Son of Gamba
JF-Expert Member
- Oct 26, 2012
- 4,720
- 6,956
Rais Magufuli amethibisha kuwa yeye ni mtu makini, mwenye msimamo usioyumba, huyu ni Amiri jeshi mkuu hasa, mwenye maamuzi magumu, Rais asiyeangalia sura ya mtu wala ukubwa wa jina la mtu, wala cheo chake, wala historia yake.
Ukiingia kwenye kumi na nane zake, hakuachi, anakumaliza. Watoto wa mjini wanasema; anakuchinjia baharini!
Wengi waliokwenda kinyume na matakwa ya Rais Magufuli wameishia kutumbuliwa bila kujali majina yao wala historia ya familia zao. Mkumbuke Anne Kilango Malecela, Kitwanga na leo ilikuwa zamu ya Nape Nnauye, kama utani vile, ametumbuliwa kwa kwenda kinyume na matakwa ya Boss wake.
Kosa kubwa la Nape ni kujiingiza kwenye vita isiyomuhusu na kuanza kuropoka. Nape hakujua kama Makonda ni “The Untouchable one”, hata siku moja huwezi kusema na kuropoka kuwa “The Untouchable” ameinajisi wizara yako! Hili ni kosa kubwa sana.
Mtu mmoja aliwahi kusema; if you can’t fight them, join them. Licha ya kuwa Nape ni mtoto wa mjini, lakini hakulitambua hili. Sasa amebakiwa na kiti chake cha ubunge tu.
Ushauri wangu kwa Nape, achunge sana mdomo wake; sababu this WAR is not over yet. This is just the beginning of another Episode! Mtoto wa Kimakonde, haya ni maji mazito sana kwako! Ukiendelea kubwabwaja, unaweza kupoteza sifa ya kuteuliwa na chama chako kugombea ubunge ikifika 2020. Kumbuka kuwa mwenyekiti wa chama ni huyu huyu nahodha asiyeangalia sura, John Pombe Magufuli!
Baada ya Nape, sasa wamebakia akina Gwajima na CLOUDS MEDIA. Hawa hakuna namna watachomoka mbele ya Mkuu! Hivi sasa wanachukuliwa “timing” tu. Mkuu ni kama “Sterling” kwenye hii movie na siku zote “Sterling hauwawi” lazima atashinda tu.
Kwa mbali nawaona CLOUDS wakifutika kwenye ramani ya Tanzania. CLOUDS wametumbukia kwenye vita wasiyoweza kushinda. Nahodha wa meli aliwapenda sana hapo mwanzo, lakini walipomchafua “The Untouchable One” hapo ndipo walipokosea. CLOUDS ni wadogo sana mbele ya “Nahodha wa Meli” na mbele ya “THE UNTOUCHABLE”.
Kuna kitu watu wengi hawakijui, hata siku moja huwezi kuwa “Enemy of the State” na ukaibuka mshindi, “always the State wins”. Wazungu wana msemo wao; “There are a thousand ways of killing a dog”
Makonda siyo mtu wa mchezo mchezo, Makonda anajua anachokifanya, tena uzuri ni kwamba Makonda yupo chini ya Nahodha katili, shupavu, asiyeangalia wala kusikia cha mtu yeyote yule. Nahodha huyu yupo tayari kumtosa baharini baharia wake yeyote yule atakayeonekana hataki kufuata maelekezo yake. Huu ni msimamo dhabiti hasa, kwani ukiwaacha mabaharia wasiotaka kukutii, unaweza kuhatarisha usalama wako na wa Meli unayoiongoza.
Ushauri wangu kwa wale wote wanaofanya kazi chini ya Rais Magufuli, ni lazima wafanye kama anavyotaka yeye ama sivyo kama hawataki, waachie ngazi wenyewe.
Binafsi namuunga mkono Rais Magufuli katika kazi yake.
Chapa kazi Magufuli, chapa kazi wala usitetemeke!