe peke yako hata Baraza la mawaziri liko kimya ugonjwa unaoitwa woga lakini wanasononeka miyoni mwao , kimya kama watoto ama mtu anayelishwa as per your statement. Kwakuwa anayeonewa ni mwingine basi haituhusu. Anayeonewa ni mtu kama wewe, Mtanzania mwanga nchi, Hakuna mtu yeyote ana haki ya kumtishia maisha. Leo kafanyiwa jirani yako kesho wewe ama jamaa yako. Lazima tujenge Tanzania ya watu wote sio Tanzania ya kutawaliwa kama ng'ombe. Picha yako, kama ni yako kweli, unaonekana wewe nimmrembo sana, lakini nasikitika kukuambia ya kuwa kichwa chako kimejaa maji badala ya akili. Watu kama nyinyi wenyekufungia macho haki kwakuwa aliyotendewa mabaya sio wewe basi haikuhusu, na watu kama nyinyi ndiyo wengi, ndiyo maana tuna hali hii tunayo. Hakuna mtu ananilisha, najilisha mwenyewe, na ninachukia uonezi wa aina yeyeote ile, hata adui yangu akionewa nitamtetea. KAZI TU, kazi ikifanywa kwa woga na wasi wasi wakufuzwa kazi iwapo ukisemwa ukweli, hii sio kazi bali ni utumwa.
 
Rais Magufuli amethibisha kuwa yeye ni mtu makini, mwenye msimamo usioyumba, huyu ni Amiri jeshi mkuu hasa, mwenye maamuzi magumu, Rais asiyeangalia sura ya mtu wala ukubwa wa jina la mtu, wala cheo chake, wala historia yake.

Ukiingia kwenye kumi na nane zake, hakuachi, anakumaliza. Watoto wa mjini wanasema; anakuchinjia baharini!

Wengi waliokwenda kinyume na matakwa ya Rais Magufuli wameishia kutumbuliwa bila kujali majina yao wala historia ya familia zao. Mkumbuke Anne Kilango Malecela, Kitwanga na leo ilikuwa zamu ya Nape Nnauye, kama utani vile, ametumbuliwa kwa kwenda kinyume na matakwa ya Boss wake.

Kosa kubwa la Nape ni kujiingiza kwenye vita isiyomuhusu na kuanza kuropoka. Nape hakujua kama Makonda ni “The Untouchable one”, hata siku moja huwezi kusema na kuropoka kuwa “The Untouchable” ameinajisi wizara yako! Hili ni kosa kubwa sana.

Mtu mmoja aliwahi kusema; if you can’t fight them, join them. Licha ya kuwa Nape ni mtoto wa mjini, lakini hakulitambua hili. Sasa amebakiwa na kiti chake cha ubunge tu.

Ushauri wangu kwa Nape, achunge sana mdomo wake; sababu this WAR is not over yet. This is just the beginning of another Episode! Mtoto wa Kimakonde, haya ni maji mazito sana kwako! Ukiendelea kubwabwaja, unaweza kupoteza sifa ya kuteuliwa na chama chako kugombea ubunge ikifika 2020. Kumbuka kuwa mwenyekiti wa chama ni huyu huyu nahodha asiyeangalia sura, John Pombe Magufuli!

Baada ya Nape, sasa wamebakia akina Gwajima na CLOUDS MEDIA. Hawa hakuna namna watachomoka mbele ya Mkuu! Hivi sasa wanachukuliwa “timing” tu. Mkuu ni kama “Sterling” kwenye hii movie na siku zote “Sterling hauwawi” lazima atashinda tu.

Kwa mbali nawaona CLOUDS wakifutika kwenye ramani ya Tanzania. CLOUDS wametumbukia kwenye vita wasiyoweza kushinda. Nahodha wa meli aliwapenda sana hapo mwanzo, lakini walipomchafua “The Untouchable One” hapo ndipo walipokosea. CLOUDS ni wadogo sana mbele ya “Nahodha wa Meli” na mbele ya “THE UNTOUCHABLE”.

Kuna kitu watu wengi hawakijui, hata siku moja huwezi kuwa “Enemy of the State” na ukaibuka mshindi, “always the State wins”. Wazungu wana msemo wao; “There are a thousand ways of killing a dog”

Makonda siyo mtu wa mchezo mchezo, Makonda anajua anachokifanya, tena uzuri ni kwamba Makonda yupo chini ya Nahodha katili, shupavu, asiyeangalia wala kusikia cha mtu yeyote yule. Nahodha huyu yupo tayari kumtosa baharini baharia wake yeyote yule atakayeonekana hataki kufuata maelekezo yake. Huu ni msimamo dhabiti hasa, kwani ukiwaacha mabaharia wasiotaka kukutii, unaweza kuhatarisha usalama wako na wa Meli unayoiongoza.

Ushauri wangu kwa wale wote wanaofanya kazi chini ya Rais Magufuli, ni lazima wafanye kama anavyotaka yeye ama sivyo kama hawataki, waachie ngazi wenyewe.

Binafsi namuunga mkono Rais Magufuli katika kazi yake.

Chapa kazi Magufuli, chapa kazi wala usitetemeke!
😆😆😆😆
 
Back
Top Bottom